Challenge ya 2011; matches na results

Full time wao 2 sisi 2. Penalti zinaanza
 
Polisi please tupunguzie presha za mnyukano wa penati...tupe final results.
 
penati zimekwisha sisi 4 wao 5. Yahee twatoka
 
Timu moja ya Tanzania imetolewa sasa matumaini pekee ni Kwa Tanganyika
 
Tumeshindwa penalties 5 Uganda-4 Z'bar!!!
Wazanzibar hawakujiamini! hilo ndo oni langu...
 
duh, wamejitahidi . Ngoja tusubiri hao ndugu zao watafanya nini...
 
kwa hiyo inayofuata ni wabara?

nani kakosa hiyo penalt?
 
Sasa wanaogopa nini wakati wanja zima limejaa ili kuwapa support wao???
 
Sasa wanaogopa nini wakati wanja zima limejaa ili kuwapa support wao???
haukuona afta wamefunga goli la kusuluhisha waliloose confidence kabisa..kubutua butua..
so ata walivyoingia penalty waliingia na wasiwasi..i term it, kujiona wameshashindwa. Ila no mtazamo wangu. We umeonaje game yao!??
 
Kaseja,Sajigwa,Yondani,Nyoso,Banka,Ngasa,mwasika tupeni raha wabongo
 
Nurdin bakari dakika ya 22 kakosa goli baada ya kupata mpira kutoka kwa Banka...
 
Uuuuuuuuwi, ndo naamka nasikia ndugu zetu Zanzibar wametoka. Mmmmh, inauma lakini angalau wamejitahidi kusawazisha magoli ndani ya 90+. Lets hope Kilimanjaro itatufuta machozi. Mungu ibariki Kilimanjaro Stars.
 
Half time ngoma 0 - 0

Asante sana kwa kutuhabarisha. Naomba nikuulize maswali mawili, katika kipindi cha kwanza Kili Stars walionyesha uhai au matumaini kuwa wanaweza shinda au walikuwa wanashambuliwa na wanyarwanda mara ka mara? Ilo la kwanza, la pili mashabiki wamejaa au muda huu wamepungua kutokana na kuwekwa kiingilio?
 
Tumeonyesha uhai lakini hakuna mmaliziaji na mara nyingi huwa tuna mtegemea Ngasa kuanzisha mashambulizi lakini naona leo kabanwa ila naona Boko kaingia badala ya Henry Joseph Shindika......unatakakulinganisha bure na pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…