Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Kwani kelele za misikitini na makanisani hazikeri wengine?

Kumbuka walevi ndio wanaendesha nchi, unakerwa na mlipa kodi[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama alivyokuwa anataka jpm awe madarakani mpaka kifo chake tu.
 
Sauti yoyote iwe muziki, mayowe au mtetemo unaozidi mawimbi mrudio (decibel) yasiyoathiri kiwambo cha sikio na mapigo ya moyo au utulivu wa akili kwa kutafakari mambo mengine ya maana yanayohitaji utulivu ni dB 80 na isizidi dB 85.
Kwa sheria ya Tanzania kelele inahesabika kama uchafuzi wa mazingira (environmental pollution). Inatakiwa wale wanaozalisha kelele ili kuwakinga wengine na madhara yake kiafya wanatakiwa kuweka vipoza mawimbi sauti ambavyo vinanunuliwa. Sheria zizingatiwe badala ya kuendekeza siasa kwa nia ya kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wapiga kura wasiwachukie. ZINGATIENI SHERIA zilizopo au mzirejeree kwa marekebisho ili watawala waue wananchi wengi kwa kusababisha afya mgogoro.
 

Attachments

Mpumbavu huyu, anapingana na sheria za nchi, hajitambui kuwa alikula kiapo
 
Ningemshauri ahamishie familia yake pemben ya kitambaa cheupe,boardroom n.k halafu ndio aje aongee hayo anayoongea ndio ataeleweka.
Zaid ya apo ni pumba tu na kutojali wengine.
 
Hii ndio Kauli aliyoitoa leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dr. Chalamila kwa watu wote, kwamba Kunywa bia kimya kimya ni sawa na kunywa Juice.

Aliyeelewa atusaidie kufafanua ili tuanze kuchangia.
Aisee..
 
Ni Chalamila aliyezuia BUKOBA CLUB na Lake Hotel kuendesha shughuli za harusi kwa sababu zinampigia kelele akiwa kwenye kasri lake jirani na kumbi hizo.
Lakini baada ya kuamia Dar ameibuka na maoni tofauti.
Wanasiasa ni vigumu kuwaelewa.
Ndio maana anaweza kukwambia kwamba atakujengea daraja hata mahali ambapo hakuna mto,ukimwambia mbona hakuna mto anakwambia na mto nitauleta!.
Chalamila ni mtu wa porojo tu usimsikilize, kumbuka alivyosema ameongea na Jiwe kuwa yupo anachapa kazi.
Kumbe mtu keshatangulia mbele ya haki,
 
Hii ndio Kauli aliyoitoa leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dr. Chalamila kwa watu wote, kwamba Kunywa bia kimya kimya ni sawa na kunywa Juice.

Aliyeelewa atusaidie kufafanua ili tuanze kuchangia.
Kwenye baa, kila mtu anapenda kuongea kwa sauti kubwa ili asikike. Na mara nyingi kadri idadi ya bia inavyozidi kuongezeka ndiyo sauti inavyozidi kupanda juu kwani karibu kila mnywaji hupenda kuongea na wengine wamsikie, matokeo yake kelele huwa nyingi sana sehemu hizo. Juice haina kilevi hivyo wanywaji sehemu hizo hawapaazi sauti zao kadri muda unavyokwenda. Kwa mantiki hiyo basi mara nyingi huwa pana ukimya maeneo yao.
 
Kelele huwa zinapimwa kwa kutumia kiwango cha usikivu wa sikio la mtu ambacho "units" zake zinaitwa decibles (dB); zero dB ikiwa ndiyo kiwango cha juu kabisa cha sauti ambayo hata kiziwi anaweza ngalau akai-feel kwenye sikio lake. Bado Mh Mkuu wa Mkoa anahitaji ashauriwe katika hilo, tusimwache tu hewani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…