Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

ee wale wadogo ndo watamu ila wakubwa radha yake sijui nikuelezee vp,ok ukiwa mdogo uliwahi kupika maembe mabichi hadi yakaiva na ukala,ile ladha yake havijaachana sana na nyama ya nyoka
Wee jamaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mambo vipi wanaJF natumai mko poa. Kwenye misosi kuna kuwa na kile chakula una hamu nacho au tu umekuta sehemu kimepikwa kwasababu hujawahi kula unaamua kula huo msosi kwa mara ya kwanza lakini chakula hicho kina kushinda kabisa hata kukupelekea kujisikia vibaya.

Mimi miaka ya nyuma nilikuwa nasikiaga kuhusu supu ya kongoro siku na mimi nikaamua nijue ikovipi hiyo supu nikaenda sehemu nzuri tu nikaulizia nikaambiwa ipo basi nikaletewa pale nikaanza kuipiga lakini kidogo tu nilikula kama vipande viwili tu vya ile nyama nikajisikia kuchefuchefu vibaya sana hata hiyo nyama kumeza haimezeki nikaacha supu karibia yote pale hadi leo hii sitaki tena kusikia kuhusu hiyo supu

Nyingine hii ilikuwa ni juisi ile ya rozela nilikuta imetengenezwa sehemu nikanywa glasi moja ilikuwa na ladha nzuri tu lakini baada ya hapo nilijisikia vibaya sana kama kizunguzungu mara kama mwili unataka ku vibrate mara jasho linatoka japo kulikuwa na feni yaani ilikuwa ni shida mpaka leo nikiiona hiyo juisi naipitia mbali kabisa. Hata juisi ya miwa ilinishinda kabisa ni bora nile muwa kama muwa

Vipi kwa upande wenu wadau ni kitu gani ulikula lakini baada ya hapo hutaki tena kukila.
Mbususu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wali na kuku wa sesame, ni cha kichina.
 
ee wale wadogo ndo watamu ila wakubwa radha yake sijui nikuelezee vp,ok ukiwa mdogo uliwahi kupika maembe mabichi hadi yakaiva na ukala,ile ladha yake havijaachana sana na nyama ya nyoka
Aisee
 
Pizza na Macroni Sirudii tena, Macroni nilikuta kwa Buffee nkabeba nitoe ushamba kumbe ovyo, Ila Pizza iko overated
Hujala Mexican Piza wew.. Mimi Bugger naona ndo iko over rated kabisaa!!
 
Back
Top Bottom