CHAMA hana msaada tena kwa timu ya Simba

CHAMA hana msaada tena kwa timu ya Simba

Kwangu mimi naona Chama bado ni msaada sana kwa Simba kwani akili zake za mpira bado zinahitajika sana uwanjani kubadilisha matokeo japo mwili taratibu umeanza kukataa. Kwa umri wa Chama ulipofika na dakika anazopewa uwanjani ni sahihi kabisa na kwa hili kocha apongezwe.

Hii ya kulazimisha Chama acheze dakika nyingi kama ilivyokuwa miaka tatu nyuma ni kutaka Chama apotee mazima mapema kama alivyolazimishwa Boko awe anacheza dakika nyingi uwanjani wakati umri umeenda matokeo yake Boko sasa ameanza kupotea mazima. Kwa viongozi wa Simba inatakiwa watafute mbadala wa Chama haraka kwani wamechelewa ilitakiwa ameshaptikana toka msimu ulioisha.
Hakuna team serious itakuwa na mchezaji kama chama kwa sasa.
 
Habari za Jumapili wanajukwaa.
Nianze kwa kusema tu kwamba kiuhalisia Jana Simba wamecheza vizuri sana kabla ya Sub Moja haijafanywa, na swala la simba kufungwa 1 tu na Wydad linadhihirisha kua Soka La Bongo Limekua.
Tusilete porojo eti Wydad wabovu au Al Ahly kutoa Sare na Yanga basi Ahly wabovu hapan soko letu limekua na Team hizi zimewekeza Kweli kweli.

Ila kitu nachotaka kukiongelea hapa ni Role ya Chama pale UNYAMANI,Huyu jamaa huenda Mashabiki wa Simba wataanza kukubaliana na Zoran aliesema Chama hafai na wakampigia kelele,akafata Robetinho akawa anampiga Sub wakapiga Kelele,
Saiv Benchika anafanya hivohivo anampiga Bench inaonyesha Kua kweli Chama sio Material ya simba ila Simba na mashabiki zao MBUMBU ndio wana force wao simba wawe Material ya CHAMA.

Kwa walio angalia Match ya Jana moja Ya Sub iliyoharibu game ya Simba ni ile Kumtoa ONANA na kumuingiza CHAMA.

Ukweli baada ya Chama kuingia simba ikawa na defensive mind zaidi ikawa inapoteza mipira zaid pale mbele Chama sio mzuiaji ila kwa game yake anavyochezaga ni mfumo wakujilinda sana coz mipira mingi ilianza kurudi nyuma sana na Chama akawa hana speed pia akawa hawez ku hold mpira anapokonywa mali inaenda.

Mwisho Kukataliwa na Walimu wa 3 inadhihirisha Chama sio Material yenu ila kwa umbumbu wenu ndio mnalazimisha mukae kwenye mfumo wa Chama.

#DOMINIKA NJEMA
Enzi za Chama Kondeboy zimekwisha. Wa kulaumiwa ni viongozi wa Simba kuwauza hawa jamaa kwani kule uarabuni walienda kusugua bench na ndiyo mpira ulipoishia
 
Hakuna watu wanakera pale Simba kama
Mashabiki wa Phiri na Chama.
Hawa watu ndio mbumbumbu wenyewe sasa.
Na sio mda utawaona hapa.
Chama anazingua ila Phiri pale Simba ni Kila kitu, yule jamaa ni striker.
Dakika 80 zote baleke hajapiga hata shot 1 on target Kaz kuruka ruka tu. Phiri kaingia kaanza kujaribu hadi ya mbali
 
Chama anazingua ila Phiri pale Simba ni Kila kitu, yule jamaa ni striker.
Dakika 80 zote baleke hajapiga hata shot 1 on target Kaz kuruka ruka tu. Phiri kaingia kaanza kujaribu hadi ya mbali
Naona mmefika sasa mashabiki wa Phiri.
 
Chama anazingua ila Phiri pale Simba ni Kila kitu, yule jamaa ni striker.
Dakika 80 zote baleke hajapiga hata shot 1 on target Kaz kuruka ruka tu. Phiri kaingia kaanza kujaribu hadi ya mbali
Phiri alivyo ingira timu ilibadilika sana
 
Kwangu mimi naona Chama bado ni msaada sana kwa Simba kwani akili zake za mpira bado zinahitajika sana uwanjani kubadilisha matokeo japo mwili taratibu umeanza kukataa. Kwa umri wa Chama ulipofika na dakika anazopewa uwanjani ni sahihi kabisa na kwa hili kocha apongezwe.

Hii ya kulazimisha Chama acheze dakika nyingi kama ilivyokuwa miaka tatu nyuma ni kutaka Chama apotee mazima mapema kama alivyolazimishwa Boko awe anacheza dakika nyingi uwanjani wakati umri umeenda matokeo yake Boko sasa ameanza kupotea mazima. Kwa viongozi wa Simba inatakiwa watafute mbadala wa Chama haraka kwani wamechelewa ilitakiwa ameshaptikana toka msimu ulioisha.
Nakubaliana na wewe ingawa inatakiwa Chama aanze kipindi cha kwanza, yakishapatikana magoli ndio atolewe maana kipindi cha pili Simba huwa wanachoka sana.
 
Chama ana misimu zaidi ya 4 simba, kwa brain kubwa ya chama Simba ndio ilipata njia ya kuanza kucheza hizi hatua za makundi na robo fainal... Ili Simba icheze vizuri inahitaji chama awe na watu wenye akili kubwa ya mpira Kama yake yenye utulivu na kucheza kitimu!.
Nakupa misimu 3 ya chama akiwa amezungukwa na wachezaji wenye big brain Kama yake, Simba ilifanya vizuri na ilikuwa ya Moto chama akiwa amezungukwa na KAHATA, LALY BWALYA, LUIS MIQUISONE (3 LEFT FOOTETRs) wakati huo DM akiwa mkude/Fraga/Thadeo. Wakati huo juu kulikuwa na finisher Adebayor wa bongo JOHN BOCCO. Simba ilishinda mechi mbele ya timu yoyote....

Simba ya saizi anagalia wachezaji wanaomzunguka chama Kama wanaendana nae... Kibu D miguvu akili kidogo, kanoute/mzamilu nguvu nyingi akili kidogo, Saido anacheza as individual sio Kama timu,onana mpira wa umiseta ...... Chama bado ni mchezaji mzuri sanaaaa kwa Simba hii na yanga anaingia kikosi chochote.
Kwani hachoki au hazeeki.

Basi kina Ronaldinho wangeendelea kucheza mpk leo mkuu
 
Back
Top Bottom