Pre GE2025 Chama Gani kina sera za kueleweka kuelekea 2024/2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa bahati mbaya Afrika umaskini, maradhi na ujinga ni mkubwa kiasi kwamba waafrika tumeachwa hoi tumetopea kwenye ugiligili wa shida zetu hata kushindwa kuwa na vipaumbele vyetu.

Mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.

Hivi mpaka Sasa kama watanzania tumeshajua ni chama gani kina sera nzuri za kutatua matatizo yetu tuliyonayo kwa kupambana na maadui zetu watatu Ujinga, Maradhi na Umaskini!?
WA KWANZA WEWE NA WAPILI CCM
 
Chama cha siasa ni kikundi cha watu wanaoshirikiana pamoja kwa msingi wa imani, malengo, na sera za kisiasa. Kwa kawaida, chama hicho huwa na mfumo wa kuongoza na utaratibu wa kufanya maamuzi. Lengo lake kuu ni kutafuta madaraka au kushika madaraka ili kuweza kutekeleza sera zake na kusimamia maslahi ya wanachama wake na mara nyingine ya jamii kwa ujumla. Katika mifumo ya kisiasa ya kidemokrasia, chama cha siasa hushiriki katika uchaguzi kwa kuwawakilisha wagombea wao, na hivyo, wananchi huweza kuchagua viongozi na sera wanazopendelea.
 
Kwa bahati mbaya Afrika umaskini, maradhi na ujinga ni mkubwa kiasi kwamba waafrika tumeachwa hoi tumetopea kwenye ugiligili wa shida zetu hata kushindwa kuwa na vipaumbele vyetu.

Mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.

Hivi mpaka Sasa kama watanzania tumeshajua ni chama gani kina sera nzuri za kutatua matatizo yetu tuliyonayo kwa kupambana na maadui zetu watatu Ujinga, Maradhi na Umaskini!?
Naomba kueleweshwa kuhusu sera ni nini na ninani Huwa anazitengeza Madhumuni yake ni yepi
 
Nakujibu Kwa njia ya mkato maana sera ni somo Pana Sana.

Chama cha siasa huwa kinakuwa na falsafa inayokiongoza kutafsiri ulimwengu. CCM inaamini maisha ya binadamu yanategemea kundi la watu ili kufanikiwa wakati CHADEMA wanaamini maendeleo yataletwa na mtu binafsi.

Hizo falsafa ndiyo hujenga msingi wa sera. Kwa kuwa CCM huamini maendeleo huletwa na kundi la watu kufanya kazi pamoja wao itikadi yao ni UJAMAA.

Na kwa kuwa CHADEMA wanaamini kuwa maendeleo yataletwa na mtu binafsi, wao itikadi yao ni ubepari.

Sasa hizi itikadi za UJAMAA na UBEPARI ndiyo hutumika kwenye kutengeneza sera. Kila chama hutengeneza sera kwa kufuata Itikadi ya chama husika.
 
Ujamaa Bado upo Duniani?

Nyerere alitaka kuiga Ule Ujamaa wa Yesu Kristo na Wanafunzi wake lakini ukamshinda 😄
 
Kwa bahati mbaya Afrika umaskini, maradhi na ujinga ni mkubwa kiasi kwamba waafrika tumeachwa hoi tumetopea kwenye ugiligili wa shida zetu hata kushindwa kuwa na vipaumbele vyetu.

Mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.

Hivi mpaka Sasa kama watanzania tumeshajua ni chama gani kina sera nzuri za kutatua matatizo yetu tuliyonayo kwa kupambana na maadui zetu watatu Ujinga, Maradhi na Umaskini!?
Sasa unauliza nini chama ni ccm tu hivyo vingine malengo ruzuku!
 
Ujamaa Bado upo Duniani?
Kinadharia bado upo pale unapopingana na Marekani.

Hata nchi zinazojiita z kikomunisti ni kundi dogo la watu hutumia hatamu za umma kujitajirisha kwa hoja ya kutetea wanyonge.

Kimsingi UJAMAA- mamboleo ni udanganyifu unaofanywa na wanasiasa kujitajirisha kwa kuifanya ni sehemu ya watu wanaogandamizwa!!
 
