VITU VINAVYOATHIRI MALEZI NA TABIA MBOVU ZA WATOTO KULIKO UMRI WAO.
❌ Tamaduni na ngoma za hovyo zisizo na maadili kama vigodoro na singili.
❌ Nyimbo za Taarabu zinachangia asilimia kubwa kujaribu maadili ya watoto wa pwani , na ukimuona mwanao wa kiume anapenda kuimba au kwenda kwenye matamasha ya nyimbo hizo, Anza kumtilia mashaka
❌ Nyumba yenye vyumba vichache ambapo watoto husikia faragha za wazazi .
❌ Baadhi ya wazazi / wakubwa hasa wa kike kupenda kuweka vikao vya majungu, kuongea mbo mazito ya mahusiano, michepuko Yao na mbinu za kumbana/ kumchuna mwanaume bila kujali kuwa watoto wapo na wanakariri neno kwa neno.
❌ Tamthilia zinazoonyeshwa kwenye Tv masaa 24 wanawake wenye nyumba/ wadada wa kazi na wanawake in general wanaziangalia masaa 24, tena wapo na watoto wanaofurahia na kuchangiwa kinachoendelea. Tamthilia hizo Zina theme nyingi za mapenzi na mahusiano.
❌ Mahubiri kwenye nyumba za ibada wale ambao hawatengi ibada za watoto Bali wote huchanganyikana. Sasa, asilimia kubwa ya mahubiri Yao ni mapenzi na mahusiano. Wanaongea mambo mazito ama wanapo kemea tabia Fulani au wanapomasisha mahusiano, wakati wanaongea hayo watoto wadogo wapo.
❌ Wakitoka hapo wanaokwenda kufanyia utafiti waliyoyasikia na hapo wanakwenda kuwa influence wenzao ambao hawajui chochote na hivyo kujaribu maadili ya jamii nzima