Chama kina nguvu kuliko Serikali, hizo ndizo siasa za nchi yetu na za kikomunisti

Chama kina nguvu kuliko Serikali, hizo ndizo siasa za nchi yetu na za kikomunisti

Hapana, haipaswi kuwa hivyo. Serikali inapaswa kuwahudumia wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa. Watumishi wa umma wanapaswa kutojihusisha na shughuli za kisiasa japo kila mmoja anaweza kuwa na mapenzi na chama fulani nk.

Hii inayofanywa na CCM hasa tangu kipindi cha Mwendazake ni uwendawazimu na ulimbukeni wa madaraka. Mf. Kumteua DED toka kwenye majukwaa ya kiasa, unadhani atatoa huduma sawa kwa wale wasio na mapenzi na chama chake? Ilifika wakati JPM anawahaidi rushwa ya vyeo kwenye campaign wale wote aliowaengua kwenye kura za maoni.

Yanayofanywa na Makonda ni muendelezo wa drama za enzi ya Magufuli. Hana uwezo wa kumwajibisha waziri au mtumishi yoyote wa umma. Kwa nchi ya mfumo wa vyama vingi hakuna chama kushika hatamu.
Magufuli kafa ila bado Samia ana endeleza ule ule utamaduni wa chama kuiweka serikali chini yake.

Wewe una tatizo na Magufuli
 
Watu mnajitoa ufahamu humujui kuwa nguvu ya chama inaanzia Kwa wananchi baada ya kukichagua ndipo chama kinakaa chini kuunda serikali hivyo hakuna Rais,waziri,Rc,DC na wengine mwenye ubavu wa kukikoromea Chama ndoo maana Rais Kwa madaraka yke moja Kwa moja anakuwa mwenyekiti wa chama ili kulinda madaraka yke mbele ya chama waziri ni kama mm tu ninaeandika hpa mbele ya chama.
 
Chama ndiyo, intelegency drives, serekali ni watekelezaji tu wa mipango ilivyopangwa na chama, chama ndicho chenye makubaliano na wananchi.
Na msemaji na jicho la utetezi la ulinzi wa makubaliano yaliyopo ndiye MAKONDA.
 
Kwa wale wote wanao shangaa maigizo ya makonda kukaripia viongozi wa kiserikali wanapaswa kufuatilia na kujifunza asili ya siasa zetu.

Baada ya ziara ya Mwalimu Nyerere uchina na Tanzania kupitia mabadiliko makubwa ya kisiasa na kuanza kufuata siasa za kijamaa.

Katika mabadiliko hayo nguvu ya kiserikali na mambo yote nchini yalikuwa chini ya chama.

Nguvu ya viongozi wa kiserikali inategemeana na nguvu waliyo nayo ndani ya chama na wala sio serikalini.

Mfano nchi ya kikomunisti Vietnam Rais wake Von Van Thuong hana nguvu yoyote ya kimaamuzi mbele ya katibu mkuu wa chama cha kikomunisti cha kivietnam bwana Nguyen Phu Trong.

Chama cha kikomunisti cha Vietnam power structure yao inaanzia kwa Katibu mkuu wa chama hawana cheo cha mwenyekiti wa chama kama hapa Tanzania.

Turudi Tanzania nguvu kubwa ya Samia Rais wa Tz ipo kwenye cheo chake cha mwenyekiti wa chama na wala sio cha urais.

CCM walipitia mabadiliko na kuamua mtu akiwa Rais basi moja kwa moja lazima awe mwenyekiti wa chama ili kuondoa migongano baina ya mwenyekiti wa chama na Rais.

China nao walipitia mabadiliko ya namna hiyo baada ya position ya katibu mkuu wa chama kutokuwa na ukomo wa muda ili walazimu na position ya Urais kuondolewa ukomo wa muda ili yasije kutokea ya migongano baina ya katibu mkuu wa chama na Rais.

