Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu

Si kama wana ubavu wamfungulie mashtaka kwa kuidhalikisha mahakama. Ili sasa aje athibitishe.

Ngoja aje akiri hadharani sisi tufungue kesi kwa ushahidi wake wa kukiri.

Hii nayo ni kazi maana ajira hakuna
 
Mnamo tarehe 26 Juni, 2023 manyabiashara Bw. Rostam Azizi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu masuala ya uwekezaji alinukuliwa akiituhumu aliyoiita Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake.

Kutokana na taarifa hiyo tunapenda kuhabarisha umma yafuatayo:

Hakuna Jaji anayehudumu katika Mahakama hiyo kama ilivyoripotiwa na mzungumzaji wa taarifa hiyo.

Mahakama ya Tanzania ni chombo pekee cha utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote.

Uongozi wa Mahakama na au Chama Cha Majaji na Mahakimu haujawahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa mtu yeyote ikionyesha Maafisa wa Mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa maamuzi katika mahakama hiyo.

Kutokana na maelezo hayo Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania tunatoa kauli zifuatazo:
  1. Tumesikitishwa sana na kauli za Bw Rostam Aziz ambaye hatukutegemea aongee mambo mazito kama hayo bila kuwa na uhakika wala uthibitisho.
  2. Matamshi ya Bw Rostam Aziz yanaweza kuhatarisha uhusiano na ushirikiano katika mihimili mitatu ya dola ndani ya nchi yetu.
  3. Tunaomba wananchi wenye nia njema na Mahakama na mihimili mingine waendelee kuwa na Imani na mfumo wa utoaji haki nchini.
Kwa taarifa hii, Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania kinamtaka Bw. Rostam Azizi athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Kiongozi wa Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo.

Akishindwa kutoa uthibitisho tunamtaka atumie Jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.

Imetolewa na:
UONGOZI WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU TANZANIA (JMAT)
4 JULAI 2023

Pia soma: Rostam Aziz: Hakuna mwekezaji atakubali kuwekeza halafu umwambie aende Mahakama ya Kisutu ambapo Majaji wanaweza kupigiwa simu na watu wa Serikali
Mbona Magufuli alisema wazi kwamba mhimili wake umechimbiwa chini zaidi na hao majaji hawakusema kitu?

Kama walikubali mhimili wa rais umechimbiwa chini zaidi, watakataaje kwamba wanaweza kuamrishwa kwa simu kutoka Ikulu?
 
Yani huyu muhindi anapambana na mahakama!?? Je mahakama ikiamua kumfikisha mahakamani kwa uchafuzi wa jina si amekwisha asubuhi na mapema
Aishe kwa hapa Tanganyika au nchi gani?

Unamfahamu huyu jamaa tangia mwaka gani?

Je,unazifahamu mahakama,mahakimu na majaji wa Tanganyika?

Unajisahaulisha enzi za miaka 4 nyuma kabla ya leo DPP Biswalo alichokuwa akikifanya?
 
Mnamo tarehe 26 Juni, 2023 manyabiashara Bw. Rostam Azizi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu masuala ya uwekezaji alinukuliwa akiituhumu aliyoiita Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake.

Kutokana na taarifa hiyo tunapenda kuhabarisha umma yafuatayo:

Hakuna Jaji anayehudumu katika Mahakama hiyo kama ilivyoripotiwa na mzungumzaji wa taarifa hiyo.

Mahakama ya Tanzania ni chombo pekee cha utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote.

Uongozi wa Mahakama na au Chama Cha Majaji na Mahakimu haujawahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa mtu yeyote ikionyesha Maafisa wa Mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa maamuzi katika mahakama hiyo.

Kutokana na maelezo hayo Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania tunatoa kauli zifuatazo:
  1. Tumesikitishwa sana na kauli za Bw Rostam Aziz ambaye hatukutegemea aongee mambo mazito kama hayo bila kuwa na uhakika wala uthibitisho.
  2. Matamshi ya Bw Rostam Aziz yanaweza kuhatarisha uhusiano na ushirikiano katika mihimili mitatu ya dola ndani ya nchi yetu.
  3. Tunaomba wananchi wenye nia njema na Mahakama na mihimili mingine waendelee kuwa na Imani na mfumo wa utoaji haki nchini.
Kwa taarifa hii, Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania kinamtaka Bw. Rostam Azizi athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Kiongozi wa Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo.

Akishindwa kutoa uthibitisho tunamtaka atumie Jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.

