Changamoto juu ya ujenzi wa nyumba kwa tofali za kuchoma

Changamoto juu ya ujenzi wa nyumba kwa tofali za kuchoma

Pia jitahidi uezeke mapema zisinyeshewe sana na mvua zikapoteza uimara
Hili napingana na wewe,niliwahi kutembelea kiwanda kimoja cha kuchoma tofali wakanihakikishia kuwa ikishachomwa maji hayawezi kufanya chochote,nilibisha wakanipa moja wakaniambia niweke kwenye maji siku 7 halafu niwape mrejesho,nilifanya hivyo na siku ya 7 nililitoa likiwa zima..
 
Kwa sababu saruji inayotumika kwenye kozi tatu za tofari za kuchoma inaweza ikawa na saruji inayotumika kujenga kozi 7 za tofari za kuchoma japokuwa kwa upande mwingine gharama ya saruji itakuja kufidiwa na gharama za tofari za kuchoma maana kidogo zipo chini ukilinganisha na bei ya tofari ya block. Kwenye lipu ahakikishe zote zimenyooka vinginevyo lipu itakuwa zaidi ya inch moja ili kuweza kunyoosha ukuta
Mkuu maelezo mazuri, isipokuwa umerudia maelezo ya tofari lilelile la kuchoma badala ya kulinganisha na tofari la saruji na kiwango cha matumizi ya saruji kwenye ujenzi.
 
Tofali za kuchoma ni imara na zinadumu kuliko za cement.
Kwa mikoa yenye udongo wa mfinyanzi unatumia udongo kujengea, cement inatumika kwenye kufunga mkanda na kupiga plasta ndani na sakafu.
Ujenzi wa tofali za kuchoma ni wa gharama nafuu
 
Vipi kuhusu tofali za hydro..
 
Ujenzi wa tofari za kuchoma ni mzuri ila hakikisha unanunua tofari zilizopigwa kwa kibao kimoja zitakazotosha nyumba nzima yaani ziwe na shape moja sio unanunua tofari zingine hapa na zingine pale (hii itakusaidia wakati wa kujenga zipangike vizuri pia hakikisha ziwe kubwa kidogo yaanizinakuwa size ya mkate wa 1000 / 1200, sio tule tudogooooooooooo). Changamoto yake yake zinakula simenti nyingi wakati wa lipu kama ukinunua zikiwa shapeless na ndio maana nikasema ununue sehemu moja lakini pia hakikisha ukifika level ya madirisha pitisha mkanda angalau wa nondo mbili kisha endelea kama kawaida juu mpaka renta.
Yaani ziwe kama hivi hapa down utapenda 👇👇
 
Hizi naona ni nzuri
[emoji116][emoji116][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my cupboard using mug
 
Mchwa ni shida aisee kwa hio nyumba
Yaani unaweza liona dirisha linapukutika hivi hivi
 
Mchwa ni shida aisee kwa hio nyumba
Yaani unaweza liona dirisha linapukutika hivi hivi
Heee kumbe, navyooenda nyumba hizo mbona navunjika moyo sasa, na hakuna jinsi ya ku Zuia mchwa
 
Tofali za kuchoma ni imara na zinadumu kuliko za cement.
Kwa mikoa yenye udongo wa mfinyanzi unatumia udongo kujengea, cement inatumika kwenye kufunga mkanda na kupiga plasta ndani na sakafu.
Ujenzi wa tofali za kuchoma ni wa gharama nafuu
Mkuu mbona naskia zinavutia sana mchwa
 
Utumiaji wa tofali choma, unaweza kunipunguza gharama za ujenzi? Na nichangamoto zipi naweza kukutana nazo endapo ntafanya ujenzi huu?
Natumaini ulimaliza kibanda chako Mkuu. Kama bado changamoto mojawapo ni mchwa. Wana tabia ya kupanda ndani kwa ndani hadi kulifikia paa na kuliharibu. Kuzuia hilo, tumia mortar (cement) badala ya udongo kuunganisha tofali.
 
Duh mbona shida sasa nilijipanga kujengea tofari za choma
 
Lakini unaweza kujengea udongo mpaka wataki wa kufunga renta baada ya hapo ukajengea cement zile kozi za kutoka kwenye renta
 
Uganda wanachoma kwa matanuri ya gas, tofauti hata upige shoka liko imara. Tatizo ni gharama za usafiri kutoka Uganda. Fikiria unajenga nyumba Mtwara yote matofali Uganda.
 
Uganda wanachoma kwa matanuri ya gas, tofauti hata upige shoka liko imara. Tatizo ni gharama za usafiri kutoka Uganda. Fikiria unajenga nyumba Mtwara yote matofali Uganda.
Kwan bong bad hawajapatikan wataalam wa kudesing vibao vya interlocking block naona zile za kuchona zikitengenezwa kwa stail hiy itakuwa bomba san
 
Lakini unaweza kujengea udongo mpaka wataki wa kufunga renta baada ya hapo ukajengea cement zile kozi za kutoka kwenye renta
Huo Ndio ujenzi uliopo huku rukwa
Msingi wa tofari za kuchoma au mawe unajengewa kwa tope, kisha wanajengea kwa tope mpk renta wanafunga renta wengi wanaendeleza na tope wengi wanatumia cement..! Ujenzi ni nafuu ukitaka na ni gharama ukipenda, kabla ya kujenga tafuta ramani nzuri, kisha tafuta fundi au maalumu wa ujenzi akupe makisio ya matilio yakakayotumika+ bei za mafundi, fanya window shopping, wewe mwenyewe kisha nunua vifaa, booom utajikuta unajenga kwa bei Nafuu.!
 
Back
Top Bottom