Madaraka ndani ya utawala wa Tanzania yana anzia ndani ya chama kabla ya serikali.
Waendelee kushangaa
 
Watu mnajitoa ufahamu humujui kuwa nguvu ya chama inaanzia Kwa wananchi baada ya kukichagua ndipo chama kinakaa chini kuunda serikali hivyo hakuna Rais,waziri,Rc,DC na wengine mwenye ubavu wa kukikoromea Chama ndoo maana Rais Kwa madaraka yke moja Kwa moja anakuwa mwenyekiti wa chama ili kulinda madaraka yke mbele ya chama waziri ni kama mm tu ninaeandika hpa mbele ya chama.
Wananchi awachagui chama wagombea wa nafasi za uwakilishi na raisi ndio wana vyama.

Serikali ina mihimili mitatu; central (core) government, bunge na mahakama.

Central government ndio ina mamlaka ya kuongoza nchi, na maana halisi ya central government ni raisi na baraza la mawaziri.

Raisi anateua baadhi ya wabunge kuwa mawaziri (wabunge wa chama chake) kuunda serikali; ndio msingi wa neno serikali ya CCM.

Serikali (core) ina Mandate ya kuongoza nchi, wanakuja na dira yao (ilani yao ya uchaguzi).

Kutekeleza ilani yao inabidi watumie civil servant ku-implement (hawa ni non-partisan wanatakiwa kuwa tayari kutekeleza ilani ya chama chochote kitakachoshinda uchaguzi).

CCM imevunja huo utaratibu hasa kipindi cha Magufuli imefanya nafasi za civil servants hasa TAMISEMI ni za makada. Ndio maana hata viongozi wa kichama wanadhani wana mamlaka ya kuwaamuru.

Watu wenye uwezo wa kuamrisha watumishi wa umma ni viongozi walio kwenye core government tu. Mawaziri, raisi na makamu wake.

Kinana, Nchimbi na Makonda wanaweza pangiana na mawaziri wa serikali huko ndani ya vikao vyao vya CCM, lakini awawezi waamrisha publicly hawana hayo mamlaka.

Hao civil servants ndio kabisa hawana mamlaka nao, hata kama wanatekeleza ilani ya CCM. Civil servants wanawajibika kwa viongozi walio serikalini kuu tu (raisi na baraza lake la mawaziri), as well as hierarchical yao ya utumishi.

This is A level politics
 
Tofautisheni ulimbukeni na ucommunist. Enzi ya Nyerere tulikuwa na chama kimmoja cha siasa ambacho kwa kuiga siasa za kidictetor ilidaiwa kimeshika hatamu. It was okay kwa kiasi fulani kwa kipindi hicho. Kwa sasa nchi ni ya vyama vingi vya siasa. Ni ulimbukeni tu ulioasisiwa na kukomazwa na mwendazake serikali kuwa chini ya chama. Wenye akili wanaelewa tulipo na tunakoelekea, kuna siku nguvu ya umma itakataa upuuzi unaofanywa na viongozi wa CCM.

Umenena vyema sana, bila nguvu ya umma ama mapinduzi ya kijeshi, tutabaki kulazimishwa huu uhuni wa ccm usiopo ndani ya katiba. Viongozi wa ccm wanaweza kuihoji serekali kwenye vikao vya ndani na bungeni, sio huo uhuni wa viongozi wa ccm kuzurura nchini kufanya maigizo ya kufokea watumishi wa umma.
 
Magufuli kafa ila bado Samia ana endeleza ule ule utamaduni wa chama kuiweka serikali chini yake.

Wewe una tatizo na Magufuli
Sina tatizo na Magufuli, hisipokuwa nina tatizo nae kwa jinsi alivyoiendesha serikali bila kufuata sheria za nchi, kanuni na taratibu. Kila mmoja anahoji madaraka ya Makonda kwasababu anajaribu kuirudisha nchi kwenye utaratibu wa Magufuli. Na ndiyo maana mnashidwa kutofautisha enzi za chama kushika hatamu, ucommunist na demokrasia ya kiliberary.
 
Wananchi awachagui chama wagombea wa nafasi za uwakilishi na raisi ndio wana vyama.

Serikali ina mihimili mitatu; central (core) government, bunge na mahakama.

Central government ndio ina mamlaka ya kuongoza nchi, na maana halisi ya central government ni raisi na baraza la mawaziri.

