Changamoto kwa watumishi walioko vijijini kufanya biashara

Changamoto kwa watumishi walioko vijijini kufanya biashara

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,104
Reaction score
1,924
Unajua, kuwa mtumishi wa umma, haimaanishi utaishi kwa kutegemea mshahara tu, inabidi ujishughulishe either na biashara au kilimo. Kilimo kwa mtumishi inawezekana lakini kwa kutegemeana na eneo husika.

Watumishi wengi wanakuwa wanakimbilia kufanya biashara ili angalau kuongeza kipato chao. Iwe biashara ya nafaka au bidhaa za dukani, watumishi Hawa wanapitia changamoto nyingi sana, miongoni mwake ni:-

1. Pressure ya mikopo; ukiwa kijijini na ukaanzisha biashara kwa kutegemea mtaji utokanao na mkopo, inawafanya watumishi kutumia nguvu sana kwasababu tayari mshahara wake ulishapungua, na unakuta biashara za vijijini ni za vipindi ,haswa kipindi cha mavuno tu ndiyo biashara zinachangamka, baada ya msimu, doro linasababisha mitaji kushuka.

2. Ufanisi mdogo kwenye kazi mama kwasababu ya kusimamia biashara maana siyo rahisi kuajiri mfanyakazi wa kukusaidia kwa nature ya mazingira ya kijijini na mzunguko wa biashara

3. Fursa finyu/ chache za kibiashara; kijijini unaweza ukawa na mtaji lakini ukashindwa kufanya biashara kwasababu ya idadi ndogo ya watu, au utajikuta unafanya biashara ile ile inayofanywa na wajasiliamali wa vijijini. Hii inadumaza watumishi katika kuongeza na kukuza mitaji, na wengi wanajikuta kuishia kuwa wafugaji au wakulima tu.

4. Uchawi na kulogeana biashara; kwasababu mtumishi anapoanzisha biashara kijijini, anaonekana kuwa ndiye tajiri, kumbe naye amejikopea tu ki mtaji chake, na kama tujuavyo, unapoonekana una uwezo zaidi kijijini, hakika uchawi na ulozi utakuandama, utajikuta unatumia muda mwingi either kusali sana au kutafuta waganga sana, hii inaathili biashara za watumishi

5. Kukopwa na kuzulumiwa; hii inatokana na ujamaa ulioko vijijini, Kuna wazee wenye heshima zao kabisa, kiasi kwamba akiomba kukukopa unashindwa kukataa, na kiuhalisia vipato vyao haviaminiki, kwahiyo suala la kuzulumiwa au kishindwa kulipwa linatokea mara kwa mara.

Hivyo basi, nivizuri kwa watumishi ambao hawajajiingiza kwenye biashara haswa walioko kwenye mazingira ya vijijini kutulia kabisa kabla ya kujiingiza kwenye biashara. Ni kheri kabisa kujikita kwenye ufugaji na kilimo kuliko kuforce kufanya biashara kijijini
 
Kwa wenye ndoto za kufanya biashara na kukua ajira za hivyo huwa zinazima ndoto zao jumla wanakuja kushtuka kipindi cha mafao na wengi wao wakiingia kwenye biashara baada ya kustaafu zinakufa.
 
Back
Top Bottom