Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Vipo, loshoro chakula cha wamasai mahindi ya kande wana mix na mtindi, ngararimo ni makande ya uchagani mahindi mazima + maharage wanapika na magadi hayo mahindi, anjero ni chapati za maji za wasomali au ethiopian
Chakula cha Wahabeshi kinaitwa Injera na sio anjero
 
Njugumawe wakati nakuwa kama imepikwa ilikuwa nakula basi tu ili nisife ila sahivi naichakata vibaya mno. (Njugu mawe kwa ubwabwa)

Kunde na choroko sipendi hata kuviona
Kunde, choroko, njugumawe, maharage ni vyakula vitamu mno vikipata mpishi mzuri na vina faida nzuri mno mwilini.

Hivyo nikipata na wali, nafurahia huo mlo
 
Cabbage [emoji3055] sitaki hata kuiona aisee nachukia hata harufi yake!,ila cha kushangaza nilivyokuwa Mtoto nilikuwa naipenda sana
 
Kunde, choroko, njugumawe, maharage ni vyakula vitamu mno vikipata mpishi mzuri na vina faida nzuri mno mwilini.

Hivyo nikipata na wali, nafurahia huo mlo
Choroko nazi kwa Wali nazi kuwe na rosti flani hivi pembeni,

Aisee nitakula hadi nifukuzwe [emoji39]
 
Wazee mimi nakulaga kila kitu aisee hakuna kinachonikera, kinachonikataa wala kunipa allergy. Pia sijawahi tapika wala kupata kichefuchefu tangu utotoni nilipojitambua.. kutokana na hivyo huwa naona kama siko sawa kwa namna flani.. seriously, kuna mwenzangu humu?
 
Kuna matunda Zanzibar kubwakubwa hivi kwa nje kama lina miiba lina harufu mbaya kama utumbo uliooza,nilitapika kisa ile harufu.......sijui jina ila lina bei kubwa.
 
Back
Top Bottom