Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Ni Chalamila tena katika matamko yake kama vile amekatwa kichwa! Mchengerwa OR TAMISEMI tunasubiri neno lako hapo, huyu bwana hajui kama kuna sheria za kufuata?
====
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali watu wote wanaojihusisha na uporaji 'vibaka' katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo hususani vibaka wa Daraja la Selenda, ili iwe fundisho kwa wale wote wanaohatarisha amani na usalama jijini.
Chalamila amesema hayo mwishoni mwa juma alipoongoza zoezi la usafi kama maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Daraja la Selenda, Soko la Kimataifa la Salamaki la Feri na maeneo mengine ikiwa ni maandalizi kuelekea Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika 'Mission 300' unaotarajiwa kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia Januari 27-28 mwaka huu.
Chalamila amesema, "Sasa, naagiza kibaka takayekamatwa, asipigwe wala kuuliwa, apelekwe maabara awe 'skeleton' mifupa ya kufundishia wengine ambao wataiga mfano kwamba wizi haustahili katika jiji la Dar, kwahiyo hilo ndio agizo langu, wakale kielelezo kizuri kwa watu wengine." amesisitiza RC huyo.