Tetesi: Chama kisha pokea milion 100 za awali katika ahadi ya Ikulu

Tetesi: Chama kisha pokea milion 100 za awali katika ahadi ya Ikulu

Wakuu naendelea kuwaletea Data za nini kilichojiri pale Ikulu siku mkuu kakutana na NCCR, ACT na CUF.

Mtu wangu wa karibu sana ambaye ni kuiongozi wa juu wa moja ya Chama kilichoitwa Ikulu kanitonya tena kwamba kwa Chama chao wameahidiwa 1.3 Billioni za kampeni ambazo zitatumika kusimika wagombea nchi nzima.

Kaniambia kwa mujibu wa bosi wake hawajaahidiwa majimbo ya bure ila watapewa pesa za kusimika wagombea nchi nzima kuanzia ngazi ya Urais hadi Udiwani.

Na wao tayari wameishapewa Milion 100 za kujenga Chama na nyingine watapewa kadri siku zinavyoenda mbele.

Pia hajui vyama vingine viwili vimeahidiwa sh ngapi kila kimoja maana waliitwa kila mmoja kivyake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu yoyote akikosoa chadema amenunuliwa?

Dk Slaa aliwakosoa chadema akawahoji hao mnaopokea ni asset au liability? Akaambiwa ni Dk mihogo amenunuliwa na ccm lakini leo Mbowe na wazee wa chadema wanajuta hadharani kupokea pokea wanachama hovyo.
Chadema badala ya kujibu hoja za Mbatia wanajificha kwenye kichaka cha amenunuliwa na ccm!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unjustifiable writing - ndani kule hakukuwa na officials zaidi ya Usalama (walinzi wa rais) - kupiga ramuli hakukusaidii badala yake jikiteni kwenye kuimarisha umoja wenu

Unachofanya ni kufitinisha wapinzani wenzako kitu ambacho hakikuongezei huruma
Kwani usalama hawana marafiki? Na ,je wewe umejuaje ilo?
 
mkuu thread zako zote ni tetesi, unajisikiaje lakini?
 
Kama kuna UKAWA, je hakuwezi kuwapo kuungana kwa mpinzani na aliyepo madarakani?
 
Hapo hakuna shida kam pesa inaenda kukuza chama ili kiwe shindani, pia hiyo pesa itatumika hapa Tanzania na kuongeza mzunguko, wanufaika ni watanzania,
pia mkumbuke zamani kuna chama kilipokea pesa kutoka kwa wafadhili kina sabodo kikaua, ni muda sasa na NCCR nayo ikuwe, kinachotakiwa ni baada ya matokeo kama ilitumika vizuri na sio mifukoni kwa watu, kwa hiyo swala la kugawa kula ni hisani ya wananchi na siyo mawazo ya mtu mmoja.
Mnachezea pesa ya walipa kodi halafu unasema hakuna shida!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM ndio chama pekee chenye Nia ya dhati ya kujenga demokrasia nchi na CCM kutumia mapato yake kutoka na vitega uchumi vyake ili kujenga demokrasia si jambo gumu.

Wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa nilisema kuwa wapinzani walisusa kutokana na ukata na si kingine mkabisha leo Mbatia kathibitisha kikwazo Cha wapinzani kutofanya michakato ya kidemokrasia ni ukata.

Msione aibu kuomba msaada wa kifedha CCM ili kujenga vyama vyenu, CCM haina tatizo Kama pesa inazotoa zitajenga demokrasia ya kweli.

Rais Magufuli hawezi kutumia pesa za walipa Kodi kufanya kitu hicho.
Huu upimbi uwe unawasimulia wakwenu huko kijijini wakati ukigongea ugimbi! Nonsense!
 
1583501809408.png
 
Back
Top Bottom