Chama cha Mapinduzi champongeza Rais Samia kwa kuimarisha Demokrasia

Chama cha Mapinduzi champongeza Rais Samia kwa kuimarisha Demokrasia

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza na kumshukuru amiri Jeshi mkuu na Rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa Uzalendo wake kwa Taifa, Ushupavu na Ujasiri katika kulinda na kusimamia "Tunu za Taifa" letu kwa nguvu zake zote kwa akili zake zote na kwa moyo wake wote huku msingi mkuu wa yote haya ukiwa ni kuwaletea wananchi hawa masikini maendeleo endelevu.

Pamoja na hilo,Chama cha Mapinduzi pia kimempongeza na kumsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwathamani watumishi wa umma nchini ikiwa ni baada ya zaidi ya watumishi 180,000 kupandishwa vyeo (kuongezwa mishahara) na Wale wote wanaodaiwa mikopo ya bodi (HESLB) ambao kila mwezi walikatwa 15% ya Mshahara wao Mhe Samia Suluhu Hassan kawaondolea hiyo Value Retention Fee (VRF) ambayo ilikuwa ni 6% nakuwafanya wakatwe 9% tu kwa mwezi hivi leo.

Chama cha mapinduzi kimempongeza pia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza kodi ya Mishahara kwa watumishi wote wa Umma na binafsi yaani (PAYE) kutoka 9% ya awali hadi 8% hii yote ni nia ya Serikali ya CCM katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu.

Chama kimempongeza zaidi Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia Utawala wa Sheria na Utawala bora, Haki za kibinadamu, Ukuzaji mkubwa wa demokrasia ya vyama vingi nchini, kujenga inchi isiyoyegemea itikadi ya dini|kabila|kanda yeyote na kuufurusha kila aina ya Ufisadi na Rushwa nchi.

Haya yamesemwa na Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi CCM Taifa Mhe Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akiongea na Wanahabari Ofisi ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam.

photo_2021-10-13_09-22-29.jpg
 
Hakika!

Rais wetu mpendwa Samia ameonyesha ushupavu wa hali ya juu.

ushupavu wake na Uimara wake alio uonyesha ndani ya muda mfupi umetufanya watanzania wote tujiamini zaidi.

tunamuomba aendelee hivyo hivyo.

tunamuombea Mungu azidi kumlinda.
 
Asante Sana chama changu cha CCM ,
Chama kinafanya kazi nzuri sana ya kuongoza serikali,

Chama kinamshauri Rais mambo yenye manufaa kwa Taifa,

Hongera CCM, Hongera Rais Samia
 
Mama anastahili pongeza sana wakati wote,
Mungu ampe ujasiri zaidi
 
CCM YAMPONGEZA, ni watu 9 wanakaa wanasema wamempongeza. Ccm ina wanachama zaidi ya 10 milioni wasikilizeni wanasema nini kuhusu maza.
 
Chama kimempongeza zaidi Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia Utawala wa Sheria na Utawala bora, Haki za kibinadamu, Ukuzaji mkubwa wa demokrasia ya vyama vingi nchini, kujenga inchi isiyoyegemea itikadi ya dini|kabila|kanda yeyote na kuufurusha kila aina ya Ufisadi na Rushwa nchi.
Hapa kuna kaukakasi kwa kiasi flan si dhani kama wanachosema kina ukwel ndani yake
 
Hakika!
Rais wetu mpendwa Samia ameonyesha ushupavu wa hali ya juu...
Hakika Rais wetu anastahili pongezi sana,

Mambo anayoyafanya yalishindikana miaka na miaka,

Leo amejitahidi katika sekta mambo yanakwenda,

Hongera CCM || Hongera Rais Samia
 
Asante Sana chama changu cha CCM ,
Chama kinafanya kazi nzuri sana ya kuongoza serikali,

Chama kinamshauri Rais mambo yenye manufaa kwa Taifa,

Hongera CCM, Hongera Rais Samia
Endelea kukipigania mkuu,

Endelea kumpigania Rais wetu mnyenyekevu
 
Back
Top Bottom