Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.

Mkuu hili sinema bado linaendelea la Bona fide? Kukifuta zitakuwa hila za watawala kufanya mbinu mbinu
 
Kwavile mkanda ni bonafide genuine na kwavile chadema wamekataa kujitenga na mambo binafsi ya Lwakatare, basi Tendwa asilaumiwe huko mbeleni...

Nashindwa kuelewa hapa busara ya msajili wa vyama iko wapi? Kwani hayo mashitaka ni juu ya Lwakatare binafsi, au Lwakatare kama kiongozi wa CHADEMA? na kama ni ya Lwakatare binafsi kama Kova alivyotuaminisha, sababu za kuifuta CHADEMA kwa makosa ya mtu binafsi inatoka wapi?

Ninachojua hata kama Lwakatare anatetewa na mawakili wa ambao ni wanachama na viongozi wa Chadema bado hakufanyi matokeo ya kesi hii kuiathiri Chadema kwa namna yoyote isipokuwa kisiasa.
 
Mimi nafiki Tendwa kama walivyo wazee wengine wahafidhina kwa CCM kina Warioba ..amechanganyikiwa kuona CHADEMA inapata kukubalika kiasi hiki!!

Anawaza kuifuta kwa kuthibitika mahakamani kuwa kina husika na vurugu zinazotokea nchini!!! kuna kesi imefunguliwa kuituhumu CHADEMA na hili?
Haiingii hata akili kujadili hili vurugu zote!!

Akafie mbele atuachie Tanzania yetu...hawa ndio wanaleta uvunjifu wa amani kwa ujinga wa ktokufikri kwao!
 
Pasco heshima mbele kaka!

Hivi motive ya swali lako ilikuwa ni nini?? Maana anayeshtakiwa mahakamani ni Lwakatare sio mkurugenzi wa ulinzi wa CHADEMA.
Lwakatare kama mwanachama ana full support ya chama chake lakini hata akihukumiwa kutenda makosa atakayekwenda jela ni Lwakatare sio Mbowe wala Zitto.

Sasa hiyo connection kisheria wewe na huyo Jaji mnaitoa wapi???

Mnachoweza kusema ni kwamba politically CHADEMA wataathirika endapo kiongozi wao atakutwa na hatia.

Sioni kisheria mtawahukumu vipi CHADEMA iwapo anayeshitakiwa si CHADEMA.
Lwakatare anatuhuma ya jinai,, je huyo Jaji amekwambia makosa yapi yanamruhusu kufuta chama cha siasa?
Hebu pitia upya Political Parties Act sec 19 na 20, inawezekana background yako ya sheria utatusaidia kuelewa.
 

Kwani aliyeshitakiwa kwenye kesi hii ni nani? Mshitakiwa wa kwanza,pili .... nk ni kina nani? Na uamuzi ukitolewa na mahakama anayepaswa kuwa guilty or not guilty ni Lwakatare au CHADEMA. Please lawyer up properly and exclude the bush whlie doing that. Thank you
 
Kwa maongezi ya Tendwa nilitarajia mpaka sasa ameshaifikisha CCM mahakama Kuu! CCM walikuwa wanatumia propaganda chafu ya udini, Yeye Mwenyewe alishiriki kumtishia Mhe Lema Kifo kule Arumeru...
TISS wasiwadanganye kwa zile options walizowapa! Kuifuta Chama ambacho kimeshawaingia wananchi mpaka kwenye mifupa si kazi rahisi sana. Pengine kama angekuwa na busara angeweza kuvisualize madhara yatakayotokana na kitedo hicho anachokitamani kukifanya...For real really nchi haitotawalika!!!! Hiki kibabu kinapashwa kitambue kuwa hata Nchi ambazo wao wanazitegemea kwa misaada tayari zinatambua uwepo wa CHADEMA!...sorry to say hivi vizee vinatuharibia nchi kwakuwa muda wao wa kuishi ni mdogo...
 

hata hiyo kalamu nyekundu ya tendwa ikitumika haitaifanya ccm kuwa nzuri,TUNAIPENDA CHADEMA
 
Ahasante Mkuu Pasco kwa uchokonozi wako, nadhani woote wamekusikia na kukuelewa, ni vizuri JF ikawa na ethics tukawa na heshima, kabla ya kurusha chochote think of the recipient!! Ubarikiwe!

 
Last edited by a moderator:
-Kukifuta chama cha siasa hakuna mahali popote sheria imeweka Exception.Hayo ya busara za kufuta chama cha upinzani na chama tawala ni mawazo binafsi

-Ilisemekana msajili wa vyama vya siasa ni mbumbu wa sheria,nimeamini

-Anajua sheria ya vyama vya siasa ina mapungufu lakini amejikalia ofisini tu
 
Umeguswa hutaki kukubaliana na ukweli, lakini kaa usubiri huyo Mungu usiye mkubali kuwa kiongozi wa chama, atakupa majibu yake!!!!

 
Polisi wanabandikia watu kesi na CCM inabandikia vyama kesi. CHADEMA ina wawakilishi bungeni na ndio chama kikuu cha upinzani, hebu ifute kama hapajachimbika. Pasco mbona huu uzi wako ni mzaha?
 
Sheria ya vyama vya siasa inasema hivi juu ya Power of Registration to cancel registration..


Ukirudi nyuma kwenye usajili sheria namba 8 inasema

Hapo kwenye red inasema if by its constitution or policy.....jamani huyu jamaa alikuwa Jaji wa mahakama gani???

Hata anaposema CCM wakikosea inabidi awapeleke mahakama Kuu, kwa provision ipi maana hakuna mwongozo wowote kwe sheria hii unless mimi nakala nilonayo haina baadhi ya vipengele.

Kinachosikitisha ni kwa Pasco kutokumwuliza maswali magumu.
 
Last edited by a moderator:

Pasco, hapo kwenye wino mweusi.
Aliyo kueleza Tendwa si mambo ya kukiufanya ubabaike, Tendwa anavitenda vibaya vyama vya upinzani, na kwa vile Mtenda hutendwa, wakati utamuhukumu Tendwa. Hana lolote la kushauri humu JF!. Lakini pia, Pasco, kuifanya JF kuwa kila kitu kwako zaidi ya familia na mke wako hiyo si sawa, acha acha kufunga ndoa ya kudumu kwa mambo km haya, JF si mamako!
 
Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifanyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.

Mkuu kama hayo yalikuwa ni mazungumzo tu baina yenu ninyi wawili:

Iweje uyalete hapa jamvini kwa ajili ya sisi wanabodi kuyajadili?
 
Itathibitika pasipo shaka, proven beyond reasonable doubt, kuwa viongozi wakuu.......................
Pasco naomba upaangalie vizuri hapo kwenye red kama pana typing error yeyote tafadhali kabla sijachangia
 
Last edited by a moderator:
Pasco
Kama kuna sheria yoyote inaweka mazingira ya Chama cha Siasa kuvunjwa kwa sababu zozote zile hiyo ni sheria inayokwenda kinyume na katiba, haina tofauti na hukumu ya Kifo kwa Binaadamu.

Ni pia zielewi uhalali wa kuvunja chama cha siasa kwa makosa ya viongozi wake unatokea wapi, ikumbukwe vyama vya siasa sio mali za viongozi.

Fikra kama hizi, hasa kipindi hiki ndio zinawapa wananchi wengi zaidi hamasa ya kujiunga na CHADEMA.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…