Imetolewa na:
UONGOZI WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU TANZANIA (JMAT)
4 JULAI 2023

Pia soma: Rostam Aziz: Hakuna mwekezaji atakubali kuwekeza halafu umwambie aende Mahakama ya Kisutu ambapo Majaji wanaweza kupigiwa simu na watu wa Serikali
Wanakimbia kivuli chao..!! Jua likiwaka tu na huku wapo juani, hiki hapa..!!
 
Nchi yetu ina double standards, angesema raia wa kawaida angekuwa polisi sasa hivi! Mpaka majaji wanalalamika kwanini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa?
 
Hawana ubavu wa kumfanya chochote.
Kama mdogo wake alipiga meno na Raisi wa Chato alishindwa cha kumfanya wataweza wao kwake yeye...!
 
Changamoto ni kwamba Rostam sio mwenzetu, au sio size yetu.

Yule ni intelligent kupita sote! Sio mara chache akihusishwa na CIA ya USA
 
Majaji na mahakimu wanaandika Taarifa kwa umma kama wanaharakati na wanasiasa?

Wanatakiwa wamwandikie summons aje a appear mbele Yao ku SHOW COURSE

Contempt of the court sio kanjubal kupiga chafya kwenye chumba Cha mahakama au kuongea wakati mahakama INAENDELEA tuu Bali ni jambo lolote lililofanywa ,au kusemwa lenye lengo la makusudi kuidharau mahakama
 
Ule mhimili uliojichimbia chini zaidi unaweza kupiga simu moja tu mahakamani au bungeni na panya wote wakafyata mkia, nafikiri ndo alichomaanisha Rostam.

Kwenye swala la spika wa bunge kuondoka madarakani kwa pressure ya rais ni udhihirisho tosha. Katika hali ya kawaida spika ndo anaweza kuitisha kura ya kumwondoa rais madarakani, lakini kwa hapa bongolala ni kinyume chake, rais ndo anamwondoa spika madarakani.​
 
Tena kipindi cha Jiwe, Majaji wengi walikuwa wanafuata matakwa yake na maagizo...
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kati ya mwaka 2017/2018 alisema kwa kunukuu " Mahakama mnahitaji pesa harakisheni hukumu ili na nyie mpate bajeti ya kukarabati maeneo yenu "
Maana yake toeni hukumu za kulazimisha malipo mpate fedha... Hayo yalikuwa maagizo ya waziwazi
 
Watu weupe wanaonewa sana, hilo liangaliwe kwa karibu.. na wengine hutafuta pesa kwa njia za ulaghai kupitia watu weupe,
 
Mnamo tarehe 26 Juni, 2023 manyabiashara Bw. Rostam Azizi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu masuala ya uwekezaji alinukuliwa akiituhumu aliyoiita Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake.

Kutokana na taarifa hiyo tunapenda kuhabarisha umma yafuatayo:

Hakuna Jaji anayehudumu katika Mahakama hiyo kama ilivyoripotiwa na mzungumzaji wa taarifa hiyo.

Mahakama ya Tanzania ni chombo pekee cha utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote.

Uongozi wa Mahakama na au Chama Cha Majaji na Mahakimu haujawahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa mtu yeyote ikionyesha Maafisa wa Mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa maamuzi katika mahakama hiyo.

Kutokana na maelezo hayo Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania tunatoa kauli zifuatazo:
  1. Tumesikitishwa sana na kauli za Bw Rostam Aziz ambaye hatukutegemea aongee mambo mazito kama hayo bila kuwa na uhakika wala uthibitisho.
  2. Matamshi ya Bw Rostam Aziz yanaweza kuhatarisha uhusiano na ushirikiano katika mihimili mitatu ya dola ndani ya nchi yetu.
  3. Tunaomba wananchi wenye nia njema na Mahakama na mihimili mingine waendelee kuwa na Imani na mfumo wa utoaji haki nchini.
Kwa taarifa hii, Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania kinamtaka Bw. Rostam Azizi athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Kiongozi wa Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo.

Akishindwa kutoa uthibitisho tunamtaka atumie Jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.

Imetolewa na:
UONGOZI WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU TANZANIA (JMAT)
4 JULAI 2023

Pia soma: Rostam Aziz: Hakuna mwekezaji atakubali kuwekeza halafu umwambie aende Mahakama ya Kisutu ambapo Majaji wanaweza kupigiwa simu na watu wa Serikali

Abebe ile clip pendwa ya jiwe yenye kuunasibu bayana Ile mhimili uliojichimbia zaidi.

Wakikiri kuusikia ujumbe huo na kutomkana aliyeyatamka hadharani mchana kweupe, basi Rostam atakuwa hana kesi.

"Go Rostam go mifano Hadi ya kesi za akina Mboye ziko upande wako!"
 
Back
Top Bottom