Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka vijana wasiharibu maisha yao kwa siasa na propaganda za chuki, badala yake wajikite katika jitihada na Elimu kwa kuwa ndio siri pekee ya mafanikio katika maisha yao.
Amesisitiza maisha si mepesi kama wengi wanavyodhani, ni magumu na hayako kwenye propaganda ya vinywa na maneno mengi, bali lazima upitie magumu ili ufanikiwe.
Chalamila ameeleza hayo leo, Jumamosi Mei 16, 2026 alipozungumza katika Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu lililobeba ujumbe wa Never Again.
"Kwa hiyo msije hata kidogo mkadhani maisha ni mepesi na kuweza kuyaharibu kwa siasa ndogo ndogo na zisizona mashiko. Go deep kwenye masomo yako. Kama baadaye unataka kuja kufanya biashara, utachagua utakapokuwa, mkono huu una jambo na mkono huu una jambo. You still have time.
Kama mimi Bwana Chalamila, sina historia yoyote ya kaka yangu, baba yangu wala mama yangu kuwahi kuwa kiongozi katika serikali, sina"