KERO Changamoto shule ya msingi Kimandafu Halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha

KERO Changamoto shule ya msingi Kimandafu Halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyerereog

New Member
Joined
Oct 16, 2024
Posts
3
Reaction score
204
Pale Arusha wilaya ya Arumeru hasa Halmashauri ya Meru shule ya msingi Kimandafu kuna mzungu anaitwa Birgita sijui ametokea nchi gani. Huyu mama anatoa vifaa kadhaa vikiwemo vitabu, chakula km unga, chereko, mchele, mafuta ya kupikia. Jambo la kwanza huyu Birgita serikali inamfahamu? Pili ukweli ni kwamba misaada wanagwana mwalimu mkuu aitwae Laizer na walimu wenzake. Swali, kwanini mzungu atumie taasisi ya umma kulaghai? Uongozi wa Halmashauri ya Meru uko wapi kuruhusu huu ubaradhuli? Kwanini shule yetu itumike na watu km hawa kufanikisha mambo yao. Kuna mambo ya siri kati ya mwl. Mkuu na Birgita. Umetolewa msaada wanafunzi wapate lishe bora badala yake wanagawana walimu wenye mishahara watoto wanalishwa makurukuru yaani makande machafu hata hayakobolewi. Hii ni taarifa serikali ifanyie kazi kabla wananchi hawajachukua hatua
 
Back
Top Bottom