CHAN2021: Mchezo umemalizika kwa Taifa Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia

Mizigo wapitishe kwenye bandari yetu na kutufunga watufunge!?
Ivi yule Nyau anapatikana wapi tumkodi timu ya Taifa?
Nyau kama Nyau.
 
Simba na yanga wanatukwamisha au mnasemaje wadau
 
Kocha hana uzoefu,wachezaji hawana uzoefu......kwa mechi ya leo tungekuwa na key players wa Tz,inawezekana tungeweza kufungwa ila siyo kijinga hivi hivi.

Timu yangu ambayo ingeleta ushindani leo

Kaseja/Manula Golini yeyote

Kapombe

Yassin

Nondo

Nyoni

Mkude(dunia nzima watukutu wapo)

Kaseke

Sure boy/Fei toto

Nchimbi

Mzamiru

Farid

Sub.Nado,Manyama,Lusajo,Kaseja,Muhilu,Tshabalala,Yondani (pressure ikizidi anaingia),Mudathiri,Boko,Nyoso,Dilunga

Hiyo timu angalau tungeleta upinzani

Tz wachezaji wa Simba,Azam na Yanga wanacheza mechi nyingi kuliko wachezaji wote WaTz,hawaepukiki
 
Tanzania katika ubora wake
 
Tunarudi home maana hawa Guinea tayari Wanaongoza 1,na kwa ukimeo wa timu yetu sidhani kama tunaweza kupata hata sare..........labda kocha abadirike
 
Wakati mwingine tunatafuta mchawi bila sababu za msingi.

Kocha wa Mbao FC kufika fainali ya Azam Fed Cup ndiyo sifa ya kuwa kocha wa National team? Hatupo serious.

Zigo la TFF hili.
 
Sisi tulikuwa busy na nyange hii game wametustukiza tu[emoji23][emoji23]
 
Man of the match ni Collins kombe, nadhani Sasa Simba na yanga wataanza kumsaka Kama kawaida yao.
Ile game ya Taifa Stars na Burundi ambapo yule Mzee Ntibazonkiza kutufunga wale Jamaa wa Jangwani hawakumuacha, na huyu Chabula kufunga bao la pili sidhani kama ataachwa.
 
Mkuu kauli za wanasiasa na masilahi binafsi ya viongozi wa mpira wa miguu hapa nchini ndio sababu kubwa ya hii team kufanya vibaya.
Kocha anataka kuwaridhisha wana siasa na baadhi ya watu kwa maslahi ya wachezaji wao kwa kutumia kivuli cha kukuza vipaji vipya.

Ukweli ni kwamba sisi Chan mwaka huu hatujapeleka team ya ushindani bali tumepeleka team ya majaribio kwenda kukuza vipaji na matokeo yake ndio haya tunayaona sasa na nakubaliana na wewe kuwa hatutapata hata pont 1 kwenye haya mashindano kamwe.

Huwezi kuacha wacheji wazoefu wote nyumbani na hata hao wachache ulio wachukua bado unawaweka bench kwa makusudi kabisa mfano mabao yote mawili makosa yalianzia katikati pale kwa baraka Majogoro Kisha cross ikapigwa pembeni kushoto kule kwa Manyama inakuja kwenye box Kapombe anajitahidi kuokoa hadi ananawa mpira, Goli la pili napo vile vile ni kule kule kushoto mtu kapiga cross jamaa anaunganisha mpira kambani.

Katikati pamekufa kabisaa ajabu Ndemla yuko bench pale hapewi nafasi, viungo wa Kati wazuri kabisa Kama Mzamiru, Sure boy, Frank Domayo na Mkude wameachwa kwa makusudi kabisa.

Kule mbele ndio kabisaa, yani unamuweka bench Faridi Musa alafu unamuanzisha Mhiru ambae hata ball control nzuri hana, Kama haitoshi tumewaacha mawinga wazuri kabisa huku Nyumbani Kama Iddi Nado na Hassani Dillunga kisa tunataka kukuza vipaji!!!

Nchimbi unamuweka mbele na Lyanga heti ndio wawe wafungaji huku huyu nchimbi hata tu kwenye team yaka hapati nafasi ya kucheza anakaa bench tangu msimu wa ligi imeanza hajafunga goli hata moja alafu eti ndio tunategemea akatupe matokeo CHAN.

Wacha tu tufungwe sababu tupo kwenye majaribio ya kikosi na si kushindana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…