Chama tawala chini ya Masisi chapoteza madaraka katika uchaguzi Botswana baada ya miaka 58

Toka maktaba : CCM mlimpeleka ujumbe mzito kujifunza

Oktoba 2024.​


Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Botswana umezinduliwa rasmi leo tarehe 22 Oktoba 2024 na Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini humo. HoM) kwa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC (SEOM) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Botswana. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Avani mjini Gaborone, Botswana.

Jamhuri ya Botswana imeratibiwa kufanya uchaguzi tarehe 30 Oktoba 2024.


Mheshimiwa Elias Mpedi Magosi, Katibu Mtendaji wa SADC aliambatana na Mkuu wa Mabalozi na kuhudhuria kikao hicho. Hafla hiyo pia iliheshimiwa kwa uwepo wa wadau mbalimbali wakiwemo; wakuu wa ujumbe wa kidiplomasia , maafisa wa serikali, wajumbe wa SADC Organ Troika kuhusu siasa, ulinzi na usalama ushirikiano , Baraza la Ushauri la Uchaguzi la SADC, Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana, vyama vya siasa, makundi ya kidini, Asasi za Kiraia , wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa. ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi, waangalizi wa uchaguzi wa SADC na vyombo vya habari .


Uchaguzi Mkuu ujao nchini Botswana utakuwa na jukumu muhimu katika kuchagua Bunge la 13 la nchi hiyo na mabaraza ya mitaa kote nchini. Jumla ya viti 61 katika Bunge la Kitaifa na viti 609 vya udiwani vitashindaniwa, vyote vitaamuliwa kupitia mfumo wa upigaji kura wa baada ya mwisho.

Taarifa ya uzinduzi imeambatanishwa
 
Upinzaji umeshafanya kazi kubwa ni swala tu la watu watanzania wengi kupenda kufatilia mambo yasiyo na tija
Hilo ndio tatizo la wengi
Watu wanakubali kuwekewa soko upande mmoja halafu hapo hapo kuna Dampo la taka na wanacheka tu
Hii nimeiona leo humu
Lingine vijana kila leo wanasema maisha magumu ilahali wanapoteza mda kwenye betting na mipira
Inasikitisha sana
 
Demokrasia imeng'ara ...
 
Hawa wakoloni wetu weusi wameapa hawatoachia madaraka hata wakishindwa kwenye sanduku la kura hii maana yake hawatokubali kuachia madaraka kwa njia ya amani! Hawa watu ni hatari sana na tena tunajuta kuwafahamu.
 
Bongo bado tunaile hali ya uwoga na ubinafsi, tukipona eneo hilo wizi wa kura na udikteta utaisha.
 
FRELIMO nayo ilitakiwa ifurushwe ili bongo nayo ione kumbe inawezekana kuipumzisha ccm iliyotawala muda mrefu nayo ikatolewa kwa heshima kutumia sanduku la kura. BDP imeonesha njia, ikajipange huenda ikarudi tena uchaguzi ujao
BDP irudi kufanya nini? Ndio imetoka hivyo. Hakuna kurudi tena. Ndio maana vyama vingi vilivyoleta uhuru vimebaki kusaidiwa na state machinery as vinajua vikitoka vimetoka
 
Ata hao wanaopata mabadiliko kuna ambao walikua na akili zakijinga kama zako.muda wa mabadiliko ukifika umefika.Huna uwezo wakuzuia ata kama utakua na chuki kiasi gani.
Wakati wa kupanda,wakati wa kuvuna,wakati baridi,wakati wa Jua,wakati kulia wakati wa kucheka,kila jambo kwa wakati Wake hata wasiotaka mabadiliko,Mabadiliko yatawalazimisha kubadilika!
 

Uchaguzi wa Botswana | 'Ushahidi ni mwingi, chama chetu dola kongwe bila kupepesa macho tumepoteza uchaguzi huu kwa kishindo ': Masisi



View: https://m.youtube.com/watch?v=og9-zzjIwuUChama dola kongwe kilichodumu madarakani kwa miongo 6 tangu uhuru BDP cha Rais Mokgweetsi Masisi cha Botswana Democratic Party kimepoteza mamlaka yake. Matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutiririka kufikia sasa yanaonyesha kuwa vyama vya upinzani vilishinda angalau viti 35 kati ya 61 bungeni.... Na bado hata yale ambayo yanaendelea kujumuishwa hali ni mbaya, tumeshindwa uchaguzi ...
 
Mifumo ya uwadilifu na uwajibikaji ni muhimu katika kuelekea democrasia ya kweli ndani ya taifa letu pendwa la Tanzania.

Ufisadi, Rushwa

Uchawa ndani ya taifa letu, HAWA ni madui wakubwa sana kwa ajili ya masilai mapana ya taifa letu.
By mwinjilist wenu Gabeji.
 
Botswana ikajifunze Zambia na kenya, pamoja na kubadili serkali maisha yao ni yale yale

USSR
 
Wajifunze nini? Wakati lengo la chama cha siasa ni kushika dola?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…