KERO Changamoto utoaji huduma Safi Shule ya Makabe

KERO Changamoto utoaji huduma Safi Shule ya Makabe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wewe unazungumzia Kayumba za kijijini kwenu Huko unapoishi wewe
Jana kuna mdau kaposti shule ya msingi Sinza, uliona picha ya majengo? Au sinza ipo kijijini kwenu?
 
Hii shule imekua shule ya hovyo sana kwa sasa kwenye utoaji huduma. Kwanza nikiri kilichonisukuma kuleta huu uzi ni upuuzi wao waliotufanyia wazazi hii January kutopokea watoto ambao hawajalipa ada yote.

Hapa ndio wametukera wazazi, hivi kweli mzazi unalipa laki 5 January hii na wanagoma kumpokea mtoto? Kweli? Halafu tena hapo umewafuata na kuwaomba ada utaongezea mwisho wa mwezi January na bado wanakataa, really?

Huu ni utapeli mkubwa,imagine ni wazazi wangapi wamelipa pesa nusu na bado watoto wamerudishwa the whole of January hawajasoma meanwhile pesa zetu wamepokea zinaendelea kutumika kwenye shughuli zao. Na wanaona kabisa malalamiko ya wazazi kwenye WhatsApp groups ila full madharau. Hii ni fair? Sometimes wakipokea watoto ambao wanadaiwa ada wanaenda kuwafungia TV room siku nzima, hivi hii ni akili kweli?

Hii shule kwa sasa wamekua wabinafsi mno na hawajali kabisa other stakeholders na ndio maana hata ada wanapandisha kiholela sana. Bora huduma yao ingekuwa standard tusingelalamika,ila sasa kwa huduma zao zilivyo za kawaida mnatufanyia wazazi maringo kiasi hiki? Magari mabovu,walimu turnover kubwa kila mara mnaleta wapya,vitabu mnatoa mwisho wa muhula,chakula kibovu watoto hadi wanalalamika kukuta mende na buibui kwenye chakula na bado hatukuamua kuwaexpose ili kuwalinda mu-improve.

Shule kama hizi ndio zinafanya shule za kulipia zionekane mzigo mzito wakati si kweli. Bahati mbaya nimeshindwa kumhamisha mtoto sababu yupo darasa la mtihani, ila next year hamnioni namhamisha mapema sana maana hamna upeo wa kuona value for money,na consideration kwa wazazi ambao ni stakeholders wakubwa. by the way sishauri upeleke mtoto wako hapo.
Hakuna usajili uliofanyika bado. Acha visingizio hamisha au lipa ada. Muda wa usajili ni February na March.
 
Neenda ukaongee na mualimu mkuu umueleze kinacho kusibu kuliko kuja huko mtandaoni, nawenyewe ni binaadamu wanasikiliza, kusomesha mtoto EMs onahitaji moyo determination uvumilivu na sacrifice, otherwise utampeleka kwenye hizo shule za wakina LIKUD za kupoteza mda wa watoto.
Soma uzi uelewe vizuri, unadhani kwanini nimeleta uzi hapa?
 
Kinacho msumbua hataki kujishusha mbele ya mkuu wa shule kwamba hana pesa apewi mda bado ana ile mentality ya shule za Kayumba, ile ni private capital ya mtu yeye ndo anajua uchungu ya pesa yake na machu gu yake.
Soma uzi uelewe usikurupuke kucomment..kila kitu nimeeleza
 
Mkuu hio ni biashara ya mtu. Lipa ada mtoto asome. Kuna shule za akina LIKUD ukiona ada mzigo mpeleke huko.
Elimu ishakuwa biashara hakuna namna.
Kuna mahali nimesema sijalipa ada? Laki 5 ni ndogo kwa mtoto kusoma wiki mbili hadi mwisho wa mwezi? Hata kama ni Biashara inategemea unaendeshaje...na mteja ndie anaefanya biashara iende...kama unadhani wazazi wakiamua wanashindwa ulizia kuna shule inaitwa Aureke kilichowakutaga hadi leo wanahaha maana hadi shule ilisimama
 
Kuna mahali nimesema sijalipa ada? Laki 5 ni ndogo kwa mtoto kusoma wiki mbili hadi mwisho wa mwezi? Hata kama ni Biashara inategemea unaendeshaje...na mteja ndie anaefanya biashara iende...kama unadhani wazazi wakiamua wanashindwa ulizia kuna shule inaitwa Aureke kilichowakutaga hadi leo wanahaha maana hadi shule ilisimama
Lipa ada mtoto aende shule. Wenye shule si wamekataa nusu ada? Acha kulazimisha mambo yaende utakavyo.
 
Lipa ada mtoto aende shule. Wenye shule si wamekataa nusu ada? Acha kulazimisha mambo yaende utakavyo.
Hivi mada mnaielewa lakini au mnaandika kuonekana mnajimudu. Mimi nasomesha watoto shule 3 tofauti na wote nimewalipia laki 5 kila mmoja January hii ila hao wengine wawili shule zao hazijanifanyia ujinga na ndio maana nimeleta uzi hapa sababu pia kwenye group la shule la WhatsApp wengi ni victims (akiwemo ndugu yako). Na huwa nafanya hivyo kusomesha watoto shule tofauti kuepuka ujinga wa shule moja. The reason why ntamuhamisha na huyu,na sababu si ada tu bali hizo kero zingine nilizozitaja japo we umeona tatizo ni ada tu
 
Sawa mwalimu mkuu wa Safi School.. asante kwa ushauri
Usilalamikie kit unachoweza kukifanya. Ni unaamka asubuhi unaamua maana hata siku ya kumleta mtoto uliamka ukagonga geti mwenyewe. Hukulazimishwa kumpeleka so kwa nini uanze visingizio kwenye kumtoa???
 
Usilalamikie kit unachoweza kukifanya. Ni unaamka asubuhi unaamua maana hata siku ya kumleta mtoto uliamka ukagonga geti mwenyewe. Hukulazimishwa kumpeleka so kwa nini uanze visingizio kwenye kumtoa???
Hii post sio kwa ajili ya wewe kutoa ushauri,bali ni ili wahusika ujumbe uwafikie. You sound more like a thoughtless moron kukomaa kuchangia uzi usiokuhusu
 
Huwezi jua pengine mwenye shule yuko desperate anamadeni ya kufa mtu na marejesho yanampasua kichwa unadhani hatakukazia ulipe ada kama mlikubaliana kwenye form ya mwisho(ilieleza usipokalimilisha ada mwanao hatapokelewa)..akilega tu soon anakuwa kama owner wa canosa..huruma inaponza unakuwa mshumaa kuwahurumia walipa ada ambao walijua jukumu lililo mbele yao Jan wakawekeza kwenye sikukuu wakajiachia wakatafuna hadi ada akati ukidhalilika kidogo wanahamisha watoto wao ASAP,uendeshaji wa shule ni gharama bila kukomaa wamalize ada kikibuma tu bado lawama juu yako mmiliki na fedheha juu.
January sio Ajali kwamba hujui nn unatakiwa kufanya kwa wanao tuwe na desturi ya kuhold na skip matumizi yasiyo yalazima au laa lipa ada fanya maandalizi Dec kuepuka fedheha hizo.
 
Back
Top Bottom