Jana niliandika Uzi kumhusu rayvanny, kuanzia support aliyopata Kwa Diamond , behind the scenes ya hyo backup , na nikaunganisha pia Kwa harmonize jinsi ambavyo wote Kwa pamoja mond aliwabeba na kuwatambulisha vyema ...!!
Harmonize akaona isiwe tabu ikabd ajikate, njia aliyopitia sio rahsi hata kidogo , ni njia ngumu yenye giza nene , hata kusikika kwake sasa angalau kuelea kwenye peak amefika Kwa gharama kuu .... Uzuri wa harmonize ni mtu wa Wana sana , Yani msela fulan hv ambaye watu wa vijiwe na kitaa wanamuelewa , ana swaga hata Kwa presenters na Kiki za hapa na pale , kiukweli imemsaidia kutrend
Nikarudi Kwa Rayvanny kijana wa Mbeya Kwa walima viazi , wapo wanaomsifu kuwa ni kijana wa heshima mara ooh mstaarabu , ukweli ni kuwa Rayvanny ana majivuno , dharau na kujiona kwingi , sio mtu wa Wana na masela , ameegemea Sana Kwa jinsia ya kike, na Kwa vile b4 alikuwa na strong backup ya Mond hii ilimbeba Sana , yaani diamond akifanya sarakasi zake za Kiki , na uhuni wake , automatically alikuwa anambeba pia dogo kutrend....
Sasa amejiachia , ni kweli ni Jambo sahihi Ila Kwa namna alivyo naona kama ni wrong move...!! Hana ngozi ngumu ya kupitia mashutumu , Kiki , kutoa mawe ya kubang , kuroga Sana na uhuni mwingi , yupo yupo tuuu , na Kwa sasa hajui hata afanye nini , kufanya kolabo na wasanii wasioeleweka , kutoa nyimbo boko , pelepele washa ndo nini sasa , matokeo yake wimbo haujaenda mjini , media karbia zote ni kama zimemsusia , rayvann anapost Instagram Kwa masaa matano replies ni 40+ hii haijawahi tokea , dogo ni mlaini Sana
Ukweli dogo yupo kwenye alarming rate , hajachelewa kuzinduka na kuona something is wrong , unatafuta machawa akina Mr Pimbi daah.... Hyo next level hata haieleweki , macvoive naye yupo yupo tuuu .....
Naamini bado ana nafasi ya kujipanga kabla hajatumbukia shimoni , Kwa jinsi mziki wetu ulivyo ni impossible kuwa katikati alaf ufikr utatoboa , lazima uchague upande , vinginevyo akubali kuwa average.... Na asipoangalia hyo lebel yake itakuwa kijiwe cha kupigia soga na slay qeen akina Paula
ni ushauri tuu , lakini akiwastua nyie moderator akawaomba muufute , bas ufuteni tena na huu