Chalamila: Dkt. Janabi alisema sukari ni hatari kwa afya, tumieni fursa ya upungufu huu kuachana nayo msipate magonjwa mbeleni

Mshahara mkubwaaa tunaomlipa kwa kodi zetu tunashkuru yeye asb. ni minyama na supu anashushia na ka-wine!!

Sisi wanyonge hamna shida basi tutakunywa majimoto bila sukari na andazi zachumvi hamna shida baaaba!!

Mkija kampeni baaaba TUNAOMBA mtuhonge kasukari kidoogo sio kanga tena ili tuwaimbie na kuwachezea ngoma ya mnaupiga mwingi eebabaaa...

Nahuu umeme janabi kasema una miyonzi inaua selihai muendelee kuukata tuu ili tuishi saana ninyi nunueni stendibai jenereta baabaaa...
 
Ni vyema Watanzania kwa umoja wetu tuitoe CCM madarakani, maana ni aibu kubwa sana kwa kweli kwa jinsi nnchi inavyoshindwa kwenye nyanja nyingi.

CCM ni wabinafsi na sio binadamu.
 
Tuna uhaba wa Viongozi. Kwenye serious issue mkuu wa mkoa analeta utani wa kijinga. Sukari Ina matumizi mengi Sana.
 
Sasa kwanini serikali inatoa vibali vya ujenzi wa viwanda? Wasitishe uzalishaji wa sukari na wasiagize toka nje ili Tanzania isiwe na wagonjwa.
 
Nilipokuwa sekondari, tulikuwa tunakunywa uji bila sukari. Nilikuwa nakilaani sana kitendo kile.
Baadae nilipoanza kazi na sukari kuwa nyingi madukani, nikachagua kunywa chai ya maziwa bila sukari baada ya ugonjwa wa kisukari kupamba moto.

Kwa ukweli kwa sasa hivi nimeshazoea chai bila sukari na kuepukana na mavinywaji kama coka cola na jamii yake. Hivyo kipindi hiki ambapo sukari bei juu, mfuko wangu hata haujaathirika. Bila magazeti na mitandao wala nisingejua kuwa bei ya sukari imepanda.

Dr Janabi endelea kuelimisha watanzania, inalipa.
 
Watakuja kuibuka na ishu kwamba Mwanga ni hatari Kwa afya ya macho Kwa hiyo tuachane na matumizi ya umeme Kwa sababu Mwanga wa umeme ni hatari Kwa afya ya macho
 
Pale Bashite, kule Chalamila, mbele kidogo Dr Mollel, ukirudi nyuma Nnape, kata Kona ....
Kweli Wa TZ kazi tunayo πŸ‘ΊπŸ€¬πŸ‘ΏπŸ’’πŸ—―οΈπŸ˜‘πŸ˜€πŸ₯Ή
 
Achana na huyo mropokaji aliyesoma sociology. Anakaririshwa madhara ya sukari iliyozidi mwilini lakini hajui kuwa hata kuwa na sukari pungufu nayo ni hatari kwa afya ya binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…