The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema maelekezo yote yaliyotolewa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya hotuba yake baada ya kuapishwa yametekelezwa na yanaendelea kutekelezwa kwa kufanyia kazi makundi yote ya msingi kwa kusikiliza hisia zao, matatizo yao ili kuweza kuyafanyia kazi na kuunda Taifa lenye umoja.
Chalamila ameeleza hayo Disemba 2, 2025, alipokuwa akiwasilisha salamu za mkoa wake mbele ya Rais na Wazee wa Dar es salaam, waliokutana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
"Mheshimiwa Rais, sisi wa Dar es Salaam, tumekusikiliza siku ukiwa unaapishwa, tumesikiliza hotuba yako ya kwanza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maelekezo yako yote tumeyatekeleza na tunaendelea kuyatekeleza kwa kuhakikisha tunafanyia kazi, kwa kusikiliza makundi yote ya msingi, kwa kusikiliza hisia zao, kwa kusikiliza matatizo yao ili tuweze kuyafanyia kazi na tuweze kuunda taifa lenye umoja" amesema Chalamila.