Pre GE2025 Chalamila aonywe, asilidharaulishe Jeshi

Pre GE2025 Chalamila aonywe, asilidharaulishe Jeshi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jeshi lenyewe linapenda kudhalilishwa, sasa kama hata RC chenjeu kama Chala boy anaweza kulipa tu amri na lenyewe likatekeleza unafikiri kuna nini hapo.
 
tatizo sio chalaboy tatizo ni udhaifu wa chadema, chadema wadhaifu sana hawanaga plan b yaani maccm yakitumia nguvu tu chadema wanakimbia ulingoni hadi chadema watakapoacha kukimbia ulingo nakupambana na woga wao ccm katiba wataitema ndani ya mwaka mmoja. kwasasa chadema ni kama watoto wanao ogopa giza.
 
Haya ndo madhara ya chama cha siasa kushika hatamu kikazidi serkali ukuu.
Hakuna namna nchi itabadirika namna ya kutawalana kama ccm haitakufa na kuzaliwa vyama vyenye uwiano wa kupambania dola.
 
tatizo sio chalaboy tatizo ni udhaifu wa chadema, chadema wadhaifu sana hawanaga plan b yaani maccm yakitumia nguvu tu chadema wanakimbia ulingoni hadi chadema watakapoacha kukimbia ulingo nakupambana na woga wao ccm katiba wataitema ndani ya mwaka mmoja. kwasasa chadema ni kama watoto wanao ogopa giza.
Tatizo siyo Chadema, tatizo ni Watanzania.

Raila Odinga maandamano yake anayoitisha huwa yanapigwa marufuku lakini Wakenya wenyewe wako tayari na huwa wanaingia barabarani, Watanzania tumejaa unafki tu.
 
Ajabu saa hii eti "Ruto naye ni role model wa Hawa mbwa wa ccm". Nchi ina wajinga wengi sana hii.
Huyo ni roleofel wenu ,Sasa alivyotembeza kichapo kwa Udinga ndivyo Samia atatembeza kichapo Kwa kina Mbowe na matapeli wenzao.
 
Huyo ni roleofel wenu ,Sasa alivyotembeza kichapo kwa Udinga ndivyo Samia atatembeza kichapo Kwa kina Mbowe na matapeli wenzao.
Tapeli ni yule aliyeikabidhi bandari kwa wajomba zake waarabu wenzake .
 
Jukumu la Kwanza la Jeshi ni kulinda katiba, sasa kinachopaswa kufanywa na Jeshi ni kumuonya Chalamila anayevunja katiba.
20240114_121636.jpg
 
Mpaka jeshi liingie mitaani kufanya usafi ina maana kama raia tumefeli kwenye kuweka mifumo ya usafi katika mazingira yetu.

Chalamila anatuambia kwamba yeye kama mkuu wa mkoa ameshindwa kusimamia jambo dogo tu la usafi katika jiji lake mpaka akaomba msaada wa jeshi.

Sasa kama hawezi simamia usafi anasubiri nini hapo ofisi ya mkuu wa mkoa si aondoke atuachie ofisi yetu ya uma?

Maana ni yetu sisi wananchi na sio yake wala ya mama yake.
 
Majukumu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzanua, na maheshi mengune yote, yameainishwa kisheria.

Ni Amiri Jeshi Mkuu pekee ndiye anaweza kulielekeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya shughuli nyingine nje ya shughuli ya msingi, kama kuna dharula, na anaona kuna haja ya kufanya hivyo. Mamlaka hayo anayo Amiri Jeshi Mkuu, siyo Chalamila wala Mkuu wa Mkoa mwingine yeyote. Wakuu wa mikoa kuwa wenyeviti wa kamati za Ulinzi na usalama mikoani mwao, haimaanishi wamekuwa wakuu wa majeshi yote yaliyopo mikoani mwao.

Tusiwafanye askari wa JWTZ kuwa ni watu wa kupewa amri na kila mtu. Tukiruhusu upuuzi wa namna hiyo kuendelea, kuna siku Wakuu wa Wilaya nao watawapa amri askari kufagia ofisi zao. Baadaye na watendaji wa kata watawaamrisha askari waliopo kwenye maeneo yao ya kiutawala kwenda kufagia maeneo ya shule za msingi.

Kama tunaona ni busara, kazi mojawapo ya kila jeshi ni kufanya usafi wa miji, basi mswada upelekwe Bungeni ili kubadilisha au kuongeza majukumu ya msingi ya majeshi yote kuwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye miji. Na hilo likifanyika, Wizara ya TAMISEMI itoe maelekezo kwa majiji, maspaa na halmashauri za miji kufuta kandarasi zote zilizoingiwa na makampuni ya kufanya usafi kwa sababu kazi hiyo sasa ni ya JWTZ, Police, Mgambo na JKT. Na hilo litaifanya Tanzania kuwa nchi ya pekee na ya ajabu iliyoamua kutothamini kazi ya askari wake.

Chalamila anathubutu kueleza kuwa magari ya JWTZ ambayo hayajatengenezwa rasmi kwaajili ya kusomba takataka, eti tarehe 23 na 24 yatatumika kusomba takataka. Yaani magari ambayo huwa yanatumika kubeba askari na mizigo mbalimbali yakatumike kubeba kila aina ya takataka vikiwemo vinyesi vinavyotupwa kwenye mifuko ya plastic, halafu gari hilo hilo kesho yake liwabebe askari, tena wakati ambao kipindupindu kinaendelea kupiga hodi mikoa mbalimbali!

Ushauri: Siasa zisitupofushe kiasi cha kukosa hekima. Rais utakuwa umelipa heshima ambayo jiji la Dar es Salaam linastahili kama ukiwapa Mkuu wa Mkoa ambaye anaendana na hadhi ya jiji la Dar es Salaam. Aliyepo, bila kupepesa macho, viatu vya ukuu wa mkoa ni vikubwa mno kwake. Labda kuna mahali anafaa, lakini siyo kwenye nafasi zinazohitaji hekima.
Mi nawaza governor wa NyC aliite jeshinla America liende kufanya kazi ya usafi...Daah Mwafrika ni Mwafrika tu
 
Serikali inajiaibisha kwa vitu vidogo sana, hivi Mfano Chadema wakisema maandamano ni tarehe 20 January huyo mkuu wa mkoa ataamuru tena jeshi lifanye usafi hiyo tarehe 20?
 
t
Tatizo siyo Chadema, tatizo ni Watanzania.

Raila Odinga maandamano yake anayoitisha huwa yanapigwa marufuku lakini Wakenya wenyewe wako tayari na huwa wanaingia barabarani, Watanzania tumejaa unafki tu.
tatizo ni chadema wakenya wanaongozwa na vyama visivyoyumbishwa, nusu ya viongozi wa chadema ni ccm watupu na hawako tayari kulipia gharama ya tume huru na katiba, kamwe hawatapata vitu hivi wakiwa wanapigwa na ac, ili wapate lazima viongozi wa chadema wawe jela au uhamishoni, kumbuka wanaoilinda katiba hii ni wezi kuanzia wao hadi wazazi wao.
 
Wapi jeshi lilipo dharaulishwa, wale sio maraia kama wewe wamefundishwa kutii amri, wewe ndio unaleta uraia wako hapa, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameelezea kile kamati imeona ili kupambana na kipindupindu si budi kufanya usafi.
Nasubiri tarehe 24 nimwone captain wa JWTZ na fagio lake kariakoo shimoni - 🤪 🤪
 
Back
Top Bottom