Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu

Mnamo tarehe 26 Juni, 2023 manyabiashara Bw. Rostam Azizi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu masuala ya uwekezaji alinukuliwa akiituhumu aliyoiita Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake.
Hili ni tamko la kipuuzi na kipumbavu kabisa, sidhani kama majaji wenye akili timamu wanaweza kuandika huu ujinga, nadhani limeandikwa na kutolewa na UVCCM. Ngoja nilikosoe hapa.

1. Limeshindwa kuonyesha limetolewa na nani au mwenye nafasi gani katika hicho chama, ukiacha hata kusainiwa na aliyelitoa.

2. Halisemi linampa muda gani Rostam kuthibitisha au kukanusha. Hakuna popote linazungumzia ukomo wa muda.

3. Halisemi litamchukulia hatua gani Rostam ikiwa atashindwa kufanya vile linavyomtaka kufanya.
 
Wawe wakali wakati ni Kila mtu anajua hupewa maelekezo.Vinginevyo kesi kama ile ya wabunge wa mchongo 19 ingeshafikia tamati!
 
rostam yuko sahihi kwa alilolisema.mahakama zetu aidha zinafanya kazi kwa maelekezo au kwa kutojiamini.wananchi wengi wa hali ya chini haki zao hupokonya na hivi vyombo vya sheria na huwa zinawapendelea matajiri.mwizi wa kuku anafungwa miaka mingi lkn wahujumu uchumi wanaachiwa huru kila kikicha.
 
Tanzania hakuna mahakama. Kuna tawi la Ccm.
Kama jaji mkuu ana jua hawezi kutafsiri katiba na ana kubali kuongezewa muda wa kukaa ofisini, je tuamini kweli kuna mahakama??
Acheni siasa.
 
Kama namuona Dr. Slaa akichukua point zake 3.
Papa kuja uthibitishe uliona au kusikia wapi kisutu wakipigiwa simu au vi-memo
 
Hawa Majaji wana Tatizo- mtu kasema " wanaweza kupigiwa simu" - nini maana ya sentensi hii? wanaweza sio kwamba ni kweli... sasa labda wanathibitisha ya kwamba labda ni kweli ndio maana wanakuja juu...? Pigia mstaru - Wanaweza... si vinginevyo - labda - ni hisia tu..hujo mahakamani hakunaga kesi inayoamuliwa kwa hisia na wao wanajua rules ya self incrimination. Huyo Rostam akae tu kimya tuone kama watamfamya chochote... hawawezi- period !
 
Rostam sio Fala hata kidogo anajua anawamudu ndio maana kasema hivyo...hawamuwezi..
Period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…