Chama cha Madaktari acheni wizi kwenye kutoa leseni za Madaktari wapya

Chama cha Madaktari acheni wizi kwenye kutoa leseni za Madaktari wapya

Kilio chako kimesikika, umeandika ovyo kwa hofu tu ili kujifichaficha ila uonevu , kuwanyanyasa madaktari wetu na kuwatesa kisaikolojia kupo kwenye huu mtihani, najaribu kuvaa viatu vyao mtu aliyesoma 5yrs plus 1yr internship halafu anapimwa kwa maswali kadhaa , udaktari ni mpana mno msiwanyanyase vijana wetu ama mnataka waikote makopo barabarani? Hiki kitu kimepangwa na watu wachache wenye roho mbaya, ila ninaimani Mh Gwajima mama mwenye hekima zake atalitatua hili
Wewe ni mmoja wa wahusika,hakuna vya buledunia hii, unaficha madhambi kupitia Gramma, nasema wizi Kama huu ni wizi Kama wizi mwingine.

Jibu, mtiani husika unawasaidiaje?

Tanzania imekua kichaka kila mtu atengeneza jinsi ya kutengeneza faida pitia kwa mwenzake,maneno ya hajabu Sana haya TOKA kwako ninae kufahamu vizuri
 
Pigeni tu pepa hakuna kulialia Engineer yeye mbona anakomaa 4years Chuo plus 3years intern. total 7years ndiyo unapata leseni ukizingua presentations utapata leseni uzeeni. Hatari sana bodi professional za hapa bongo.​
 
Acha kulalamika wewe ,tatizo madaktari hua mnajikweza sana ,mbona wenzenu kozi zote wanafanya mitihani toka muda kwa level zote hujawahi sikia wakilalamika ,nyie mmeanza mwakahuu tu tayari mmeanza kutoa povu,kama mnahitaji muondolewe hio mitihani yaleseni basi nawenzenu waondolewe ,I mean , pharmacist, scientist, technician,nurses etc maana Sasa umekua niutaratibu waserikali kupima competency kwawote ,ila wakipimwa wenzenu sawa ,mkipimwa nyie povu na waraka mrefu
 
Kijana umeenda huko China kwenye vyuo vya uchochoroni unakuja huku internship nzima machief wanakushangaa hujui vitu upo upo tu vitu common kabisa hauvijui yani kilaza kilaza kwenye ward rounds unatetemeka halafu unaogopa professional exam?

Nikuhakikishie tu, huo mtihani ni namna nyingine ya kuchuja na kujua nani kanjanja na nani amepikwa. Bado kuna continuous professional development. Hatutaki madaktari vilaza watakaotuua.

Kafanye mtihani kijana, udaktari ni fani ya watu wenye akili kama una uweo mdogo njoo tufyatue matofali nayo ni kazi na tunaishi vizuri tu.
 
Mkuu sory lugha Zina wenyewe ,lengo ni kwamba watoe majibu mtiani unamsaidiaje mlengwa, kutokana na hatua nilizozotaja Kama sio wizi tu
Pamoja na ujumbe wenye kusudi zuri, lakini unafanya tuhoji kama kweli wewe ni mwana taaluma hii ya uganga wa binadamu (Medical doctor), kiswahili ulichoandika ni tabu, nikafikiri labda kwa kuwa umesoma kwa kutumia lugha ya kigeni (kiingereza) kwa muda mrefu basi utakuwa sawa kwene uandishi wa lugha hiyo...huko nako naona una tabu ...ona ulivyoandika neno"sorry"! inasababisha wenye kufikiri wahoji uwezo wako!
 
Sijaoina point yako hapo.. Exams baada ya intern ni kitu cha kawaida ktk nchi yoyote.

Usitafute huruma hapa . Tena lipieni hata 300000 ili kufidia gharama za uandaaji na kusaisha. Si huwa mnalipwa mshahara (80%) ya salary ya Dr?!? Mnaishia kununua tv na music system.

Akili yako haijakuwa ww.
 
Wako sahihi sasa hivi kuna vyuo vingi vinatoa kozi ya udaktari lakini vingine vinazalisha madaktari bomu, wafanye hivyo ili kulinda taaluma yao.
 
mtihan unendelee ili kusud kama ujnanja ujnaja pepa ikutene
 
Hata watu wa procurement uko ndo kuna utumbo na uozo vibaya mno SHAME ON YOU PSPTB.mnawaibia sana vijana masikini wasio na ajira pesa zao...raisi ipitie hii board uone uozo uliopo...
 
Chama cha madaktari (MAT) hakihusiki na usajili wa madaktari. Usajili hufanywa kwa mujibu wa sheria chini ya Medical Council of Tanganyika (MCT).

You may want to edit your heading if you intend to talk about MCT.
 
Sijaoina point yako hapo.. Exams baada ya intern ni kitu cha kawaida ktk nchi yoyote.

Usitafute huruma hapa . Tena lipieni hata 300000 ili kufidia gharama za uandaaji na kusaisha. Si huwa mnalipwa mshahara (80%) ya salary ya Dr?!? Mnaishia kununua tv na music system.

Akili yako haijakuwa ww.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]analipwa mil 1.2 mwaka mzimaa kuirudishia serikali 180k anaona ni utapelii
 
Nawapenda sana wafamasia..shule yao ni konki sana na pepa zao ni konki sana...but nyie doctors pepa zenyewe mnafanya MCQ mshaanza kulia lia..

Bado kazini kuna continuous professional exams ..ni jiwe juu ya jiwe..

Doctors,pharmacist and nurses,radiology..hizi ni life learning professional..

Kila siku kuna mabadiliko ya sayans na technology lazima kusoma na kufanya exams ili kujiupdate.

Acha kulialia kijana...
 
Pamoja na ujumbe wenye kusudi zuri, lakini unafanya tuhoji kama kweli wewe ni mwana taaluma hii ya uganga wa binadamu (Medical doctor), kiswahili ulichoandika ni tabu, nikafikiri labda kwa kuwa umesoma kwa kutumia lugha ya kigeni (kiingereza) kwa muda mrefu basi utakuwa sawa kwene uandishi wa lugha hiyo...huko nako naona una tabu ...ona ulivyoandika neno"sorry"! inasababisha wenye kufikiri wahoji uwezo wako!
Kuna mtu hapa kwakwe akili au uwezo wa mtu anaupima kwa lugha/maandishi

2020 nimeona mengi
 
Back
Top Bottom