Chakula gani unachokipenda na usichokipenda?

Napenda mboga za majani, vyakula vyenye madini chuma na matunda
 
Mi sipendi wali maharage, ugali maharage, Napenda sana ndizi nyama na ndizi samaki lakini sio ndizi wa kilimanjaro
 
Napenda ugali dagaa samaki kuku kisamvu matembele figiri mlenda maharage ila nile na ugali dagaa au nile na wali AU na Ugali na samaki wa kukaanga na mboga ya majani. Sipend Makande ndizi viazi mbatata majani ya kunde
 
Napenda: Ndizi-nyama (mshale mgumu), wali, pasta, chapati maji na za kawaida, vitumbua, matunda, mboga mboga kwa sana tena spinach, mtindi, zege, rolex ya Uganda, nyama ya kuku na ya kanga, kachumbari, samaki wa salmon, johari na sato vilevile matunda karibia yote.

Aste aste: Ugali, pilau, nyama ya ng'ombe - naupenda na siupendi hivyo nakula mara chache.

Sipendi: Makande, dona, biryani, mihogo, uyoga, mlenda, maharage, supu, viazi vya kupikwa, nyanya chungu, uji.

Sili kabisa: nyama ya utumbo, mbuzi & kondoo, prawn, shrimp, crab, mussel, lobster, kisusio.
 
Ndizi mzuzu iliyoiva vzr ichomwe, ichemshwe au ikaangwe napenda sana, kinyume ndizi mbichi mzuzu
 
Napenda vyakula vyote isipokua;
1.kitimoto(kutokana na Imani yangu ya dini)
2.Majani ya Kunde
3.Mnafu
 

Yaani vyakula ambavyo hupendi mie ndo napenda kasoro mkate toa siutaki kabisa
 
Napenda Wali na bamia - (bamia likatwe dogo dogo litiwe na nyanya chungu)
 
Basi mie napenda kichuri tu basi, ila sipendi kabichi.
 
Kuna watu humu watasema wanapenda "K" ngoja waje uone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…