Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kuna baadhi ya mambo wana madaraka nayo moja kwa moja kwa niaba ya raisi,isipokuwa kutengua teuzi na baadhi ya maagizo ambayo wameelekezwa au ambayo yapo nje ya uwezo waoKwa hiyo wanapitia amri za ajabu ajabu wakati mwingine hata hivyo kitu hakielewi ana kuwa ametumwa na Raisi au anevuka mstari , unajua uongozi ni zaidi ya hicho cheo au Jina la nafasi iliyo nayo. Mfano unamgombeza Daktari, au Yule aliye Mwambie Dada ya watu Mimi Nina Mke mzuri la la la , hapo anamuwakilisha Raisi, Kwa hiyo taratibu zinawekwa ili kupunguza au kuondoa nafasi za MTU kwenda nje ya mstari. Au kama suala la Marehemu Kleruu na Mzee Mwamwindi huko Iringa , ukasema Kleruu alitumwa au alikuwa anamuwakilisha Raisi ipasavyo. Au Yule Dereva anayatumia utambulisho wa RC , kupata vizawadi anakuwa ana kuwakilisha Raisi.
Majukumu yake kama mwakilishi wa Raisi ni kujua Mipango ya serikali ktk sehemu husika na kiwakumbushia malengo ya sirikali, na kupata mrejesho wa kufikia malengo hayo. Kusikiliza kero za wananchi , Kwa ushahidi wa kutosha kushauri Mkuu wa idara husika kufuatilia Jambo hilo au kulitatua tatizo hilo. Ikitokea kwamba afisa fulani mara mara matatizo yake yanajirudia rudia ndio kuomba mamlaka husika kumchukulia hatua za kinidhamu, na kwakuwa wao wana fursa ya kuongea na mawaziri ni kuwa Shauri Waziri husika kuchukua hatua ya kimwadhibu au kumuhamisha mfanyakazi huyo. Waziri husika asipochukua hatua , hapo Mkuu wa Mkoa atamtaarifu Raisi, ambaye ana mudu Waziri na sio RC kuvimbishiana kifua na Waziri au IGP au Hakimu
Ila usiniambie kwamba wao ni wenyeviti wa kamati za usalama halafu washindwe kusimamia usalama na kutoa maagizo vyombo vya dola visichukue hatua
Ila nakiri na kukubaliana na wewe kuna baadhi madaraka yapo juu ya uwezo wao na kujikuta miungu watu,wanadharau watu na kudhalilisha watu,,hiyo sio sawa na hapo hawamwakilishi raisi vizur