Wanyonge real sio hao matapeli
Unyonge ni Falsafa ya Kiroho yaani watu walioumizwa na kukata tamaa

Mfano Mzuri wa Wanyonge ni hawa CHAWA wa Kwenye Siasa ukiwaangalia wengi wao Wana maskendo ya kuwapeleka Jela Lakini Vyama vimewanasa na vinawatumia bila Wao Kupenda

We angalia nyuso zao tu, ni watu Wenye hela Lakini hawanaga furaha kabisa 🐼
 
Automatically watu walizaliwa wanyonge,jamii ipi hiyo sio wanyonge?
Kila jamii ina maskini ila siyo Kila jamii Ina wanyonge.

Wanyonge ni zao la kugandamizwa. Kila penye wanyonge jua kuna ugandamizaji wa haki za binadamu.

Ule msemo wa "mnyonge mnyongeni, ila haki yake mpenzi" unasawiri hoja yangu.
 
Kwamba kuna Sera za Magufuli, Samia na Tundu Lissu ? Tupo enzi za Ufalme au demokrasia ya vyama vingi ? In short unachosema hivi vyama havina Sera bali maamuzi ya kiongozi ataamka vipi

Na huku so called kufungulia nchi madhara yake yatalitafuna vizazi mpaka vizazi..., huitaji kubembeleza watu waje kuchuma resources bali wao ndio wakubembeleze ukishaonekana weak kwenda negotiations utaishia kugawa kila kitu (unless kama unanufaika katika ugawaji AKA 10%) Na on paper hizo privatization ni more of CHADEMA kuliko CCM
Ndio, kwa Tanzania vyama havina sera ni maamuzi ya mtu mmoja, hata Upinzani ni hivyo hivyo,

Kufungulia nchi ndio kulifanya hata baba zako wakawa wanamudu kununua sabauni, walikuwa hawawezi

Tanzania haina uspesho wowote, ni nchi yenye rasilimali ghafi nyingi, lakini haiwezi kuzivuna kwa tija kama nchi nyingi za Afrika zilivyo
Unahitaji sera friendly kwa uwekezaji wafanye uzalishaji wenye ufanisi na kukuza pato la nchi na kukuza ajira

Vitu vya maana unavyoviona nchi hii, kama benki kubwa, mitandoa mikubwa ya simu, ni matunda ya uwekezaji sio utopia za kujifungia
 
Nakujibu Kwa njia ya mkato maana sera ni somo Pana Sana.

Chama cha siasa huwa kinakuwa na falsafa inayokiongoza kutafsiri ulimwengu. CCM inaamini maisha ya binadamu yanategemea kundi la watu ili kufanikiwa wakati CHADEMA wanaamini maendeleo yataletwa na mtu binafsi.

Hizo falsafa ndiyo hujenga msingi wa sera. Kwa kuwa CCM huamini maendeleo huletwa na kundi la watu kufanya kazi pamoja wao itikadi yao ni UJAMAA.

Na kwa kuwa CHADEMA wanaamini kuwa maendeleo yataletwa na mtu binafsi, wao itikadi yao ni ubepari.

Sasa hizi itikadi za UJAMAA na UBEPARI ndiyo hutumika kwenye kutengeneza sera. Kila chama hutengeneza sera kwa kufuata Itikadi ya chama husika.
Nimeuliza pia Madhumuni ya sera, hua nasikia kuna sera ambazo hazina muelekeo
 
Madhumuni ya sera ni kuweka msingi Kwa "Ilani ya Uchaguzi" ambayo ni mpango wa kutekeleza sera.

Sera ipo ili mipango yote ya nchi ifanane na falsafa ya chama husika.
Kwanini hutengenezwa sera ambazo hazina muelekeo yaani sera ambazo hazina tija je wabunge huwa wanayajua madhara ya sera wanazo zipitisha? Kwa hapo baadae, (the aftermath of policies approved)
 
Kila jamii ina maskini ila siyo Kila jamii Ina wanyonge.

Wanyonge ni zao la kugandamizwa. Kila penye wanyonge jua kuna ugandamizaji wa haki za binadamu.

Ule msemo wa "mnyonge mnyongeni, ila haki yake mpenzi" unasawiri hoja yangu.
Nani anagandamizwa Sasa? Wanyonge hutoka kwenye kundi la maskini na lazima walindwe
 
Back
Top Bottom