Pre GE2025 Chama Gani kina sera za kueleweka kuelekea 2024/2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwa bahati mbaya Afrika umaskini, maradhi na ujinga ni mkubwa kiasi kwamba waafrika tumeachwa hoi tumetopea kwenye ugiligili wa shida zetu hata kushindwa kuwa na vipaumbele vyetu.

Mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.

Hivi mpaka Sasa kama watanzania tumeshajua ni chama gani kina sera nzuri za kutatua matatizo yetu tuliyonayo kwa kupambana na maadui zetu watatu Ujinga, Maradhi na Umaskini!?
 
CCM Wana Sera zinazoeleweka hata kama nyingine hazikubaliki

Wapinzani Sera yao Kuu ni kupata Kura za Kuwapa Ruzuku iliyonona
Ccm nyie bado mnasiasa zilizopitwa na wakati mkifika wakati wa uchaguzi sera zenu ni zile zile tumejenga Barabara,mitaro tumenunua ndege nk

Wakati chadema wanafanya siasa za kisasa zinazotuletea mabadiliko ya mfumo mzima wa uongozi bado chadema ni chama changu Bora muda wote
 
Mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.

Hivi mpaka Sasa kama watanzania tumeshajua ni chama gani kina sera nzuri za kutatua matatizo yetu tuliyonayo kwa kupambana na maadui zetu watatu Ujinga, Maradhi na Umaskini!?
Kwa upande wa vyama, Tanzania we are very unfortunately, hatuna vyama kabisa in a real sense ya vyama vya siasa!, hivyo Watanzania hatuna choice to choose from, tuna chama kimoja tuu, the one.and only, kile chama chetu!, tena sio chama cha siasa, ni chama dola!, ni dola!. CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

Uchaguzi wa Tanzania ni kugombea kisu cha makali kuwili, huku mmoja ameshika mpini! Hivyo unategemea nini?.

P
 
Hakuna chama chenye sera ya kumkomboa mTanganyika, labda kuna watu wachache wenye sera za kumkomboa mTanganyika.
 
Kwa mfano chama gani kina sera nzuri kuhusu:

1. Uhifadhi wa mazingira

2. Ajira

3. Haki za jamii

4. Mahusiano ya kimataifa

5. uchumi

6. Ustawi wa jamii

7. Ulinzi na usalama wa nchi

8. michezo na burudani

9. Nishati.
 
Kwa bahati mbaya Afrika umaskini, maradhi na ujinga ni mkubwa kiasi kwamba waafrika tumeachwa hoi tumetopea kwenye ugiligili wa shida zetu hata kushindwa kuwa na vipaumbele vyetu.

Mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.

Hivi mpaka Sasa kama watanzania tumeshajua ni chama gani kina sera nzuri za kutatua matatizo yetu tuliyonayo kwa kupambana na maadui zetu watatu Ujinga, Maradhi na Umaskini!?
Tofauti na CCM hakuna Vyama Kwa mbali ACT ,hicho Kingine kinategemea matukio ila hakina sera zozote.

Aliyewahi kushika sera ya maana Chadema aweke hapa
 
Chini ya Samia CCM kidogo naikubali, baada ya miaka ile ya magufuli ya kukimbiza wawekezaji, kuvuruga wafanyabiashara, kuvuruga demokrasia na utawala wa sheria na kuvuruga mahusiano na majirani na nchi za ng'ambo
Kidogo Samia anaeleweka japo mapungufu yapo

Chadema chini ya Tundu Lissu, ambaye ndie amekua kama De facto party leader, naona imekuwa very extreme, intolerant, na ya kibaguzi, haina sera, sera yao wanakuambia ukiitoa CCM matatizo ya nchi hii yanakwisha....hawana alternative inayoeleweka kuhusu uchumi wala mambo ya kijamii, ni vululuvululu tu, na ukiwa challenge kidogo kuhusu sera na mikakati yao unaambulia matusi
 
Hakuna cha Sera wala nini ni Sound tu bora zamani walikuwa wanadanganya kwa kupiga sound wapate kura siku hizi wala hawana huo muda wa kudanganya.... hadi nilishajiuliza...

Tofauti na CCM hakuna Vyama Kwa mbali ACT ,hicho Kingine kinategemea matukio ila hakina sera zozote.

Aliyewahi kushika sera ya maana Chadema aweke hapa
Sera ya Chadema tangu awali ilikuwa kumilikisha mabwanyenye njia Kuu za uchumi ila walipomchumkua Dr Slaa kutokea CCM Ndio wakajivuruga na kupoteza mwelekeo
 
Chini ya Samia CCM kidogo naikubali, baada ya miaka ile ya magufuli ya kukimbiza wawekezaji, kuvuruga wafanyabiashara, kuvuruga demokrasia na utawala wa sheria na kuvuruga mahusiano na majirani na nchi za ng'ambo
Kidogo Samia anaeleweka japo mapungufu yapo

Chadema chini ya Tundu Lissu, ambaye ndie amekua kama De facto party leader, naona imekuwa very extreme, intolerant, na ya kibaguzi, haina sera, sera yao wanakuambia ukiitoa CCM matatizo ya nchi hii yanakwisha....hawana alternative inayoeleweka kuhusu uchumi wala mambo ya kijamii, ni vululuvululu tu, na ukiwa challenge kidogo kuhusu sera na mikakati yao unaambulia matusi
Kwamba kuna Sera za Magufuli, Samia na Tundu Lissu ? Tupo enzi za Ufalme au demokrasia ya vyama vingi ? In short unachosema hivi vyama havina Sera bali maamuzi ya kiongozi ataamka vipi

Na huku so called kufungulia nchi madhara yake yatalitafuna vizazi mpaka vizazi..., huitaji kubembeleza watu waje kuchuma resources bali wao ndio wakubembeleze ukishaonekana weak kwenda negotiations utaishia kugawa kila kitu (unless kama unanufaika katika ugawaji AKA 10%) Na on paper hizo privatization ni more of CHADEMA kuliko CCM
 
Back
Top Bottom