LGE2024 Chalamila aliagiza Jeshi La Polisi kuwashughulikia wananchi watakaopinga matokeo ya Uchaguzi ujao wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kashapewa maelekezo kutoka juu
 
CCM na viongozi wake wakisha wekwa ofisini na madarakani wanageuka kuwa majahili na kututeka nyara raia.

Wakidhani wao pekee ndiyo wenye haki ya maamuzi nchi hii iendeje. Wanasahau sisi ndiyo waajiri wao tunawalipa mishahara na marupurupu.

Uongozi ni kushawishi hoja zako kiongozi siyo kuburuta raia, kama umekosa uahawishi wa hoja jiuzulu badala ya kutumia mabavu dhidi ya tajiri zako tunaokulipa mshahara

Hata mishahara na marupurupu yenu viongozi ilitakiwa msikilize raia wanasema kodi zao zitumike vipi, magari ya aina gani sisi raia tunataka mnunuliliwe. Kodi zetu mmeziteka nyara kwa kufanya matumizi ya anasa kununua gari za kifahari ma-V8.

Maeneo yaliyochagua wapinzani mnasema hamtapeleka hela wakati raia wote wanakatwa kodi bila ubaguzi vipi kwenye matumizi mnabagua kwa kusema hatuwajengei barabara kwa kuwa mmechagua upinzani.

Pesa za kodi mnasema ametoa mama, kweli kuna kiongozi nchi anaweza kuwa tajiri kuliko nchi, hakuna kiongozi wa Dola au nchi aliye na utajiri kuliko kodi zinazokusanywa iwe Marekani, Omani, Australia, Tanzania, Kenya n.k


View: https://m.youtube.com/shorts/JxhZ3K-gXzU
 
Kwani wagombea sio wananchi?
Halafu yeye ametumia Sheria gani kutoa tamko?
Sio kwamba amelewa madaraka mpaka anatoa Siri za bosi wake
 

Huyu si ndio alitishia kuwalipua mabomu wananchi wabeya Kama watakataa matokeo.
 
TOKA MAKTABA :

Mwezi Machi 2018 : Rais na viongozi wake wadhibitiwe


Watu hawataki kuwa mateka wa kikundi cha watu kwa kuwatisha kupitia chama dola. Chama dola siyo chama cha kweli cha kisiasa maana hakina ushawishi bali kinatumia dola kutisha watu...


View: https://m.youtube.com/watch?v=RiOTQa88chQ
Watanzania wanataka Maendeleo ndani ya uhuru, demokrasia ndani ya uhuru, uchaguzi huru na wa haki ... chama cha ukombozi kujigeuza chama tawala wakati tumetoka kutoka ukoloni ni dhana potofu, chama kinatakiwa kinachoongoza siyo kutawala maana hatupo ndani ya ukoloni ...
 
H
Huyu jamaa ni mbwa. Hajielewi hadi anae mlisha atoe amri
 
Hivi unajua kwamba RC na DC wanamwakalisha Raisi katika mamlaka yao?
 
Mathayo 10
24 Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake.
 
Huyu kuharisha ni kawaida yake . Actually, huyu ni BATA
 
Huyu mpumbavu akishavuta bangi anajiona yeye ndiye Rais wa nchi hii, hili domo lake lililokauka kwa kuvuta bangi linamuingiza matatani siku zote, na Rais alishamuonya kuchunga mdomo wake. Mara nyingi watu wenye vichwa modeli ya huyu mjinga wana shida sana hasa ukichanganya na bangi.
 
“Nataka mfahamu ndugu zangu
kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi
kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na
tutakwisha kweli.”

Jakaya Kikwete.
 
Tuna RC kiherehere kweli kweli hadi anafanya kazi amabazo si zake!! Aombe kuwa waziri wa TAMISEMI tujue moja.
 
Hivi unajua kwamba RC na DC wanamwakalisha Raisi katika mamlaka yao?
Kwa hiyo wanapitia amri za ajabu ajabu wakati mwingine hata hivyo kitu hakielewi ana kuwa ametumwa na Raisi au anevuka mstari , unajua uongozi ni zaidi ya hicho cheo au Jina la nafasi iliyo nayo. Mfano unamgombeza Daktari, au Yule aliye Mwambie Dada ya watu Mimi Nina Mke mzuri la la la , hapo anamuwakilisha Raisi, Kwa hiyo taratibu zinawekwa ili kupunguza au kuondoa nafasi za MTU kwenda nje ya mstari. Au kama suala la Marehemu Kleruu na Mzee Mwamwindi huko Iringa , ukasema Kleruu alitumwa au alikuwa anamuwakilisha Raisi ipasavyo. Au Yule Dereva anayatumia utambulisho wa RC , kupata vizawadi anakuwa ana kuwakilisha Raisi.
Majukumu yake kama mwakilishi wa Raisi ni kujua Mipango ya serikali ktk sehemu husika na kiwakumbushia malengo ya sirikali, na kupata mrejesho wa kufikia malengo hayo. Kusikiliza kero za wananchi , Kwa ushahidi wa kutosha kushauri Mkuu wa idara husika kufuatilia Jambo hilo au kulitatua tatizo hilo. Ikitokea kwamba afisa fulani mara mara matatizo yake yanajirudia rudia ndio kuomba mamlaka husika kumchukulia hatua za kinidhamu, na kwakuwa wao wana fursa ya kuongea na mawaziri ni kuwa Shauri Waziri husika kuchukua hatua ya kimwadhibu au kumuhamisha mfanyakazi huyo. Waziri husika asipochukua hatua , hapo Mkuu wa Mkoa atamtaarifu Raisi, ambaye ana mudu Waziri na sio RC kuvimbishiana kifua na Waziri au IGP au Hakimu
 
Atashindwa vibaya sana
 
Wanatumia dola kubaki kuongoza Dola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…