Pre GE2025 Chalamila aonywe, asilidharaulishe Jeshi

Pre GE2025 Chalamila aonywe, asilidharaulishe Jeshi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe unaingea kama nani, yeye ni mwenyekiti wa usalama wa dar kuna maandamano huoni wakifanya usafi watazuia waandamanaji
Why if amri imetoka kwa mama? Think big mkuu usifikiri mwisho wa dar ni urafiki
 
Dar ndio inaongoza tanzania kila kitu.....awekwe mtu anaejielewa
Dar ni mkoa mgumu kuongoza kila kigogo anataka asikilizwe kwenye kuendesha mambo yake.

Mkoa wa lawama, mkoa wa maelekezo ukiwa mjuaji Sana ni kheri uwe na baraka zote kutoka juu.

Au uondolewe kwa kushindwa kula na kipofu.
 
Akili ni kujitokeza kuandamana tarehe.24 zporojo za jf hazitakusaidia.
Ahahahahha nashangaa analeta kelele humu na jina lake bandia.

Hatuko mbali, tarehe 24 kaandamane basi! Hapo ndipo ataonesha kuwa ana akili na fikra pevu!
 
Chalamila; Bia bila mziki ni kama juisi

Profesa janabi; unywaji wa bia hupanua na kuharibu moyo.
 
Wapi jeshi lilipo dharaulishwa, wale sio maraia kama wewe wamefundishwa kutii amri, wewe ndio unaleta uraia wako hapa, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameelezea kile kamati imeona ili kupambana na kipindupindu si budi kufanya usafi.

Ila jeshi ndio limejidharaulisha. Ndio maana wameamriwa tarehe 24 wakazibue chemba za mavi kariakoo.
 
Majukumu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzanua, na maheshi mengune yote, yameainishwa kisheria.

Ni Amiri Jeshi Mkuu pekee ndiye anaweza kulielekeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya shughuli nyingine nje ya shughuli ya msingi, kama kuna dharula, na anaona kuna haja ya kufanya hivyo. Mamlaka hayo anayo Amiri Jeshi Mkuu, siyo Chalamila wala Mkuu wa Mkoa mwingine yeyote. Wakuu wa mikoa kuwa wenyeviti wa kamati za Ulinzi na usalama mikoani mwao, haimaanishi wamekuwa wakuu wa majeshi yote yaliyopo mikoani mwao.

Tusiwafanye askari wa JWTZ kuwa ni watu wa kupewa amri na kila mtu. Tukiruhusu upuuzi wa namna hiyo kuendelea, kuna siku Wakuu wa Wilaya nao watawapa amri askari kufagia ofisi zao. Baadaye na watendaji wa kata watawaamrisha askari waliopo kwenye maeneo yao ya kiutawala kwenda kufagia maeneo ya shule za msingi.

Kama tunaona ni busara, kazi mojawapo ya kila jeshi ni kufanya usafi wa miji, basi mswada upelekwe Bungeni ili kubadilisha au kuongeza majukumu ya msingi ya majeshi yote kuwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye miji. Na hilo likifanyika, Wizara ya TAMISEMI itoe maelekezo kwa majiji, maspaa na halmashauri za miji kufuta kandarasi zote zilizoingiwa na makampuni ya kufanya usafi kwa sababu kazi hiyo sasa ni ya JWTZ, Police, Mgambo na JKT. Na hilo litaifanya Tanzania kuwa nchi ya pekee na ya ajabu iliyoamua kutothamini kazi ya askari wake.

Chalamila anathubutu kueleza kuwa magari ya JWTZ ambayo hayajatengenezwa rasmi kwaajili ya kusomba takataka, eti tarehe 23 na 24 yatatumika kusomba takataka. Yaani magari ambayo huwa yanatumika kubeba askari na mizigo mbalimbali yakatumike kubeba kila aina ya takataka vikiwemo vinyesi vinavyotupwa kwenye mifuko ya plastic, halafu gari hilo hilo kesho yake liwabebe askari, tena wakati ambao kipindupindu kinaendelea kupiga hodi mikoa mbalimbali!

Ushauri: Siasa zisitupofushe kiasi cha kukosa hekima. Rais utakuwa umelipa heshima ambayo jiji la Dar es Salaam linastahili kama ukiwapa Mkuu wa Mkoa ambaye anaendana na hadhi ya jiji la Dar es Salaam. Aliyepo, bila kupepesa macho, viatu vya ukuu wa mkoa ni vikubwa mno kwake. Labda kuna mahali anafaa, lakini siyo kwenye nafasi zinazohitaji hekima.
Kuna Makampuni ya Usafi yanafanya usafi kwa mkataba. Hadi huko serikali za mitaa hizo kampuni zipo.
Anaposema Jeshi litafanya usafi huku ni kulidharau kabisa Jeshi.
Yaani Jeshi hili ambalo kipindi kile cha migomo ya Madaktari lilikua likiingilia kati kwa kwenda kuokoa msisha ya wananchi kwa kwenda kubeba jukumu la kutibu wagonjwa mahospitalini, leo hii limeshushwa hadhi hadi kukabidhiwa mafagio na makopo ya chooni ili likafanye usafi???
 
Haya peleka komwe lako tarehe 24 / Januari ndiyo utajuwa maana ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa

Hiyo mwenyekiti wa kamati ni mjinga Sana, Yani anamrisha jeshi likazibue chemba za mavi kariakoo tarehe 24 baadala ya kulinda mipaka ya nchi. Tukivamiwa na adui atajiteteaje.
 
Ila Tanzania Ina uhaba wa Viongozi. Yani wameiingiza JWTZ kwenye ujinga wa siasa.
 
Back
Top Bottom