Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Yani amefanya move ya ajabu sana. Huyu kuwa Dar ni aibu. Hapo yeye itakuwa ni kutafuta matamko ya hovyo ili apigiwe makofi na kushangiliwa, baasi. Huwa ni mchekeshaji na si mtendaji.
Haifai kiongozi kuhamasisha upumbavu
 
Sema viongozi wetu bana Sheria wanapitisha wenyewe zikianza kutekelezwa wanakuja mbio mbio kuzuia. Tukichekea huu uhuni wa viongozi kugomea Sheria/ kanuni ipo siku li mtu litakatalia madarakani na hamtakua na chakulifanya.

Hata akina kagame, museveni, Mugabe n.k msifikiri waliruka tu mpaka kubadili katiba/sheria no!
Nchi inaenda kuwa ya hovyo sn
 
we huna mbunge? Ulitaka wananchi wote tuende bungeni kutunga sheria? Sheria ikipita tumeshirikishwa maana yupo mwakilishi wako kule anategemewa kutoa ushauri na mawazo yake kwa niaba yako
Hatujawahi kumuona mbunge wetu jimboni. chochote atakachowasilisha bungen n mawazo yake c ya wananchi. mbunge wako akilala bungen wakat wakuptisha sheria n upumbavu wenu mliomchagua.istoshe kwani hawa wa bunge ni sisi tumewachagua au tumechaguliwa na mwendazake?
 
Kasema leo, Dar ni jiji la biashara, wasiopenda kelele waende Dodoma, watu watafute pesa, wale bia, mziki mnene. Maana wanachangia maendeleo ya jiji.

==========

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo huku akiongezeka kuwa Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukwepa kelele wala kukwepa starehe.

Akiongea wakati wa Swahili Comedy Show iliyofanyika Swahili Exprience, Coco Beach Dar es salaam, amesema “Kikubwa Mimi kama RC naahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi lakini zaidi kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo kwasababu maana na tafsiri ya kelele bado ni jambo ambalo ni gumu kidogo, adhana ikipiga asubuhi asiye Muislamu atasema hizo ni kelele"

"Vyombo vya Kanisani vikipiga kwa nguvu asiye Mkristo atasema ni kelele, miziki ya Baa ikipigwa Mtu ambaye sio mnywa pombe atasema ni kelele, kwahiyo kuna mahali panahitaji busara kuhusu tafsiri sahihi ya kelele ili Muislamu, Mkristo wapate haki zao, mnywa pombe apate haki yake na asiye imani apate haki yake, kikubwa Dar es salaam huwezi kukwepa kilele, huwezi kwepa starehe"

View attachment 2638831
Mangi peleka sanduku 5 za maji ya dhahabu kutoka Mchikichini kwa jirani yangu Mheshimiwa sana Chalamila, jamani nani kama Chalamila, kula bia hadi kuchee, RC kasema ,kauli ya RC ni kauli ya serikali ya DSM, kula bia kula bata maisha yenyewe yako wapi? hujui kesho kama utaamuka au ndio utaimbiwa mapambio ya tutakutana tena paradiso!
 
NEMC ifutwe inakula kodi zetu bure maana haina meno kama kazi yake inaweza zuiwa na mkuu wa mkoa bora ifutwe
 
Jiji linataka mapato....

Jiji linataka amani kwa raia wake....

Hakika mh.Chalamila amenena [emoji106][emoji7]

#SiempreJMT[emoji120]
 
Kasema leo, Dar ni jiji la biashara, wasiopenda kelele waende Dodoma, watu watafute pesa, wale bia, mziki mnene. Maana wanachangia maendeleo ya jiji.

==========

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo huku akiongezeka kuwa Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukwepa kelele wala kukwepa starehe.

Akiongea wakati wa Swahili Comedy Show iliyofanyika Swahili Exprience, Coco Beach Dar es salaam, amesema “Kikubwa Mimi kama RC naahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi lakini zaidi kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo kwasababu maana na tafsiri ya kelele bado ni jambo ambalo ni gumu kidogo, adhana ikipiga asubuhi asiye Muislamu atasema hizo ni kelele"

"Vyombo vya Kanisani vikipiga kwa nguvu asiye Mkristo atasema ni kelele, miziki ya Baa ikipigwa Mtu ambaye sio mnywa pombe atasema ni kelele, kwahiyo kuna mahali panahitaji busara kuhusu tafsiri sahihi ya kelele ili Muislamu, Mkristo wapate haki zao, mnywa pombe apate haki yake na asiye imani apate haki yake, kikubwa Dar es salaam huwezi kukwepa kilele, huwezi kwepa starehe"

View attachment 2638831
Niliwaonya Nemiki...
 
Ndio maana Mimi nikiona watu wanalilia katiba mpya nawaona kama machizi tu. Tatizo la hii nchi sio katiba ila ni usimamizi wa hiyo katiba. wanao taka katiba mpya wangehakikisha kwanza katiba na sheria zilizopo zinafuatwa kiuhakika.

Ni mara chache sana kusikia viongozi wetu iwe wa chama tawala au upinzani wakisimama na kukemea usinginaji wa katiba/ sheria
Exquisite [emoji7]
 
Kama kasema hivyo kakosea sana kwa sababu inakuwaje starehe yake na walevi wenzake iwe kero kwa watu wengine wanaoishi maeneo jirani bila kujali kama kuna wagonjwa,watoto,wazee na hata wakati mwingine hutokea dharura ya misiba lakini wote hao wateseke eti tu kwa vile kuna washenzi wachache wanakunywa pombe!
Halafu kama yeye anapenda sana kulewa ndio anatakiwa arudi kwao huko akanywe ulanzi atakavyo sio kuwaambia wenye mji wao eti wahame,halafu nilikuwa namsapoti sana Rais lakini tayari ameanza kunitoka kabisa naona kile kilevi kiitwacho madaraka kimemzidi kwa sababu hata kilichomshawishi kumleta Dar sijui ni kipi au sijui kuja kuhamasisha ulevi na mikelele!
Mbona makanisa wanakesha Wanapiga vyombo vya muziki hamsemi ?
 
Back
Top Bottom