Chama cha Madaktari acheni wizi kwenye kutoa leseni za Madaktari wapya

Chama cha Madaktari acheni wizi kwenye kutoa leseni za Madaktari wapya

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
8,406
Reaction score
9,619
Sina Shaka nyie ni Madaktari pia mliopitia mafunzo haya magumu yatakayo moyo na maamuzi magumu kuchukua fani hii.

Naomba mjitokeze na mtoe ufafanuzi kuhusu mitiani ya Madaktari wetu wanaomaliza intern kuamua kuwafanyisha mtihani tena na kwa malipo ya Tsh 150,000/= yana faida gani kwa mhusika au yanamjenga kwa lipi kama siyo ufisadi na wizi wa mchana kweupe?

Niseme nimewahi pitia huko that's naandika kwa uchungu maana mzigo naujua vizuri.

Mnajua nyie haikuwai kuwatokea, na hata muda huu mkipewa huo mtihani huwezi fanya lolote hata kama wewe Profesa maana medicine ni pana utafanikiwa ambulia kile wakifanyia kazi kila siku na kwa bahati mbaya hakuna duniani Profesa wa mwili mzima wa binadamu.

Sasa mmekuja na wizi kwamba Daktari (MD) amalizapo intern afanye mtihani kwa kulipia Tsh 150,000/= tena atafanya mara ya kwanza au ya pili au tatu Kama hakuweza faulu.

Iko hivi, Daktari husoma miaka mitano na ndani ya muda wote hupata mitihani ya theory na practical ambayo haina hesabu na amalizapo huenda intern takriban mwaka mzima, kwa practical zaidi chini ya Hospitali na madaktari ambao huendelea kumpika, Sasa mtihani wenu mnaowafanyisha unampima nini, kuliko madaktari waliokuwa nae na kumlea miaka yote na hatimaye mnawafanyisha mitihani tena kikanda tena wa theory?

Huenda nia ikawa nzuri japo sioni nia hiyo why wasifanye hiyo mitihani kwenye hospitali walizomalizia intern na bila malipo kama sio wizi na ufisadi.?

Na Kama huo mtihani una maana yoyote basi Madaktari wote kwa level mkiwemo na nyie mfanye. Kwamba muwatungie intern nao intern wawatungie tuone kama mtachomoka. Acheni kunyanyasa watu mara moja.

Mwisho
Waziri wa afya mpya najua wewe na Daktari, tena umesomea Urusi, niliona CV yako ebu wahoji hawa na wakupe majibu sahihi kwanini wanaleta wizi na uhuni mbele ya watanzania kwa mgongo wa chama cha Madaktari?

Watanzania siyo wajinga bwana.
 
dah haiseee inatia huchungu balaa.150k hembu semea sahana
 
Acha kulia lia wewe
Pharmacy
Maabara nurses
Wote wanafanya mitihani baada ya intern
Nyie kwa nn msifanye??
Sasa sio ombi ukitaka leseni ya udaktar piga paper Kama hutani hama nchi
Huo ndiyo utaratibu hata wizara inajua

Usituletee ukanjanja wenu hapa ni mwendo wa mitihani hadi ufaulu ndiyo upewe lesen yako
Tumegundua wengi weni wanapita njia za panya
Hapa kwetu mtagonga mwamba
Vijana someni narudia tena someniii
Tukutane kwenye mtihani
 
Hapo KUNA PHARMACY...MANESI NAO WEMBE ULE ULE..!! sasa sijui utasemaje
 
Kilio chako kimesikika, umeandika ovyo kwa hofu tu ili kujifichaficha ila uonevu , kuwanyanyasa madaktari wetu na kuwatesa kisaikolojia kupo kwenye huu mtihani, najaribu kuvaa viatu vyao mtu aliyesoma 5yrs plus 1yr internship halafu anapimwa kwa maswali kadhaa, udaktari ni mpana mno msiwanyanyase vijana wetu ama mnataka waikote makopo barabarani?

Hiki kitu kimepangwa na watu wachache wenye roho mbaya, ila ninaimani Mh Gwajima mama mwenye hekima zake atalitatua hili
 
Uzi mzuri sana na unapoint mbili muhimu bahati mbaya muandishi amekosea sana maandishi yake mpaka uzi umetaka kupoteza maana ila umeeleweka ...

Kuna sehemu kanichekesha sana

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] "... kwamba muwatungie intern nao intern wawatungie tuone Kama mtachomoka ... "
 
Mkuu sipo apa kwa kiswahili Safi,kina wenyewe bati ujumbe ufike,mengine badae, ila elewa watu usomea miaka mitatu lugha hii
Inalela Sana, tz wizi kila mahali why
Ujumbe hauwwzi kufika kwa style hiyo
Yaani Mtu akisoma tu huo utopolo haendelei Tena kusoma
Sasa hapo ujumbe utafika?
 
Yani balaa tupu[emoji23][emoji23][emoji23] disco limeingia masai..! Yani chama cha Madoctor wataumia sana walikuwa wapi miaka yotee hizii hela zilikuwa zinawapitaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndiyo tumerudi rasmi Sasa
Lazima tuwachuje na sisi
 
Unazungumza kitu gani wewe,mnaibiwa pia,phamarcy,nurse miaka mingapi, linganisha na madactari, by the way bado ni wizi tu, lakini apa nimezungumzia madactari
Utaelewa tuu
We endelea kulia haisaidii ishapita hiyo
Ni mwendo wa mitihani hadi ufaulu ndiyo upewe lesen yako
 
Wewe kama ni daktari utatumalizia watu.! Yaani usome shule ya msingi miaka 7, upili miaka 4, advanced miaka 2, usome miaka 5 udaktari halafu usijue hata kuandika neno daktari!?? Hiyo uliyoandika sijui ni lugha gani!??
Siko hapa kwa lugha zaidi ujaelewa kaa kaa pembeni
 
Back
Top Bottom