Chama cha riadha kidhibiti hizi marathon za kihuni zinazofanyika kiholela kama hii Akili Marathon

Chama cha riadha kidhibiti hizi marathon za kihuni zinazofanyika kiholela kama hii Akili Marathon

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Mimi kama mdau mkubwa wa riadha ninaandika kwa huzuni kutokana na malalamiko ya watu kuhusu mbio za Akili Education Marathon. Walioshiriki wamejitokeza hadharani na kutupa lawama za kutosha kwa waandaaji. Wanasema mbio zilichelewa kuanza na huduma barabarani zilikuwa za kishenzi sana. Maji yalikuwa adimu na hata medali zilikuwa hakuna. Kimsingi uratibu ulikuwa wa kipumbavu.

Mbaya zaidi wanariadha waliotakiwa kulipwa walipewa cheques badala ya cash. Na hizo cheques zenyewe ni za kusubiria kwa siku kadhaa ili uweze kutoa hela. Mimi kama mtoto wa mjini nimenusa harufu mbaya sana ya utapeli kwa kuwapa watu cheques.

Ninasihi chama cha riadha kisiwe kinatoa vibali vya mbio zisizo na msaada kwa nchi. Nchi ina mbio nyingi ila haitoi mwanariadha wa ngazi ya dunia kuonyesha kuwa ni mbio za kihuni.
 
Sehemu ambayo wake za watu wanadanga live bila chenga basi ni kwenye hizi marathon uchwala.
 
Back
Top Bottom