Chalamila aanza kwa kishindo! Atumia usafiri wa bajaj

Hiyo Bajaj ni mali ya Ilala boma?
Haijalishi ni ya nani bali tambua usafiri wowote wa kawaida ikitokea kiongozi anatakiwa autumie ima ni wa mtu aliye ndani ya mfumo asiyetambuliwa na wanaomzunguka ama unamilikiwa na Taasisi ya Serikali.

Chukua hii 👇:

Mara nyingi Taxi, Bajaj na Pikipiki ukiona anapanda Kiongozi huwa ni za PT Idara ya I.
 
Kichaa kapewa rungu.. Disco limeingia mmasai na sime
 
Haya maigizo na sarakasi hatutaki kabisa.

Hawa akina Chalamila na CCM ni waigizaji na opportunists.
Ndio mfumo wetu wa utawala ulivyo; hao ndio level yetu ya watawala ambao huitwa "waheshimiwa".
Hawa ndio zao la Katiba mbovu ya sasa yenye mapungufu makubwa na yenye kuligharimu Taifa kila siku.

Yatosha maigizo na ulaji.

Sasa tunataka Katiba Mpya! Tunataka utawala bora, uwajibikaji, maendeleo na uhuru .
 
Huyu 'Ninja Turtle' ana vituko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…