Chama kina nguvu kuliko Serikali, hizo ndizo siasa za nchi yetu na za kikomunisti

Magufuli kafa ila bado Samia ana endeleza ule ule utamaduni wa chama kuiweka serikali chini yake.

Wewe una tatizo na Magufuli
 
Watu mnajitoa ufahamu humujui kuwa nguvu ya chama inaanzia Kwa wananchi baada ya kukichagua ndipo chama kinakaa chini kuunda serikali hivyo hakuna Rais,waziri,Rc,DC na wengine mwenye ubavu wa kukikoromea Chama ndoo maana Rais Kwa madaraka yke moja Kwa moja anakuwa mwenyekiti wa chama ili kulinda madaraka yke mbele ya chama waziri ni kama mm tu ninaeandika hpa mbele ya chama.
 
Chama ndiyo, intelegency drives, serekali ni watekelezaji tu wa mipango ilivyopangwa na chama, chama ndicho chenye makubaliano na wananchi.
Na msemaji na jicho la utetezi la ulinzi wa makubaliano yaliyopo ndiye MAKONDA.
 
Waendelee kushangaa
 
Wananchi awachagui chama wagombea wa nafasi za uwakilishi na raisi ndio wana vyama.

Serikali ina mihimili mitatu; central (core) government, bunge na mahakama.

Central government ndio ina mamlaka ya kuongoza nchi, na maana halisi ya central government ni raisi na baraza la mawaziri.

Raisi anateua baadhi ya wabunge kuwa mawaziri (wabunge wa chama chake) kuunda serikali; ndio msingi wa neno serikali ya CCM.

Serikali (core) ina Mandate ya kuongoza nchi, wanakuja na dira yao (ilani yao ya uchaguzi).

Kutekeleza ilani yao inabidi watumie civil servant ku-implement (hawa ni non-partisan wanatakiwa kuwa tayari kutekeleza ilani ya chama chochote kitakachoshinda uchaguzi).

CCM imevunja huo utaratibu hasa kipindi cha Magufuli imefanya nafasi za civil servants hasa TAMISEMI ni za makada. Ndio maana hata viongozi wa kichama wanadhani wana mamlaka ya kuwaamuru.

Watu wenye uwezo wa kuamrisha watumishi wa umma ni viongozi walio kwenye core government tu. Mawaziri, raisi na makamu wake.

Kinana, Nchimbi na Makonda wanaweza pangiana na mawaziri wa serikali huko ndani ya vikao vyao vya CCM, lakini awawezi waamrisha publicly hawana hayo mamlaka.

Hao civil servants ndio kabisa hawana mamlaka nao, hata kama wanatekeleza ilani ya CCM. Civil servants wanawajibika kwa viongozi walio serikalini kuu tu (raisi na baraza lake la mawaziri), as well as hierarchical yao ya utumishi.

This is A level politics
 

Umenena vyema sana, bila nguvu ya umma ama mapinduzi ya kijeshi, tutabaki kulazimishwa huu uhuni wa ccm usiopo ndani ya katiba. Viongozi wa ccm wanaweza kuihoji serekali kwenye vikao vya ndani na bungeni, sio huo uhuni wa viongozi wa ccm kuzurura nchini kufanya maigizo ya kufokea watumishi wa umma.
 
Magufuli kafa ila bado Samia ana endeleza ule ule utamaduni wa chama kuiweka serikali chini yake.

Wewe una tatizo na Magufuli
Sina tatizo na Magufuli, hisipokuwa nina tatizo nae kwa jinsi alivyoiendesha serikali bila kufuata sheria za nchi, kanuni na taratibu. Kila mmoja anahoji madaraka ya Makonda kwasababu anajaribu kuirudisha nchi kwenye utaratibu wa Magufuli. Na ndiyo maana mnashidwa kutofautisha enzi za chama kushika hatamu, ucommunist na demokrasia ya kiliberary.
 
Ndoo maana hakuna mgombea binafsi unagombea kupitia chama uwe Rais,uwe Mbunge,Diwani na hta mwenyekiti wa mtaa Sasa chama ndicho kinakupa nafasi ya kugombea ili uende kutekeleza Yale ambayo wao kama chama wanataka ukayasimamie na ukipata nafasi hiyo watakufuatilia Kwa ukaribu kujua unafanya Yale ambayo wao walikutuma ujue hta Rais anafuatiliwa Kwa ukaribu na chama kama anatekeleza matakwa ya chama.
 
Hilo halina ubishi lakini hayo ni maswala ya kichama sio ya kiserikali, wanatakiwa wafanyiane tathmini katika vikao vyao vya ndani.

Vinginevyo serikalini kuna hierarchy yao raisi, makamu, waziri mkuu, naibu wake kwa sasa na mawaziri. Kwa hivyo kwa taratibu za serikali Bashe yupo sahihi.

Japo sijasikiliza yote aliyosema Bashe ila ukisikiliza clip ndogo inayosambaa sidhani kama alikuwa anamuongelea Makonda, kuna mention ya watu wanaojaribu kufanya lobbying aondoe price ceiling ya bei ya sukari aliyoweka clearly huyo mtu au hilo kundi sidhani kama Makonda yupo.

Huko serikalini wote wanajua Makonda hana hayo mamlaka anachofanya ni ‘charm offensive’ ya kujaribu ku-boost falling popularity ya raisi; so they’re are just playing their part along the way.

Mtu ajichanganye sasa na kumchukulia Makonda poa hadharani, maana hiyo ni mission ya raisi na mwenyekiti wao huko CCM. Asije shangaa kitumbua kinaingia mchanga.
 
You're very right, CCM inafanya uhuni kwa sababu ya ujinga wa wanaojiita machawa na ukimya wa wananchi. Lakini wanachokipandikiza kuna siku kitakuwa kisu cha kuwachinja. CCM inawaona wananchi wajinga na inawachezea kama wanavyotaka, mbaya zaidi inajaribu kuliingiza jeshi kwenye mambo ya siasa. Na upuuzi huu ulikolezwa na Magufuli na huyu wa sasa anafanya mwendelezo. Kidogo Samia alianza vizuri lakini sasa hivi kanogewa na ameanza kuwakumbatia akina Makonda, watampoteza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…