Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.
Mwalimu wangu wa uraia amewahi kuniambia maneno haya: "Bangi ukivuta leo itakusumbua na kukuendesha miaka 20 Ijayo".. Amini usiamini,.. Hapa TZ kuna ofisi zinaendeshwa kwa nguvu ya bangi za miaka 20 iliyopita.

Mh! Kama sikuelewi na kama najaribu kukuelewa embu funguka kidogo
 
Tunajuwa amekutuma kupima upepo juu ya mipango yake na MAGAMBA. Na hii inajulikana kwamba ni Plan B ya serikali ya MAGAMBA baada ya kuona kwamba mipango yake ya kuiua CHADEMA imeshindikana. Lakini kamwambie kwamba "KINA CHA BAHARI HAKIPIMWI NA VIDOLE".

CHADEMA sio ya Msajili wa Vyama vya Viasa, CHADEMA ni chama cha waTanzania walio choka kuwa watumwa katika nchi yao.
 
Huyu huwa ananipa kinyaa hata kumsikiliza. Kwa sababu imejifungamanisha sana na CCM kiasi kwamba hana sifa hata moja ya kuwa msimamizi wa vyama vya kisiasa. Mwulize aaondoka lini? Tumemchoka kupita kiasi, aondoke aende ili watu wenye mapenzi mema waiongoze hiyo ofisi aliyoiharibu.
 
Naamini na ndivyo itakavyokuwa hii kesi ya lwakatare itapigwa damadana mpaka 2015 ili hukumu yao dhalimu kutolewa wakiamini itaweza kuondoa credibility ya CHADEMA kwa raia japo naamani njia zote zinazotumika na ccm pamoja na polisi wake zimekuwa zikiipaisha CHADEMA kisiasa na watashangaa na kutoamini pale watakapokabidhi nchi mikononi mwa upinzani na uhuru rasmi wa Tz kutangazwa
 

Which wa CCM is not necessarily mwanzo wa CHADEMA...
 
Pasco,

Hivi Nikimuita Tendwa KIBARAKA wa MACCM nitakuwa nimekosea au Kumtusi kweli?

Kifupi: Weka Mbali na TEMBO.
 

Kwa ujumla kuna wenzetu humu wanaandika maneno yasiyo ya kistaarabu. Fisadi/dhaifu sio matusi ni maneno yanayotafsiri hali katika kipindi fulani.
 
Nafikiri tunapokuwa na watu wa kukumbukwa kutokana na uzalendo wao baada ya vifo vyao, tuwe pia na orodha wa watu ambao walikuwa ni balaa katika Taifa hili. Watu hao waandaliwe mahali maalum pa kuwazika ili iwe rahisi kwa watu wa vizazi vijavyo kuijua historia ambayo nchi yetu imepitia hasa katika uongozi.

Kwenye orodha hiyo TENDWA AWE WA KWANZA. HAYA HATA AKIFA AKUMBUKWE KWA MABAYA YAKE YA KUDIDIMIZA DEMOKRASIA, KUKOSA UONGOZI WA KIMAADILI NA KUSHIKILIA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA YEYE AKIWA MKEREKETWA NA SHABIKI MKUBWA WA CHAMA KIOMOJAWAPO, CCM.
 
Ni wazi kama Tendwa kayanena haya haelewi matekeo na madhara ya alichosema kuhusu kuifuta CHADEMA
 
Tendwa ni mpuuzi, kama haujiheshimu nani mwingine akuheshimu, ata tusipo kutukana kwenye mitandao tutakutukana kwenye roho zetu, kitu usichoweza kuficha wewe ni kibaraka wa CCM. ambayo inatutesa na kudhalilisha mama zetu... kwa ufisaid uliopitiliza. na Chadema si mali ya tendwa ni mali ya wanachi wenye nia njema ya taifa hili. hivyo kama unataka kuelewa kifute kisha usikilizie....
 

Wewe kweli kiboko....umeona useme hauhusiki kimtindo....ngoma inogile kwa Pasco....teh teh teh
 
pasco asante kwa kutiririka ila siyo raisi kiasi hicho kuifuta cha mungu na kama wanataka nchi ichafuke wathubutu.

"PASCO NAONA KINANA LARGER ILISHAMKOLEA TENDWA NDIO MAANA AKAWA ANA ROPOKA TU"
 
blah blah blah blah......pole kaka Pasco kwa zile "aibu" za "Bukoba boy".
 

Mwigulu cjui ndio jina lake. Yuko china ktk kutengeneza ushaidi wa video ili ionekane ilopo sasa polisi ni fake ila atakayotoa yy ndio original kwa madai ya kupewa na kiongozi mkuu wa CHADEMA. Mtackia ndicho kilichompeleka China. Wachina wameikamata CCMafisadi na CCMafisadi ndio wanaongoza nchi kwass ivyo CHADEMA inatakiwa wawe makini sana. Lkn kukifuta CHADEMA napo nj shughulu pevu kwani CHADEMA co Lwakatare, Mbowe, Slaa, Zitto, Arfi. CHADEMA ni watanganyika wote,, ivyo hapo pagumu tataaaaa
 
Tendwa na wenzake wa CCM wangetamani sana CHADEMA ifutike kwenye anga za kisiasa nchini, lakini hii siyo NCCR -Mageuzi walioiangamizwa baada tu ya kuwa tishio kwenye uchaguzi wa 1995.

CHADEMA ni taasisi iliyosheheni watu wa idara mbali mbali. Pasco usimsikilize Tendwa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi yule, hatakusaidia kupata yale unayoyadadisi kwa usahihi.
 
"Nikadadisi zaidi, iwapo hayo kwa CHADEMA, yatathibitika kuwa kufanywa na CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Msajili kwanza alisita kidogo na kusema kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa hayo, hakiwezi kufutwa right away kwa sababu huko kutakuwa ni kuvunja serikali iliyopo madarakani, bali atakipeleka Mahakama Kuu ili mahakama itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!. Hii inamaanisha as of now, hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!".

Hapo umeibua swala muhimu sana mkuu wangu kudos!!


"Kwa kumalizia, nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua jf, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na watu ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa viongozi wa taifa hili!".

Mods wanafanya kazi nzuri tuwape ushirikiano wa kutosha kupunguza haya mambo.Tunaweza kukosoana bila matusi na kweli hii ni changamoto hapa JF ambayo bila sisi tunaopenda jukwaa hili kujitahidi kubonyeza Report Abuse kazi si ndogo na namuomba pia mzee wangu Tendwa awe anabonyeza hicho kitufe pia kuwasaidia mods.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…