Pre GE2025 Chalamila aonywe, asilidharaulishe Jeshi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Anatenguliwa leo usiku kuamkia kesho trh 15 na Ally Hapi anachukua jukumu la RC
 
Hiyo mwenyekiti wa kamati ni mjinga Sana, Yani anamrisha jeshi likazibue chemba za mavi kariakoo tarehe 24 baadala ya kulinda mipaka ya nchi. Tukivamiwa na adui atajiteteaje.
Hizo jeshini zinaitwa "fatiki", kama hujapitia jeshi huwezi kuelewa
 
Wewe unaingea kama nani, yeye ni mwenyekiti wa usalama wa dar kuna maandamano huoni wakifanya usafi watazuia waandamanaji
Why if amri imetoka kwa mama? Think big mkuu usifikiri mwisho wa dar ni urafiki
Basi atamke kuwa ameyasema hayo kwa maagizo ya Amiri Jeshi Mkuu. Ili na majeshi yote yajue kuwa hiyo ni amri toka kwa Amiri Jeshi Mkuu, siyo Chalamila mropokaji.
 
Ujafikiria Kuna Watu wamemtuma ?
Kama ametumwa na Amiri Jeshi Mkuu basi aseme kuwa ni agizo la Amiri Jeshi Mkuu, siyo tuhisi tu kuwa ametumwa.
 
Ikitoka kwa mama ndo inaanzia kwa mkuu wa mkoa then mkuu wa mkoa ndo anaishusha kwa mkuu wa majeshi? Kwani ni lazima uoneshe upunguani wako?

Wewe ndiyo bure kabisa. Kwa uelewa wako mdogo, unaelewa kuwa Mkuu wa Majeshi yupo chini ya CDF?
 
Kwa ambao hamjui.. mkuu wa mkoa Ni mkuu wa usalama wa mkoa husika hivyo majeshi yote ya mkoa huo yapo chini yake

Siyo kweli. Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti tu wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, lakini siyo mkuu wa vikosi vya majeshi yote yaliyopo mkoani. RC hana uwezo hata wa kuamrisha operesheni ya kipolisi mkoani mwake mpaka kibali kitoke kwa IGP baada ya kushauriana na Rais.

Vikosi vya JWTZ, hivyo vipo mbali kabisa kutoka kwa mamlaka ya RC. RC hana uwezo wa kuamrisha hata platuni ya JWTZ ifanye operesheni yoyote ya kijeshi. Na hiyo imewekwa kwa sababu maalum. Kama vikosi vya jeshi vingekuwa vinapokea amri kutoka kwa wakuu wa mikoa, basi ingekuwa ni rahisi sana kwa mkuu wa mkoa, hata kuipindua Serikali. Fikiria mkoa labda una vikosi 7, vyenye ujuzi mbalimbali na aina mbalimbali za silaha.
 
sio kwamba wanafanya usafi mazee!!!,wanazuia maandamano ya CHADEMA kimtindo!!
 
Nasubir mdahalo.watanzajia wa sasa wamesoma tunataka debate . Tujue is it worthwhile kwendea kuvunjwa miguu au unworthily. Hatutak kuwa mangombe
 
Jeshi lenyewe ingekuwa linajitambua sasa hivi ccm ingekuwa ilishang'olewa kitambo tu
 
Kama kuna wizara yenye wafanyakazi hewa,basi hata huyu anastahili kuhamishiwa huko. Japo ni jambo la kawaida jeshi kusaidiana na wananchi,kama kuna uhitaji,si tangazo au jukumu la RC kulipa jambo hilo muongozo. Ila sasa kama kweli kaongelea na magari yao, hapo amepitiliza kituo. Utawala wa ............
 
M
Mwisho kabisa ungemalizia na busara
 
Wapi jeshi lilipo dharaulishwa, wale sio maraia kama wewe wamefundishwa kutii amri, wewe ndio unaleta uraia wako hapa, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameelezea kile kamati imeona ili kupambana na kipindupindu si budi kufanya usafi.
Kwa hiyo,huyo RC ana uwezo wa kuliamrisha jeshi cha kufanya!? Sahau. Fanya ka utafiti kadogo,hata kwenye ripoti anazopewa,yasiyomhusu hapewi. Hata rais,hawezi kutoa tamko kama hilo bila kuwashilikisha walengwa.
 
Haikwepeki hii kwani ujui mkuu wa mkoa ndie mwenyekiti wa kamati yote ya ulinzi.
Yaani yeye ndie boss wao
 
Haikwepeki hii kwani ujui mkuu wa mkoa ndie mwenyekiti wa kamati yote ya ulinzi.
Yaani yeye ndie boss wao

Kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama haimaanishi yeye ni kamanda mkuu au amiri jeshi kwenye mkoa. Mkuu wa mkoa hana uwezo wa kuamrisha hata platuni moja ya jeshi, achilia2r mbali kikosi kizima.

Mkuu wa mkoa hana hata uwezo wa kuamrisha operesheni ya kipolisi mkoani mwake.

Mkuu wa mkoa au wilaya, anapokuwa mwenyekiti wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama, anakuwa kama mwenyekiti wa kamati ya arusi. Kwa vile uwezo wake unaishia kwenye kuongoza vikao lakini siyo kuwaamrisha makamanda wa majeshi au vikosi vya jeshi.

Vikosi vya jeshi katika kazi zao za kawaida, vinapokea amri kutoka kwa makamanda wa vikosi tu. Na kwa matukio makubwa ni baada ya tangazo la Amiri Jeshi Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…