Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongolo anaongea na taifa muds huu.
Yuko mubashara channel ten
Updates;
Katibu mkuu ameagiza serikali ipeleke fedha za ujenzi wa miundombinu kwenye halmashauri ili ifikapo December kazi zote ziwe zimekamilika ibakie swala la kupokea wanafunzi tu wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza.
Katibu mkuu ndugu Chongolo amemuomba radhi Rais Samia kufuatia kitendo cha gazeti la uhuru kumlisha maneno.
Katibu mkuu amelifungia gazeti la uhuru kwa siku 7
Bodi ya Wakurugenzi imewasimamisha kazi mkurugenzi wa Uhuru Dr Sungura na mhariri mkuu.
Chongollo amesema Katiba mpya ni takwa la wanasiasa kwa sababu hakuna pahala Wananchi wamedai katiba mpya.
Mungu ni mwema wakati wote!