Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila siku ya leo akiwa kwenye mkutano na baadhi ya maaskari, ameliomba Jeshi La Polisi kuisaidia serikali kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Chalamila amesema kuwa analiomba Jeshi La Polisi kushugulika na watu wote watakaopinga matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuongeza kuwa uwepo wa sera ya 4R ya Rais Samia haimaanishi kuwa maji ya washawasha na mabomu ya machozi havitatumika
Soma pia: RC Chalamila: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utafanyika katika Mitaa yote 564 ya Dar kwa Uhuru na Haki
"Tunakumbushana kuwa Taifa letu sasa Tarehe 27 mwezi wa 11 na hapa hatuombi vyombo vya dola vikasaidie kubadilishe matokeo hapana. Tunaomba vyombo vya dola viwe imara zaidi ili matokeo yatakapotangazwa ili kwa mtu ambaye hatakubali na ni kweli amefeli basi ashughulikiwe kwa mujibu wa taratibu"
Aliongeza kwa kusema:
"Unataka mabadiliko kuna muda lazima ka mkono ka nguvu kanahitajika. Kwa hiyo hizi 4R za Mheshimiwa Rais ambazo zinatajwa watu wasitafsiri kama bunduki haipo, bomu halipo, maji ya washawasha hayapo. Huwezi kujitenga namna hiyo"
Una maoni kuhusu kauli hii ya mkuu wa mkoa? Binafsi naona imekaa kimtego?