Moja kwa moja kwenye mada
Kila mtanzania anajuafiki kua amani yetu ni tunu kubwa na muhimu katika kuleta ustawi wa jamii. Inapotokea kua kuna kundi au chama cha siasa kinajaribu kushirikiana na kushinikiza nchi marafiki kuona Tanzania aifai basi kundi ilo au chama hicho inabidi kipigwe marufuku nchini. Tunakumbuka wakati wa JPM wenzangu waliwai kuomba ata na kupanga safari kwenda nchi mbali mbali huku Ulaya wakiziomba nchi hizo kuinyima Tanzania misaada na ushirikiano.
Leo tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi ni kundi ilo ilo linashauri nchi hizo hizo zisitishe urafiki kwa Tanzania.Zisitishe misaada na mambo mengine kwa Tanzania kisa kundi ilo linataka mabadiliko flani kwenye mchakato wa uchaguzi.
Kundi au chama hicho kiliamua chenyewe kutoshiriki uchaguzi ata kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.... Nchi Misri kilikuwepo chama kinaitwa Muslim Brotherhood, kundi au chama hiki kilikua kimeifanya Misri kama uwanja wa vita asa dhidi ya madhehebu ya kidini. Rais ALISSIS alipoingia madarakani alifanya uamuzi wa kukifuta na leo Misri imetulia tuli.
Kuna umuhimu mkubwa wa kuifuta CHADEMA ya sasa maana inakihuka kwa kiasi kikubwa maadili ya Taifa letu...