Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Kuna watu wanafanya kazi DSM mshahara wa siku ni elfu sita. Hata akijibana vipi lazima matumizi yawe makubwa kuliko kipato. Pia, kuna kundi la watu wasio na ajira. Wanaishi kwa kudura tu, wakipata wanakula wakikosa wanalala.
Mkuu hiyo 6000.kwa siku ukijibana vizuri kuna akiba inabaki labda uendekeza milo mitatu na soda. Na hao ambao hawana ajira wameshindwa kupata hata mtaji wa kufanya biashara au ndo hela za boom walikuwa wanazila zote? Mkuu sasa huku ni kuendekeza ngono. Sawa tuseme ndo starehe yao wameshindwa kutumia hata kondomu.ambazo ni bure?
 
Ndiyo maana nimekuambia inaonyesha wewe umekulia kwenye rough environment. Hakuna ustaarabu bali mmezoea kupayukiana!

Mimi nimezoea kumjibu mtu vile atakavyokuja.

Kum-treat mtu vile anavyojilengesha kwangu.

Sasa mtu akikuuliza swali la kijinga unataka utumie Busara kumjibu?
 
Kuwa na bima haikufanyi hizo gloves ziwepo hospital kwenye hospital za serikali 90% dawa ni kununua hata uwe na bima kiasi Gani Kuna muda unaenda unaambiwa hata kipimo Cha maralia hakipo vimeisha😭😭

Nadhani Huwa huendi government wewe
 
Maskini wa tanzania wanajifariji kwa kuzaa watoto wengi ambao hawana uwezo wa kuwahudumia
 
Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.
Kuna huduma ukienda na hako kabima kako hupati ng'o ni kabima kasicho na thamani hospitalini ni kabima ka kupata get pass ya kumuona daktari na kuandikiwa dawa za bei rahisi mno na kukiwa na vipimo vikubwa utaambiwa ulipie tu maana bima yako hairuhusu wewe kupata hio huduma dawa za bei juu huwezi kupata kwa hio bima mfano dawa za kuanzia 100,000/= na kuendelea hupati kwa hio bima lazima uambiwe ulipie tu
 
Kama ilivyo kwa kondomu kuwa bure, ndivyo na gloves ziwe bure.
Watu hawajaomba chakula, wameomba gloves za bure!
___
Kuhusu ujira wa 6,000 kwa siku, hebu jaribu kufanya uchanganuzi.
Nauli, chakula, familia, kodi, mavazi, dharura na kila kitu halafu niambie kwa siku una-save ngapi.
 
Ndio maana kuna Bima Mkuu.
Kata Bima ili kujihami na hizo circumstances
Bob, kuna kaya hawawezi kupata Tsh. 30,000 ya pamoja ili kupata hizo bima za CHF.
Ili kupata hicho kiasi kwa pamoja, itawabidi wasile ama wasinunue hata mafuta ya taa kwa mwezi mzima.

Nenda Singida, Dodoma na mikoa mingine mikame ambako chakula walichovuna huisha mwezi Septemba kisha miezi mingi wanaishi kwa kubaingaza ndipo utajua 30,000 ni fedha nyingi sana kwa baadhi ya Watanzania.
 

Ndio maana nikaorodhesha utanufaika na nini kwenye hiyo Bima.

Ultrasound bila Bima serikali ni Tsh 15,000 - 25,000 kutegemeana na hospital.
Lakini ukiwa na Bima ya Tsh 40k hutoi Pesa.

Kujifungua kwa OP serikali ni Tsh 150,000 - 300,000 serikalini ukiwa huna bima.
Ila ukiwa na Bima ya 40k hutoi Pesa yoyote.

Kulala usiku Mmoja kwenye vitanda vya hospital za serikali ukiwa huna bima, Tsh 10,000 to 20,000. Lakini ukiwa na Bima ya 40k hutoi hata Buku.

Hiyo Bima ya 40k ni ya watu wa kipato cha chini Sana ili nao Wapate matibabu.

Imesaidia wengi.

Hiyo Bima ya 40k
Unapima Magonjwa yafuatayo;
UTI
Malaria
Taifodi
Na Magonjwa yote ya bacteria.

Kama haitoshi, unaweza kucheki full blood picture

Sasa wewe unataka nini zaidi?

Magonjwa makubwa hata hizo Bima za Milioni Moja hayatibu.
 

Nakuhakikishia hizohizo Kaya zinapeleka zaidi ya Laki kwa waganga wa kienyeji. Ushahidi huo ninao.

Mtu hospitalini anasema gharama. Ni kweli kwa sababu si Hana Bima.
Lakini mtu huyohuyo anaenda kwa sangoma anaambiwa atoe Laki tatu na anatoa.
 
Nakuhakikishia hizohizo Kaya zinapeleka zaidi ya Laki kwa waganga wa kienyeji. Ushahidi huo ninao.

Mtu hospitalini anasema gharama. Ni kweli kwa sababu si Hana Bima.
Lakini mtu huyohuyo anaenda kwa sangoma anaambiwa atoe Laki tatu na anatoa.
Hizo familia zipo, na zipo ambazo haziendi kwa waganga na hazina kitu.
 
Mkuu kwenye hiyo 6000 ningetumia 2000 kwaajili ya chakula kila siku. Hapo kwa siku nasave 4000. Mwezi unasiku 30 hivyo basi 4000×30=120,000. Mkuu hiyo 120,000 inatosha kwakodi(let's say kwa mwezi unalipa 60,000) hapo inabaki 60,000 ambayo inatosha kwa mavazi na nauli kama ukiitumia kwa makini na akiba inabaki.
 
Nimefurahi kusoma maoni yako, mdogo wangu.
Nikutakie usiku mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…