Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo


Hivyo ndivyo inavyotakiwa.
 
Ww na yy wote wapuuzi, inamana vifaa vipo? Au hyo bima ingeteremsha vifaa kutoka peponi?
 
Ulitaka aseme Kwa namna ipi kwa mtu ambaye hataki kuchangia pesa kwa Mtoto wake aliyetumboni ili azaliwe?
Au mwanamke ambaye hataki kuchangia mtoto wake azaliwe anataka azaliwe burebure
Namna nyingine inayofaa
kauli za "kama huwezi....fanya..." eg. mtu akwambie kama hutaki kupokea maoni anzisha JF yako, kama huna elfu10 ya hela ya twisheni kafungue shule yako umfundishe mwenyewe
elfu50 sawa ichangiwe tatizo RC kawasilisha hoja kwa maneno yasiyofaa
 
Kwamba huduma bure ni wehu, hapana tunakuwa na ujinga fulani, ni kwamba haiwezekani ama shida nini

Heka moja elfu 30 mpaka 40, sawa tufanye 40, heka moja mtu mmoja anailima kwa siku ngapi, jiulize kwa siku kaingiza sh ngapi? Jiulize hiyo pesa inamtosha kwa chakula, mavazi na vitu vingine, serikali haijitambui, viongozi wabinafsi, kuna mataifa yanaweza sisi kwanini tushimdwe, kwa tanzania hii inawezekana, kifupi tu viongozi wetu ndio wabaya wetu, nimetembea nimeona kuna watanzania hawajimudu hata kwa hiyo 40 ya pamoja.
 
Kwamba huduma bure ni wehu, hapana tunakuwa na ujinga fulani, ni kwamba haiwezekani ama shida nini
Sisi wapenda Haki. Bure ni dhambi. Kitu chochote lazima ugharamike. Hiyo ni Moja.
Ndio maana Mungu Mkuu tunayemuabudu licha ya kuwa sio mhitaji lakini anatutaka tukienda kwake tusiende Mikono mitupu.
Kwa Sisi Watibeli, huo ni Wehu


Ubaya wa viongozi wetu unatokana na kushindwa kuwajenga watu wawe na minute ya kujitegemea(falsafa ya Nyerere)

Ingawaje Sera ya Elimu inataka watu wakimaliza shule waweze kuwa na uwezo wa kujitegemea. Ukishakuwa na uwezo wa kujitegemea huwezipendelea mambo ya burebure
 
Jamii yenyewe imefundishwa na serikali kuombaomba
Hakuna wa kulaumiwa hapa ila serikali
Wanapokea mpaka misaada ya vyoo na hata hivyo havidumu au havipo tu
Kila leo nchi masikini zinaomba misaada na wengi wanasema ooh watoto wanakufa mara magonjwa mengi yaani ni kulia lia tu
Ila mkipewa na kuhurumiwa hela zinapigwa na wachache
Tuache utani yaani leo hospital inakosa gloves?
Hiyo misaada inafanya nini?
Kuropoka kwake ni kawaida maana tunawajua wengi wa hivyo ila tunawapiga stop lakini huyu wa kumpiga stop ndio anaemdekeza
 
Acheni kutoa majibu ya jumla. Kuna kipindi cha Radio Free Africa kinaitwa "Je Wajua" hurushwa kila J'pili saa nne. Jaribuni kusikiliza halafu mje hapa kutoa maoni yenu.
 

😂😂😂

Hiyo ndio Lugha inayogusa Mtima nyongo na kumfanya mtu aelewe kwa urahisi.
Huoni hapa tunajadili
Angesema unavyoshauri wewe Wala isingekuwa habari Wala tusingekuwa haa tunajadili
 

Umeongea Jambo kubwa na muhimu

Kila mtu ombaomba
 
Acheni kutoa majibu ya jumla. Kuna kipindi cha Radio Free Africa kinaitwa "Je Wajua" hurushwa kila J'pili saa nne. Jaribuni kusikiliza halafu mje hapa kutoa maoni yenu.
Acha kuadvertise radio na vipindi vya watu. Toa hoja yako ueleweke.
 
Acheni kutoa majibu ya jumla. Kuna kipindi cha Radio Free Africa kinaitwa "Je Wajua" hurushwa kila J'pili saa nne. Jaribuni kusikiliza halafu mje hapa kutoa maoni yenu.

