Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Ripoti ya Deaf Women Included iliyochapishwa 2021 ilifanya utafiti na kugundua, Asilimia kubwa ya watoto wanaopatwa na changamoto ya uziwi mara nyingi huwa wahanga wa ukatili katika jamii kwa sababu wanaoamua kuwafanyia ukatili hujua hawawezi kusema.
Inahitaji ufuatiliaji wa karibu kufahamu kama mtoto kiziwi anafanyiwa ukatili kwa sababu familia nyingi huwatenga Watoto viziwi na jamii. Watoto viziwi wana changamoto Zaidi katika kuwasilisha mashitaka polisi au kwa mamlaka nyinginezo kwa sababu ya watoa huduma kutokufahamu lugha ya alama.
Watoto viziwi wanaofanikiwa kupelekwa shule maalumu, huwa na uwezo wa kueleza ukatili wanaofanyiwa kwa walimu wanaoelewa lugha ya alama na shule huchukua hatua za kisheria.
*Jamii ina wajibu wa kutoa msaada gani kwa mtoto mwenye ukiziwi:
FUWAVITA inahimiza wanajamii, maafisa afya na viongozi wa maeneo husika kutambua uwepo wa Watoto viziwi na kufuatilia kwa karibu maendeleo yao ili kukomesha ukatili dhidi yao.
FUWAVITA inaishawishi serikali kuweka watoa huduma wenye ujuzi wa alama ya lugha katika huduma za umma ili waweze kuhudumia kundi la viziwi na hasa Watoto viziwi.