Raisi anateua baadhi ya wabunge kuwa mawaziri (wabunge wa chama chake) kuunda serikali; ndio msingi wa neno serikali ya CCM.

Serikali ina (core) ina Mandate ya kuongoza nchi, wanakuja na dira yao (ilani yao ya uchaguzi).

Kutekeleza ilani yao inabidi watumie civil servant ku-implement (hawa ni partisan wanatakiwa kuwa tayari kutekeleza ilani ya chama chochote kitakachoshinda).

CCM imevunja huo utaratibu hasa kipindi cha Magufuli imefanya nafasi za civil servants hasa TAMISEMI ni za makada. Ndio maana hata viongozi wa kichama wanadhani wana mamlaka ya kuwaamuru.

Watu wenye uwezo wa kuamrisha watumishi wa umma ni viongozi walio kwenye core government tu. Mawaziri, raisi na makamu wake.

Kinana, Nchimbi na Makonda wanaweza pangiana na mawaziri wa serikali huko ndani ya vikao vyao vya CCM, lakini awawezi waamrisha publicly hawana hayo mamlaka.

Hao civil servants ndio kabisa hawana mamlaka nao, hata kama wanatekeleza ilani ya CCM. Civil servants wanawajibika kwa viongozi walio serikali kuu tu (raisi na baraza lake la mawaziri
Ndoo maana hakuna mgombea binafsi unagombea kupitia chama uwe Rais,uwe Mbunge,Diwani na hta mwenyekiti wa mtaa Sasa chama ndicho kinakupa nafasi ya kugombea ili uende kutekeleza Yale ambayo wao kama chama wanataka ukayasimamie na ukipata nafasi hiyo watakufuatilia Kwa ukaribu kujua unafanya Yale ambayo wao walikutuma ujue hta Rais anafuatiliwa Kwa ukaribu na chama kama anatekeleza matakwa ya chama.
 
Hilo halina ubishi lakini hayo ni maswala ya kichama sio ya kiserikali, wanatakiwa wafanyiane tathmini katika vikao vyao vya ndani.

Vinginevyo serikalini kuna hierarchy yao raisi, makamu, waziri mkuu, naibu wake kwa sasa na mawaziri. Kwa hivyo kwa taratibu za serikali Bashe yupo sahihi.

Japo sijasikiliza yote aliyosema Bashe ila ukisikiliza clip ndogo inayosambaa sidhani kama alikuwa anamuongelea Makonda, kuna mention ya watu wanaojaribu kufanya lobbying aondoe price ceiling ya bei ya sukari aliyoweka clearly huyo mtu au hilo kundi sidhani kama Makonda yupo.

Huko serikalini wote wanajua Makonda hana hayo mamlaka anachofanya ni ‘charm offensive’ ya kujaribu ku-boost falling popularity ya raisi; so they’re are just playing their part along the way.

Mtu ajichanganye sasa na kumchukulia Makonda poa hadharani, maana hiyo ni mission ya raisi na mwenyekiti wao huko CCM. Asije shangaa kitumbua kinaingia mchanga.
 
Umenena vyema sana, bila nguvu ya umma ama mapinduzi ya kijeshi, tutabaki kulazimishwa huu uhuni wa ccm usiopo ndani ya katiba. Viongozi wa ccm wanaweza kuihoji serekali kwenye vikao vya ndani na bungeni, sio huo uhuni wa viongozi wa ccm kuzurura nchini kufanya maigizo ya kufokea watumishi wa umma.
You're very right, CCM inafanya uhuni kwa sababu ya ujinga wa wanaojiita machawa na ukimya wa wananchi. Lakini wanachokipandikiza kuna siku kitakuwa kisu cha kuwachinja. CCM inawaona wananchi wajinga na inawachezea kama wanavyotaka, mbaya zaidi inajaribu kuliingiza jeshi kwenye mambo ya siasa. Na upuuzi huu ulikolezwa na Magufuli na huyu wa sasa anafanya mwendelezo. Kidogo Samia alianza vizuri lakini sasa hivi kanogewa na ameanza kuwakumbatia akina Makonda, watampoteza.
 
Back
Top Bottom