Chakula kikidondoka chini kula. Sababu ni hii

Chakula kikidondoka chini kula. Sababu ni hii

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Mfano unakula kitu chochote halafu kwa bahati mbaya kimeanguka, okota na ule. Acha kuogopa bakteria na wadudu wengine hatari kwa sababu wadudu ama bakteria pindi waonapo chakula kimeanguka kwenye mazingira yao hawakifakamii ghafla bila kuunda tume ya uchunguzi.

Kwanza kabisa kuna bakteria atapeleka taarifa makao makuu na kuwataarifu wakubwa kwamba kuna kitu kimeanguaka kwenye mazingira yao. Kisha kikao cha dharura kitaitwa kwa zile sekta nyeti kama za ulizi afya, uchumi na ustawi. Sasa hapa inategemea kama wapo karibu na makao na sio nje kwa ziara ama vikao.

Baada ya hapo kikao hiko cha dharura kitaunda tume ya kwenda kuchunguza ni nini kilichopo kwenye mazingira yao sambambana vyombo mbalimbali vya ulinzi, mamlaka zao za udhibiti na usalama wa chakula. Hii huchukua muda hadi dakika 70 kisha watatoa ripoti na kisha vigogo hao wa bakteria kuamua sasa kwamba wanaweza tuma wataalamu waende wakiozeshe au kukiharibu ili kwao iwe rahisi kukitumia.

Huu mchakato wote huo hapo juu, wa madakika mengi sana kutekeleza kunakufanya ushindwe kuokota nyama au chakula kukitikisa na kula?

Bakteria hawana pupa kiivyooooo tunavyodhania.

Wao pia wana mamlaka na vyombo vyao vya udhibiti kama TBS, EWURA n.k
 
Na kuna bakteria wengine wao ni kulalamika na kugoma kama chadema hvy wanachelewesha maamuzi kutoka juu.

Pia kuna bakteria wengine wao ni uchawa na kujipendekeza kwa wakubwa kama ccm hawa watajifanya wajuaji wa mambo hvy ni kuwatupia chakula chenye sumu ili wakafie mbele hukooooooo.
 
Bakteria hao labda wa ulaya mkuu
Bakteria wa bongo kabla hakijafika chini wenyewe washakipandia ndege wanakifatia huko huko washuke nacho 😀
Inategemea na maeneo. Kama dar pale wapo fasta sana na makao makuu ni dodoma parefu pia
 
Dondosha juu ya kinyesi ufute ule tuone kama hutoharisha.
 
Back
Top Bottom