Changamoto gani ulipitia ukaitatua, ukaamini nikweli kwamba nyakati ngumu hazidumu

Changamoto gani ulipitia ukaitatua, ukaamini nikweli kwamba nyakati ngumu hazidumu

Mimi ni kati ya watu waliopitia changamoto kubwa....from Hero to Negative infinity,kasoro tuu sikufa...ila

Muda wote nilikua namuomba Mungu...tafuta nyuzi zangu humu utazikuta,siongelei imani yako utafanyaje...lakini mimi kama mkatoliki


Nilifanya bidii ya kuhudhuria misa...kusali rosary,kufunga,kusoma maandiko matakatifu na kuwa na mwenendo mwema,lakini kusaidia watu hata katika hali yangu ya kusaidiwa

Kuna muda niliacha kusali nikasema hivi Mungu anasikia?thanks kwa mama yangu alinitia moyo nkaendelea....


Mungu sio mzee Mkumbo...leo niko na maisha mazuri na familia...nkiongelea maisha mazuri siongelei kuendesha benzi au BMW...No! Silitaki...ila familia yangu tunapata mahitaji ya msingi na tuko wenye furaha ya kweli tukiifurahia zawadi ya uhai wa muumba


Mytake...Acha kuwaza kama utatatua kila kitu mwenyewe...ni Congo,yaache yote mikononi mwa Mungu

Epuka huduma za maombezi na manabii,lakini pia ushirikina

Ntakuombea Mungu ayaone unayopitia,akupe moyo mkuu,akuoneshe njia,ukawe mwenye kumpenda katika yote
Amiin
 
Mkuu nlikuwa na madeni, nikapoteza marafk ambao nlikuwa nakunywa nao bia na kuwagawia pesa kipindi nna pesa. Nikauza gari, ikafika nikauza hadi kila ktu ndan nikabak na kitanda na sofa tu. Kodi ikanishinda nikabeba vitu nikapeleka kwa rafiki yangu akanipa chumba kwake. Nikageuka hadi kuwa kama houseboy kwake kwa miez 9.
Nikaona hapa nikiendelea kukaa sitoboi nikaondoka.
Nikaenda kukaa chumba kimoja kodi 30000, nikaanza upya kufanya jambo ambalo nikilisema hapa watu watabisha mpaka kesho na wala wakati naanza ilikuwa njaa tu sikutegemea kama itanlipa. It was just for surviving kqa muda huo ila ikanipa zaidi.
Ndani ya miezi 6 ilipoanza corona maisha yalianza kurudi kwa reli na sasa naweza kusema niko vzuri kuliko awali.
Jambo gani ilo mkuu ebu share nasi
 
madeni ndio yanani sumbua sana.
Kuna familia, koo na makabila fulani ukienda kumposa au kumchumbia binti yao hicho ndio kipengele muhimu cha kukupa binti yao utaulizwa "una madeni au umewahi kukopa?"

Sasa jichanganye useme "sina madeni na sijawahi kukopa", kuna mawili hawakupi binti yao au utapigwa mahari kubwa kuliko ulivyotarajia
 
Back
Top Bottom