LGE2024 Chalamila aliagiza Jeshi La Polisi kuwashughulikia wananchi watakaopinga matokeo ya Uchaguzi ujao wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Polisi ni chombo cha Dola Wana mpaka zao za Uongozi, sio kila mtu awape maelekezo, DC na RC hawapo kwenye taratibu zao zaidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kumpa Taarifa IGP kama kuna mapungufu kwenye kituo kimojawapo cha Polisi. Rejea kauli ya Mzee Warioba hivi karibuni
 
This is too much! Dharau kubwa sana Kwa wananchi!! Aaaaaghrrrrr!!!!!!
 
🤔😭
 
CHADEMA susieninuchaguzi huu
 
Ubarikiwe sana kwa maneno ya hekima na busara kwa jamii.
 
Changamoto inakuja baada ya CHADEMA kuamua kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa!
Hapa imeshaleta hofu kwa CCM kuwa kinaweza kupoteza viti vingi kwa CHADEMA, kilichobaki ni kutumia Polisi kutoa vitisho! Vitisho ambavyo huenda vitawaogopesha hata wananchi kutokwenda kupiga kura!
Nadhani CCM ilikuwa inangoja maamuzi hayo ambayo huenda waliamini matokeo yangekuwa mteremko kama CHADEMA wasingeshiriki uchaguzi huo.
CCM haina option nyingine ya kushinda uchaguzi zaidi ya kutumia vitisho na nguvu kupora uchaguzi.
RC hakusema kwa bahati mbaya!
 
OGOPA NCHI IKIWA NA WAJINGA WENGI WANAWEZA KUMCHAGUA RAIS
 
Anawashwa huyo Sio bure
 
Kweli kabisa eti "kuisaidia Serikali" Ikoje hii wadau??
Kuwatishia wananchi
 
Plato alikuwa na mtazamo wa kushuku demokrasia, akiamini kwamba inaweza kuongozwa na watu wasio na hekima, na hivyo kupelekea kuchukua maamuzi mabaya kwa ajili ya jamii. Aliona demokrasia kama mfumo ambapo wengi wasio na maarifa au elimu wanaweza kuchukua madaraka na kufanya maamuzi kwa ushawishi wa hisia badala ya mantiki. Hii ni kwa sababu Plato aliamini kwamba umma unaweza kudanganywa kirahisi na viongozi wenye maslahi binafsi.
Kwa kuhusianisha mtazamo wa Plato na hali ya viongozi walioko madarakani hivi sasa nchini Tanzania hasa kutumia silaha na nguvu ya jeshi la polisi ili kuwatisha wapiga kura kukubaliana na matokeao hata kama yana dosari, tunaweza kusema kwamba hii ni ishara ya hatari ya demokrasia isiyosimamiwa vyema, kitu ambacho Plato alikuwa akikihofia. Katika mazingira kama haya, ambapo viongozi wanatumia nguvu kuimarisha nafasi zao, inaonyesha kutokuwepo kwa maadili ya kweli ya kidemokrasia na badala yake, kuonesha udhaifu wa mfumo. Ni udikteta uliovaa sura ya demokrasia, ambapo sauti ya wapiga kura haina maana na viongozi wanatumia nguvu ili kulazimisha matokeo wanayotaka, hata kama yana dosari.
Katika demokrasia ya kweli, maamuzi yanapaswa kufanywa na watu kwa uhuru bila hofu ya kulazimishwa. Plato aliona hali hii ya kutumia nguvu kama ishara ya uharibifu wa mfumo wa demokrasia, ambapo badala ya kuheshimu sauti ya umma, viongozi wanatumia vitisho kudhibiti matokeo.
Hii inathibitisha hofu kwamba bila uongozi wa watu wenye hekima, demokrasia inaweza kugeuka na kuwa mbaya zaidi kuliko mifumo mingine ya utawala, hasa pale inapotekwa na wale wenye uwezo wa kutumia nguvu kwa maslahi yao binafsi.

Pascal Mayalla

P
 
Hivi huko DSM mapori pia yapo? Kwa maana CCM wakati wa uchaguzi huwa wanakwenda maporini
 
hii maana yake yeye yupo kwa ajili ya chama chake na sio wananchi kama tunavyoaminishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…