Mkuu wewe si umesikiliza. Jenga hoja zako
 
Kwa akili hizi tutapelekeshwa sana na watawala.

Ukipenda bure lazima upelekeshwe na wanasiasa

Wanasiasa hawapelekeshi watu wanaogharamia mambo Yao.

Niliwahi kusema hii nchi tukilipa Kodi Watanzania angalau asilimia 50 wananchi watakuwa na nguvu zaidi ya viongozi
 
Anaweza akawa sahihi lakini lugha aliyoitumia kama kiongozi sio sahihi......

Lakini pia watu tumetofautiana vipato kwa wengine buku ni hela ya sigara na kwa wengine buku ni hela ya mboga......

Kiongozi ni wa watu wote.... masikini na matajiri.....kauli zake ziwe kwenye kujenga na sio kuzua taharuki
 
Watu wanataka bure tu kila kitu!
Yani hata wakipeana mimba kwa starehe zao wanataka serikali iwahudumie bure!
Tatizo sisi tunaoishi uswahilini hakuna mtu anatuelimisha kuhusu bima hiyo. Ni kweli bima hiyo IPO na inafanyakazi hosp zote za serikali nchi nchi mzima kasoro national referral hosp kama muhimbili.

Mimi nimeona faida ya hiyo bima hawana tatizo nayo popote penye government hosp au kituo cha afya.

Tunaomba kuwepo na juhudi za makisudi za serikali kutoa elimu umuhimu wa bima hii.

Temeke wakiwaweka watu wao ambao w alikuwa wanafuatilia na kukatia watu lakini sikuizi sijui nini kimetokea hawaonekani pale mpaka uende ofisi za manispaa
 
Haupo sawa kichwani hata kidogo. Na kama ndiyo watanzania baadhi mpo hivi basi ni laana kwa nchi. Hivi kweli wewe kwa akili Yako unaona ni sawa mtu anayehitaji huduma ya kiafya kuambiwa hatuna gloves? Hospital tena ya umma ambayo mwananchi anakatwa Kodi na kabebeshwa mzigo wa tozo. Tukisema chalamanda yupo sawa tunatoa taswira Gani katika sekta ya afya? Juzi kuna mama kafa kwa kung'atwa na nyoka wamekataa kumtibu Hadi atoe 150.000. wewe unaona ni sawa tu. Bila shaka wewe utakuwa ni baba yake shetani. Utakufa vibaya wewe.😭
 

Unaweza kuwa Sawa kabisa
Moja ya faida ya kauli za namna hiyo ni kufanya Jambo Fulani kuwa habari na kujadiliwa Jambo ambalo linaongeza uelewa, watu kujua nini chakufanya

Angeongea kawaida wala isingekuwa habari na tusingekuwa hapa.
 
Says a privileged keyboard warrior.
Ukipenda kuandikandika kwenye majukwaa, lazima ujue unahitajika kuwa mtafiti.

Ungelikuwa unajua umasikini uliopo kwa Watanzania wenzako, usingeizungumzia elfu arobaini kama jero.

Wewe na aliyeongea nyote mko sawa kwa sababu hamjui kina cha ufahamu wenu ni kifupi sana.
 
Hiyo ndio Lugha inayogusa Mtima nyongo na kumfanya mtu aelewe kwa urahisi.
Huoni hapa tunajadili
Angesema unavyoshauri wewe Wala isingekuwa habari Wala tusingekuwa haa tunajadili
hata hivo mentality ya BURE imeharibu wengi badala ya kutumia neno GHARAMA NAFUU wanatumia BURE sasa wakiambia watu changia inakuwa kelele, si unaona POTUS kajitoa kusaidia Africa imekua kilio kwasababu tumezoea bure/msaada badala ya kuchangia japo kidogo imagine leo waseme net za malaria ziuzwe elfu5 utasikia vilio wakati malaria anatuadhiri sisi wenyewe, kuchangia tunaona ni kuteswa. Why tumezoeshwa BURE!
 
Mkuu sawa ni haki yenu kulalamika kwa kile alichokiongea RC ila usiniambie ya kuwa ndani ya miezi tisa umeshindwa kudunduliza hadi ifike 50,000 hata kama ni umasikini ila hii imezidi.
Mimba inakuja na vikwazo vingi kuweka pesa kidogo kidogo ni muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…