Changamoto gani utakutana nazo kwa kuoa au kuishi na Mwanamke mwenye mtoto?

Changamoto gani utakutana nazo kwa kuoa au kuishi na Mwanamke mwenye mtoto?

Sio wanawake wote wenye watoto wamezalishwa wakaacha kilambimkwidu

Wengine wameamua kukaa pembeni baada ya kuona yule aliyeshirikiana nae kupata mtoto sio mume sahihi

Hujawahi kutana na wanawake wanadai talaka na waume zao hawako tayari kwa hilo?

Hujawahi kutana na situation ambayo mahakama inabidi isimame talaka itolewe ili kuokoa maisha ya mwanandoa?

Btw kuvunjika kwa ndoa sio kitu kizuri wala cha kupendeza ila ndoa hatarishi ni hatari zaidi ya talaka

Hayo mengine ya baby baba ni maoni yako wewe binafsi
Wanawake waliotoka kwenye ndoa kwa sababu hii au ile wapo kwenye majuto mazito japo wengi wao kwenye komenti wamenyooka utadhani hawajapigwa kichwani na kitu kizito chenye ncha kali
 
Habari wakuu,
Hapa nakusudia mwanamke mwenye mtoto ambaye si wako, Mtoto ambaye kwa kiasi kikubwa bado anahitaji ukaribu na mama yake.

Nimeshuhudia ndoa ya Jirani yangu ikiyumba baada ya mtoto wa miaka takribani miwili na nusu au mitatu Kuletwa nyumbani na mkewe kwani wamekaa wastani wa miezi 3 bila ya mtoto huyo kuwepo.

Tatizo ninaloliona ni utundu wa huyo mtoto ambao wakati mwingine unasababishwa na kudekezwa na mama yake.

Mfano siku moja aliiburuza chini Iphone ya baba yake mlezi, akafokewa na baba huyo, Jambo hilo lilisababisha mama akasirike kwa madai kuwa baba hampendi mtoto.

Je changamoto gani nyingine za kuoa mwanamke mwenye mtoto mdogo?

Kama waweza epusha kuishi na mtu Mwenye mtoto Ni Jambo gumu Sana, wazazi kuachana kabisa Ni ngumu Sana, labda mjane
 
Wanawake waliotoka kwenye ndoa kwa sababu hii au ile wapo kwenye majuto mazito japo wengi wao kwenye komenti wamenyooka utadhani hawajapigwa kichwani na kitu kizito chenye ncha kali

Kuna walionyooka kwa gunia mbili za mkaa, wapo waliishia kwenye tundu za choo, wapo waliokatwa korodani na wake zao na wengine wengiiii wakihofia huko kunyooka

Haya mambo ni ya kumshirikisha Mungu sana

Ukikosea kumshirikisha wakati wa kuanza basi anza kumshirikisha sasa atafanya wepesi katika yote
 
Teenagers ndiyo wenye kiburi cha kusema sioi/siishi na mwanamke asiye na mtoto, kwakua wana uhakika wa kupata mwanamke chuchu konzi ambaye bado hajazaa.

Wanaume wenye umri kuanzia miaka 35+, ni nadra kupata mwanamke hajazaa, kwakua wanawake saizi yao wanakua wameshazaa.

Hizi kauli za sioi mwanamke aliyezaa, ni za vijana wa umri mdogo, watu wazima oeni tu mwanamke aliyezaa, hakuna namna

Hiyo 'size' yao unaipima kwa kuzingatia vigezo gani?
 
Hiyo 'size' yao unaipima kwa kuzingatia vigezo gani?
Umri.
Asilimia kubwa, mwanaume anaishi/anaoa mwanamke ayeendana naye kiumri. Mwanaume mwenye miaka 35+, mwanamke wa kuendana naye anakua ameshazaa
 
Umri.
Asilimia kubwa, mwanaume anaishi/anaoa mwanamke ayeendana naye kiumri. Mwanaume mwenye miaka 35+, mwanamke wa kuendana naye anakua ameshazaa

Ambaye anapaswa kuwa na umri gani huyo mwanamke?
 
Mwanamme anayefika 35+ hajaoa, chances are ni msomi au mtu fulani siriazi mwenye kujiandaa…. huyu mtu ataoa msomi mwenzie ambao wanatoka Chuo na miaka 25 hadi 28 ya kujipanga kimaisha.

Wanaozalishwa mapema ni wale wanawake wa kawaida tu ambao ni wengi, yote kwa yote hakuna sheria ya umri….. ni kuchagua tu.
 
Umri.
Asilimia kubwa, mwanaume anaishi/anaoa mwanamke ayeendana naye kiumri. Mwanaume mwenye miaka 35+, mwanamke wa kuendana naye anakua ameshazaa

Mbona wapo ambao wanaendana nae na hawajazaa?
 
Nimeona ndoa za watu wengi zikiharibika mara tu baada ya mtoto wa baba au mama mwingine kuletwa ndani ya nyumba…..na nimekua najiuliza shida ni nn kwa ndoa za siku hizi mbona mababa zetu walilea watoto sio wao na mpaka mtu wa nje kujua ni mpaka uwe karibu na hiyo familia…

Tuna shida sehem aisee.
 
Ukiwa na hela watoto wako watapendwa tu hakuna mwanamke anaetaka kuishi kwa dhiki.
 
Back
Top Bottom