Changamoto juu ya ujenzi wa nyumba kwa tofali za kuchoma

Changamoto juu ya ujenzi wa nyumba kwa tofali za kuchoma

MUBIKU

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2014
Posts
283
Reaction score
384
Utumiaji wa tofali choma, unaweza kunipunguza gharama za ujenzi? Na nichangamoto zipi naweza kukutana nazo endapo ntafanya ujenzi huu?
 
Na kwa sisi wa Dar je? Ukiacha changamoto ya upatikanaji wake kingine?
 
Utumiaji wa tofali choma, unaweza kunipunguzi gharama za ujenzi? Na nichangamoto zp naweza kukutana nazo endapo ntafanya ujenzi huu?

Changamato ipo kubwa kwenye matumizi makubwa ya cement wakati wa ujenzi wa boma na plasta....ukizingatia kwamba inakua na joint nyingi kwenye ujenzi na wakati wa plasta ndani panakua na mahandaki hiyo wakati wakuweka ukute ukae levo cement nyingi na mchanga vitatumika
 
Ujenzi wa tofari za kuchoma ni mzuri ila hakikisha unanunua tofari zilizopigwa kwa kibao kimoja zitakazotosha nyumba nzima yaani ziwe na shape moja sio unanunua tofari zingine hapa na zingine pale (hii itakusaidia wakati wa kujenga zipangike vizuri pia hakikisha ziwe kubwa kidogo yaanizinakuwa size ya mkate wa 1000 / 1200, sio tule tudogooooooooooo).

Changamoto yake yake zinakula simenti nyingi wakati wa lipu kama ukinunua zikiwa shapeless na ndio maana nikasema ununue sehemu moja lakini pia hakikisha ukifika level ya madirisha pitisha mkanda angalau wa nondo mbili kisha endelea kama kawaida juu mpaka renta.
 
Uko wapi kwanini mkuuu?
Umeona hii mkuuu, Kwenye kona kote wanatumia sementi, katikati wanajenga kwa udogo, tofali huku kwetu Njombe zipo aina mbili, ndogondogo na kubwa.
IMG_20180726_175345.jpg
 
Changamato ipo kubwa kwenye matumizi makubwa ya cement wakati wa ujenzi wa boma na plasta....ukizingatia kwamba inakua na joint nyingi kwenye ujenzi na wakati wa plasta ndani panakua na mahandaki hiyo wakati wakuweka ukute ukae levo cement nyingi na mchanga vitatumika
Kwa sababu saruji inayotumika kwenye kozi tatu za tofari za kuchoma inaweza ikawa na saruji inayotumika kujenga kozi 7 za tofari za kuchoma japokuwa kwa upande mwingine gharama ya saruji itakuja kufidiwa na gharama za tofari za kuchoma maana kidogo zipo chini ukilinganisha na bei ya tofari ya block. Kwenye lipu ahakikishe zote zimenyooka vinginevyo lipu itakuwa zaidi ya inch moja ili kuweza kunyoosha ukuta
 
Hii kona zote tumetumia sementi kwa kujengea Ila kwa ndan katkat tumetumia tope, uko vizuri mkuuu ni rahisi mkuu
 
Ukiweka mbali upatikanaji wake, tofali za kuchoma ni imara. Zinadumu kuliko za siment. Hasa ukizingatia waandaaji wengi wapo kibiashara zaidi, mchangayiko unakua hafifu wenye kiwango kidogo cha siment.

Tofali za kuchoma hazina chemicals, inapelekea nyumba kudumu zaidi.

Niliona sehem kwa nje ukuta unapakwa kitu kama polish, matofali yanang'aa na hayachakai.
 
Utumiaji wa tofali choma, unaweza kunipunguzi gharama za ujenzi? Na nichangamoto zp naweza kukutana nazo endapo ntafanya ujenzi huu?
Kama huwleweki "sielewekii-🙂 utajibiwaje?
 
Unaweza kujengea udongo boma zima pia.
Wewe umetumia matakwa ya tofali za Hydrafom
Hii kona zote tumetumia sementi kwa kujengea Ila kwa ndan katkat tumetumia tope,,uko vzr mkuuu ni rahisi mkuu
 
Back
Top Bottom