Changamoto gani ulipitia ukaitatua, ukaamini nikweli kwamba nyakati ngumu hazidumu

Tunaelekea msimu wa mavuno,
tafadhali sana, nashauri ukiuza mazao yako kadiri ya majaaliwa ya Allah, katika kilimo chako cha msimu ujao, ongeza na ufugaji hususani wa ng'ombe,

nunua ndama wa dogo saizi ya kati hata wa5 tu ambao utawalisha na kuwanenepesha kwa miezi 3-6 ukiwauza unaongeza idadi ya ndama wengine wadogo wa kunenepesha,


na ninakuhakikishia,
ndani ya misimu miwili tu, utajikuta unatamani kufuga kuku, mbuzi, nguruwe, kondoo n.k na halafu maisha yako yatabadilika kabisa,

ni kuthubutu na kufanya maamuzi magumu tu gentleman,
Hongera kwa kazi ya kilimo 🐒
 
ok thank u chief
 
Kuna kitu nilikuwa natafakari Jana! ... Sidhani kama nitakikumbuka chote!

By the way, katika hayo Mapito hupiti wewe tu tupo wengi!

Sijui wewe ni mtu wa Imani Gani! Ila Jana nilikuwa natafakari maisha ya Yusufu yule mtoto wa Yakobo.

Maswali niliyokuwa najiuliza yalitokana na fikra hii ... Yusufu alipata ndoto akiwa na miaka 17 ila Ile ndoto ilikuja kutimia akiwa na miaka 30 ... 30 -17 = 13

So ilimchukua miaka 13 kile alichokiota Yusufu, kutimia! ...

Maswali yangu yalikuwa ni hivi!

Kwanini Mungu, aliruhusu Yusufu apitie magumu kwa miaka yote? Kwanini Dogo asingekaa tu kwako na Dingi, then akiwa na age 27, 28, 29 ndo amchukue kumpeleka Misri ili kutimiza hiyo ndoto!

Ila ni ukweli kuwa! Malengo, ndoto, maono tuliyo nayo Kuna namna ili yaweze kutimia yanatuhitaji tuwe kwenye best version of ourselves ... Hili Sasa ndo Lina demand mtu kupitishwa katika magumu ili aweze kuwa kuchongwa kwa lengo la kufanania Ile ndoto na maono inataka awe!

The best kichongeo Cha kumuandaa mtu awe kwenye the best version ya kuweka kupokea au kupata mafanikio then kuyatunza na kufanya yaongozeke ni magumu ... Tough time ni kichongeo kizuri!

Ubaya ni kuwa hakuna somo katika maisha yetu ya shule tulilofundishwa kuhusu umuhimu wa Nyakati Ngumu katika maisha ya mafanikio na namna ya kuweza kubakabiliana na Nyakati hizo!

Nisikuchoshe ... Kikubwa kuwa mgumu, refuse to give up ... Kwa maombi, mifungo, kuishi matendo mazuri n.k

Nimewahi kujiuliza kuwa! Katika magumu ninayopitia nikikata tamaa, kulalamika it will change my situation?

Mzee tukaze tutavuka hapa!
 
Mrudishie Mungu Kwa kusaidia wenye uhitaji kama huyo jamaa,utabarikiwa zaidi
 
thank mkuu japo bado nina imani ipo siku nitatoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…